Utunzaji wa taka ni mbovu sana Kawe - Mzimuni, zinazagaa ovyo Mitaani, hii ni hatari kwa afya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Mimi ni mkazi wa Kawe - Mzimuni karibu na Shule ya Ali Hassan Mwinyi, kwa muda wa wiki yote hii kama sijakosea ni kuanzia Jumapili (Machi 17, 2024) nimeshuhudia taka zikizagaa mitaani tena nyingine zikiwa katikati ya Barabara.

Mazingira ya utunzani taka mtaani kwetu ni ya ovyo sana, hili tumelalamika muda mrefu lakini hatua hazichukuliwi, sasa baada ya kuona tumekuwa kimya wameamua kutupa taka barabarani na Serikali ya Mtaa ipo kimya tu.

Hii ni hatari kwa afya, kwa wapita njia na hata kwa sisi wakazi wa Kawe, kibaya zaidi kuna Watoto wamekuwa wakipita na kuanza kuokota baadhi ya vitu kwenye takataka hizo.

photo_2024-03-20_09-33-35.jpg

photo_2024-03-20_09-33-31.jpg

photo_2024-03-20_09-33-26.jpg

Zoezi la kuzoa taka lafanyika - Hatimaye wazoaji taka wametimiza wajibu wao kwa kuzoa taka Mtaa wa Mzimuni - Kawe
 
Wewe ndio mkazi halisi wa kawe unaleta kero halisi za kawe na picha unaweka sio yule popoma anaishi huko Bunda vijijini hajawahi kufika hata Dar maisha yake yote tangu azaliwe lakini kila siku kujichocha kujifanya yupo Kawe.

Anyways I hope wahusika wataona kero hiyo na wataishughulikia mara moja.
 
Mimi ni mkazi wa Kawe - Mzimuni karibu na Shule ya Ali Hassan Mwinyi, kwa muda wa wiki yote hii kama sijakosea ni kuanzia Jumapili (Machi 17, 2024) nimeshuhudia taka zikizagaa mitaani tena nyingine zikiwa katikati ya Barabara.

Mazingira ya utunzani taka mtaani kwetu ni ya hovyo sana, hili tumelalamika muda mrefu lakini hatua hazichukuliwi, sasa baada ya kuona tumekuwa kimya wameamua kutupa taka barabarani na Serikali ya Mtaa ipo kimya tu.

Hii ni hatari kwa afya, kwa wapiti njia na hata kwa sisi wakazi wa Kawe, kibaya zaidi kun Watoto wamekuwa wakipita na kuanza uokota baadhi ya vitu kwenye takataka hizo.

Duh inasikitisha sana alafu Kila mwisho wa mwezi wanataka buku tatu za kutoa uchafu wakati taka hawatoi
 
Wewe ndio mkazi halisi wa kawe unaleta kero halisi za kawe na picha unaweka sio yule popoma anaishi Tunda vijijini hajawahi kufika hata Dar maisha yake yote tangu azaliwe lakini kila siku kujichocha kujifanya yupo Kawe.

Anyways I hope wahusika wataona kero hiyo na wataishughulikia mara moja.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom