Taasisi ya Jafari Chege Foundation (JCF) Yaendesha Kampeni ya Ondoa Paa la Nyasi Rorya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

TAASISI YA JAFARI CHEGE FOUNDATION YAENDESHA KAMPENI YA ONDOA PAA LA NYASI RORYA

Mbunge wa Jimbo la Rorya ambaye pia ni Muasisi wa Taasisi ya JAFARI CHEGE FOUNDATION (JCF) ameendesha Kampeni Maalumu Jimboni Rorya ya kuondoa Paa la Nyasi kwenye nyumba za Wanawake Wajane, Wazee na Wenye Ulemavu inayokusudia kuboresha makazi.

Mpango huu umerejesha matumaini mapya kwa wananchi baada ya kushuhudia nyumba zikijengwa na kuwaondoa katika mazingira magumu waliyoishi kabla ya Mpango huo kuanza

"Huyu mtoto mimi sijui lakini msaada unafanya vizuri kwa Mungu na kwa Yesu. Lakini mimi hata kitu sina. Nimeshukuru Mungu Baba. Mimi nakaa hapa Kijijini hata mtoto sina" - Mama ambaye ni Mnufaika wa JAFARI CHEGE FOUNDATION (JCF)

"Tumefanikiwa kujenga nyumba kama inavyoonekana na tunaendelea kutoa ahueni kwa familia ambazo awali hawakuwa na nyumba zenye paa la bati kama hizi katika mpango wa kujenga nyumba kwa Wajane, Walemavu pamoja na Wazee wasiojiweza. Mpango ni wa kujenga nyumba tatu (03) kwa kila Kijiji.
 
Back
Top Bottom