Bhikalamba
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 1,706
- 2,353
Siyo kweli kwamba vitabu vya kiada (T.I.E) vina kila kitu au vinajitosheleza kwa kila eneo au mada ndo maana tuna vitabu vya ziada na rejea.Kabla hujasema NONESENSE kwa vitabu vya TIE jiulize, mwenye jukumu la kuandaa mtaala ni nani? Na umeangalia mitihani ya NECTA ukakuta iko nje ya vitabu vya TIE?
Mi nafikiri tupime usharo wa vitabu vyao kwa kuangalia mitihani na marking scheme za mitihani ya NECTA Kama ziko nje ya vitabu vyao ndio tuwahukumu
Syllabus ndo inamwongoza mwalimu ni kipi kinapaswa kufundishwa na kipi hakipaswi kufundishwa wala si kitabu. Kitabu ni sehemu ya kufanyia rejea anapo andaa notes pamoja na kuongeza maarifa, kuhusiana na mada tajwa ndani ya syllabus. Kuna mengi yaliyo kwenye kitabu lakini yanaweza yasiwe ndani ya syllabus au kuna yaliyoelekezwa kwenye syllabus lakini usiyakute kwenye text books badala yake unayakuta kwenye reference books.
Ndiyo maana T.I.E pamoja na kuandaa text books huwa wanatoa ithibati kwa vitabu vingine vilivyo hakikiwa kutumika mashuleni kama vitabu vya rejea.
Nikirudi kwa mtoa mada, huenda baada ya ukaguzi wamekuta mnatumia vitabu ambavyo havina ithibati, yaani havijathibitishwa rasmi kutumika kama vitabu vya kufundishia mashuleni. Hii hufanyika ili kuepuka kuwa na vitabu vilivyo na makosa ya kiuandishi au vyenye maelelezo hafifu na yaliyojaa makosa ili kuepuka kumpotosha mwanafunzi au kuleta mkanganyiko kwa walimu. Tafadhalini zingatieni sheria