Taasisi ya Elimu ichunguzwe

Taasisi ya Elimu ichunguzwe

Mimi ni mzalendo ila Sina imani na elimu ya Tanzania,,,. Sionagi ata inamsaidia nin mwanafunzi... Ningekuwa na fwedha watoto zangu ningewasomesha ulaya tu... Tatizo ukwasi
 
Ndalichako ana akili za kujibia mitihani tu .ila akili za kuongoza na kudadavua mambo kama hayo hana hata kidogo ilo niseme wazi pasi na chuki yeyote .
 
Please please please mheshimiwa Professor Ndalichako Mama yangu na Mwalimu wangu ninayekuheshimu mno, Bado naamini you are very smart na si sehemu ya ufisadi na ulafi wa taasisi ya elimu.

Unda tume huru uchunguze uozo na ulafi wa mkurugenzi wa taasisi ya elimu na kundi maslahi lake.

Wanaiumiza Tanzania, wanaua ekimu ya Tanzania, Wanaua reading culture makusudi ili wafanye biashara ya vitabu vyao.
 
TIE ni janga! Kila muda unavyozidi kwenda vitabu vyao havina tofauti na machapisho ya Fema
 
Taasisi ya elimu imeacha jukumu lake la msingi la kutunga na kusimamia mitaala sasa imejawa na uroho na tamaa ya fedha na biashara haramu.

Wanalazimisha shule binafsi zitumie vitabu vyao ambavyo ni below standard.

Wanahonga wakaguzi (wadhibiti ubora) na kuwatumia kufanikisha biashara yao haramu.

Wakaguzi wanapita shule za English medium kunyanyasa wenye shule na kuwaamrisha wakusanye na wachome moto vitabu vyote ambavyo si vya taasisi.

Tunahimiza reading culture lakini taasisi ya elimu wanadiscourace reading culture ili wauze vitabu vyao pekee.

Wanefikia hatua kulazimisha shule binafsi English medium wanunue log book, attendance register walizoziprint wao huu ni uhujumu uchumi.

Hawalipi Kodi wanafanya biashara ya mabilioni pesa zote zinaliwa na mkurugenzi wa taasisi ya elimu akishirikiana na kundi lake maslahi

Waziri Ndakichako ulikuwa mwalimu wangu UDSM very smart indeed nakuheshimu daima

Mama you are so smart please unda tume haraka kuchunguza upuuzi unaofanya na mkurugenzi wa taasisi ya elimu ba kikundi maslahi chake

Wanaihujumu elimu na wanaihujumu Tanzania

Wanatumia ofisi ya Umma kwa maslahi binafsi

Please please please mama yangu Ndalichako na mama yangu Samia Suluhu Hassan nawapenda na kuwaheshimu sana .

Taasisi ya elimu wanawachafua na wanawakosea adabu mno

Please please taasisi ya elimu ni jipu
Mkuu achana na maisha ya udalali ya vitabu vya watu binafsi utaondokana na haya maisha ya kulalamikia watu hovyo.
 
Hao taasisi. ya elimu ni ngumu kuwajibishwa kwanI hakuna kitu. kinaendelea pale bila serikali kujua ukweli maana AFISA VIFICHO na VIPENYO wako tele pale,ni kwamba pesa nyingi zilizotolewa na wafadhili kuboresha elimu serikali haitaki zitoke nje na ndio maana taasis hiyo ina tumika kuua kampuni binafsi za publicatons wakipeleka vutabu kupata ithibati havipiti na ada ikapandishwa. pia tangu lini mshindani wako akawa ndio mkagua viwango ?wakati mwenyewe vitabu vyake havina kiwango? kumbuka katibu mkuu mshikaji wa mwendazake alikuwa pale kama mkurugenzina ndio master mind na baada ya kuharibu pale akapelekwa kuwa katibu mkuu. akaja Kibuga wakamtoa na huyu mama aliyepo ndio simuelewi hata anachofanya
 
Mkuu achana na maisha ya udalali ya vitabu vya watu binafsi utaondokana na haya maisha ya kulalamikia watu hovyo.
kama kweli wako vizuri basi uwepo mfumo huru wa kushindanisha tenda kama zenji na kitabu kizuri kipite na kama wao wako vizuri basi watashinda
 
macmilan haipo kwa sasa lakini vitabu vyao vilikuwa vizuri pia EMAC ilichangia kutokana na usisiamzi wake licha ya changamoto ya tuhuma za ruhswa
Mimi binafsi nimetumia vitabu vya MACMILLAN nikiwa elimu ya kidato cha nne na kidato cha sita.

Vitabu vya MACMILLAN ni vizuri sana, hata hawa TIE wenyewe huwa kuna vitu wanachukua kutoka huko.

Ukitumia vitabu vya MACMILLAN kwenye PRACTICALS za Physics, Chemistry na Biology majibu yake ndio huwa yanapatikana huko kwenye hivyo vitabu.

Sasa sijafahamu ni kwanini sasa hivi, hivi vitabu vya MACMILLAN havipatikani.
 
Hizi taasisi za serikali zilikuwa zimepewa mandate ambazo siyo zake wakati wa utawala wa mwendazake. Mwendazake alikuwa anawaza kizamani mno! Alitaka kuturudisha kwenye sera za kijamaa ambapo serikali inafanya kila kitu,mpaka kichunga ng'ombe!

Ni wakati muafaka sasa,taasisi za serikali zibaki kwenye majukumu yake. Waache kabisa kuchezea kodi zetu kufanya biashara. Shughuli hiyo hawaiwezi! Waache sekta binafsi ifanye biashara. Serikali ikusanye kodi.
 
Sasa sijafahamu ni kwanini sasa hivi hivi vitabu vya MACMILLAN havipatikani.
[/QUOTE]
MACMILLAN ilikuwa kampuni ya Uingeleza walipofunga shughuli zao na Kuza umiliki kwa hapa nchini vitabu vichache vilivyokuwa vimebaki vilikuwa chini ya Macmillan Aidan ambayo ilikuwa inamilikiwa khalaf rashid kama sikosei naye alilazimika kuifunga baada ya serikali kuamua kuwa inanzalisha yenyewe vitabu maana kwa miaka zaidi mitatu alikuwa analipa wafanyakazi bila kuuza akiwa na imani labda serikali itabadili uamuzi iwe soko huria ,si yeye tu bali makampuni mengi yamekufa huku yakiacha mamia ya watu wakiwa hawana ajira na hata industry yenyewe iko mahututi kama haijafa kabisa ingawa wao husema chenji ya rada ilichangia wao kuja kupokwa uzalishaji na utayalishaji wa vitabu vya kiada
 
Acha kudanganya watu. Hivi umeshasoma utumbo uliomo kwenye vitabu vya TIE.

Kwenye Maths form 1 topic ya Inequalities haipo, walimu tynalazimika kuifundisha kwa kuwahurumia watoto.

Herufi O kwenye BODMAS wanasema ni Open Bracket wakati ni Of hata uki Google utawaumbua.


Halafu Division by Number Line wanasema it is impossible wakati ni it is possible bali ni ukilaza wao..

Mtoto anaingia firm 5 hajui neno parabola kwa sababu ya vilaza wa TIE.

Physics ya TIE huwezi kuilinganisha na ya kwenye Abbot hata chembe.

Kimsingi TIE imeua elimu na vilaza wengi kama wewe hamlijui hili.
Nimewadanganyaje watu?!! Soma vizuri hoja yangu, kimsingi mi sijasema vitabu vya T.I.E viko vizuri sana au kwamba vinajitosheleza. Rudia kusoma vizuri uelewe hoja yangu.
Pia naomba upitie mchango wa fazaksd (thread #35) kwa uelewa zaidi, kama hukuelewa maelezo yangu uliyo quote (thread #21)
 
Back
Top Bottom