Pendekezo binafsi na maoni kwa makampuni yanayoajiri madereva

Rayze

New Member
Sep 6, 2022
1
0
Habari..
Msininukuu vibaya na SIONGELEI WALA SIINGILII MIFUMO ya makampuni ila ni Maoni tu kama dereva kwasababu kuna vitu vinatukatisha tamaa sana baadhi ya madereva wenye uzoefu wa miaka 0-5

Nitaongelea hususani kwa makampuni ya usafirishaji yanayo husisha magari makubwa ya mizigo (Heavy Duty/Goods Vehicle)nitaongelea vitu viwili vikubwa kwa upande wangu.

1. Makampuni yaache kuogopa kuajiri madereva wa magari makubwa wenye Ngazi tofauti za Elimu.
Makampuni yanatakiwa yawe yenye fahari kupata watu wenye ngazi tofauti tofauti za Elimu na ziwape nafasi watu wote zisijikite sana kwenye ngazi tulizo zoea Mfano form 4 na STD VII.

Kama Dereva amevuka vigezo unavo hitaji Kwenye kampuni basi nae apatiwe nafasi ya kupitiwa kama anafaa kwa kazi tajwa sambamba kama wale wa vigezo kamili kwa sababu unaweza ukatoa vile vigezo vya juu vilivo zidi na kuacha kigezo cha kampuni na akifaa apewe vigezo na masharti kulingana na hitaji la kampuni sio kumuacha kabisa.

Kuna baadhi ya kampuni mkipeleka watu 10 CV yani kuna form4 tisa na degree mmoja na wote mkawa sawa sawia na mkafanya vizuri sawa wote kuna uwezekano Tisa wa form4 watachukuliwa ila 1 wa degree ataachwa hata kama ni Dereva mzuri vipi au unauzoefu vipi (msininukuu vibaya). Wakati uyo wa degree pia ana uhitaji wa kazi na anaweza kupokea masharti yote kama yule wa form 4.

Naongea hivi kwa sababu mimi mwenyewe kuna baadhi ya changamoto napitia kama dereva ni dereva wa magari makubwa nina uzoefu nina degree na nimejiendeleza kozi NIT HGV lakini changamoto ni nyingi hususani likija swala la Elimu yangu na mda mwingine inanilazimu kuwaza kudanganya elimu niseme elimu ndogo ili tu nifikiriwe katika kazi wakati natakiwa kujivunia kile nilicho nacho kama dereva.

Makampuni tuwape sapoti madereva wote wa ngazi zote kwa kuwapa masharti yenu.
Na ndio maana vyuo mbali mbali vya taaluma ya udereva hapa nchini mfano NIT ukitoa vigezo vyao vya muhimu haichagui wala haibagui una ngazi gani ya elimu unapoenda kusoma kozi pale imewapa uhuru ngazi zote za elimu kwa kufwata masharti yao muhimu.

Pia inaeleweka kuna madereva wenye uzoefu mkubwa sana wenye ngazi tofauti za Elimu na Mafunzo kutoka vyuo tofauti


2. Uzoefu kazin katika kuomba kazi.
Uzoefu ni kitu muhimu na kizuri kazini, kwa madereva wa magari makubwa ni muhimu kwasababu mizigo au bidhaa zinachangamoto yake ki uhalisia na ki gharama ndo mana kampuni inapo mpa gari dereva asafirishe mzigo wa Mil. 100 au zaidi inamaanisha dereva amepewa dhamana kubwa na imemuamini.

Ila kuna madereva wanaotokea kwenye hizi Small Local Hire yani taasisi ya chini ya kuajiri na amefanya kazi miaka mi5 labla huwa wanapataga changamoto sana wanapo tafuta cheti cha uthibitisho wao wa kazi walipo toka kwa sababu ya mfumo wa kazi yao mfano Mwajiri ana Semi-trailer 1 tu ya kokoto au mchanga na hana ofisi yani yeye anaenda kupakia kwa oda maalum ya mtej na wew ndo dereva yani ukiondoka apo huwez pata cheti cha uthibitisho wa kazi na hata kupata barua ya uthibitisho pia inaweza kua changamoto.

Hivyo Makampuni ya simamie vigezo vyao na pia iwazingatie hawa ambao ni madereva wazuri ila wanakosa vyeti vya uthibitisho wa kazi.
Na kwaku sapoti hilo kama wanakidhi vigezo vingine vya kampuni wapewe test ili kupima uwezo wao kama wanavo dai ili kuthibitisha ilo.

Pia naamini kuna madereva wazoefu sana na wa mda mrefu Kazini wenye Elimu tofauti na ujuzi kutoka vyuo tofauti. Naamini madereva hawa wazoefu wanawe kupewa madereva wenye uzoef kias au wapya ili wawafundishe kazi na kishauriana kwa masharti ya kampuni kwamba kampuni iandae madereva wanao wataka kwa kiwango chao ili kusaidia na hawa wapya kupata nafasi ya kichangia nguvu kazi katika kampuni. Pia makampuni yasisitize madereva wakaongeze ujuzi kwenye vyuo vya ujuzi vya uderewa wa juu au kuwapelekea mafunzo makazini kwa aajili ya manufaa ya wote.
 
Kumbe siku hizi kuna degree ya udereva?

Ninachojuwa kazi ya driving kinachohitajika ni driving licence na cheti cha veta au NIT hayo ndio mahitaji muhimu, ziada kwenye maofisi ya kisiasa ni basic computer course na kuwa fluently kwenye English and Swahili.
 
Kweli sasa naamini Kuna watu wengi wana vyeti ila hawajaelimika kabisa.
Kaz ya udereva alaf upeleke degree ya ualim itakusaidia nini? We fata vigezo na masharti hakuna anaetaka kujua kuhusu elim yako umeambiwa leta chet cha form 4 na driving license peleka hivyohivyo ulivyotumwa
 
Kumbe siku hizi kuna degree ya udereva?

Ninachojuwa kazi ya driving kinachohitajika ni driving licence na cheti cha Beta au NIT hayo ndio mahitaji muhimu, ziada kwenye maofisi ya kisiasa ni basic computer course na kuwa fluently kwenye English and Swahili.
Soma uelewe mkuu.. Halafu beta ndio kitu gani??
 
Back
Top Bottom