BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,050
- 10,489
Kwanza napenda kutoa shukrani kwa muumba na pia kwa wale wote waliofanikisha Mimi Baba Morgan kupata hii kazi kwenye moja ya kampuni maarufu hapa nchini japo nipo katika ngazi ya chini ila sina budi kushukuru maana ni bora kidogo kuliko kukosa kabisa.
Napenda kutumia fursa hii kuwakumbusha waajiri wa makampuni makubwa kujali maslahi ya wafanyakazi wao kama vile wanavyojali brand name zao, yaani ukubwa wa kampuni uendane na uwezo wa uchumi wa mfanyakazi.
Mimi kule kwetu Namtumbo wanajua nimeajiriwa kwenye taasisi kubwa ila wanapata wakati mgumu na kupelekea kuulizwa maswali ambayo hata mimi binafsi yananiumiza kama vile ni wapi napeleka pesa maana sina maendeleo yoyote na ninapoombwa msaada nakuwa mgumu kusaidia.
Mwisho, nipende kuwakumbusha ndugu zetu sio kila anaefanya kwenye taasisi hizi kubwa ana wadhifa mkubwa; wengine tupo kwenye ngazi za chini kabisa ni vibaraka hatuna kitu mfukoni, tupo tupo tu tunasubiri kuiona kesho.