Taarifa za intelijensia zilizovuja yaweka wazi uhusika wa Marekani katika suala la Ukraine

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111432763435.jpg

Vyombo vya habari vya nchini Marekani vimeripoti kuwa, nyaraka kadhaa za jeshi la Marekani zimevujishwa kwenye mitandao ya kijamii, zikiwa na taarifa kamili kama vile ramani ya Ukraine na sehemu ambazo askari wake wako na aina ya silaha walizonazo.

Moja ya nyaraka hizo imeandikwa “Siri Kuu” na ina kichwa cha habari kinachosema “Hali ya Vita mpaka Machi Mosi.”

Wachambuzi wanasema, kama hizo nyaraka ni za kweli, ina maana kuwa Marekani inahusika katika vita kati ya Russia na Ukraine, na inatoa taarifa za kiintelijensia kuunga mkono upande wa Ukraine kuliko ilivyofahamika awali. Sio hilo tu, kuna nyaraka zaidi ya 100 ambazo zimevuja, na licha ya suala la Ukraine, kuna taarifa nyingi za siri za kiusalama za Marekani kuhusu China, Mashariki ya Kati, Peninsula ya Korea, na eneo la Indo-Pasific.

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, katika kukumbusha kuwa Marekani inawachunguza hata na wale inaowaita washirika wake, waraka mwingine unaeleza kuwa Baraza la Usalama la Taifa la Korea Kusini mapema mwezi Machi lilishughulikia ombi la Marekani kuwa nchi hiyo itoe silaha kwa Ukraine, bila ya kugombana na Russia.

Mpaka sasa bado haijafahamika kama nyaraka hizo zilivujishwa kwa makusudi na intelijensia ya Marekani. Nyaraka hizo zilizovuja zinafumbua macho ya wengi kwa kuwa zinahusisha maeneo mengi, sio tu hali ya Ukraine, lakini pia masuala ya China, MAshariki ya Kati, Peninsula ya Korea na maeneo mengine.

Waraka wa mwisho kuvujishwa wa intelijensia ya Marekani ulikuwa ni ule wa PRISM uliowekwa wazi na Edward Snowden. Wakati huo, taarifa za Marekani kupeleleza nchi nyingine duniani, ikiwemo washirika wake, ziliwashangaza na kuwashtua washirikia hao, na Marekani yenyewe kukumbwa na aibu kubwa.

Safari hii, haijulikani imekuwaje mpaka taarifa hizo za kiintelijensia zimevuja, kuna penfo kubwa kiasi gani kwenye mfumo wa intelijensia wa Marekani, na kama tukio hilo limetokana na hitilafu za kiufundi katika taasisi za intelijensia za Marekani, ama ni taarifa zilizovujishwa kwa makusudi.

Lakini, kuvuja kwa nyaraka hizo kumewafanya washirika wa Maekani kuingiwa na wasiwasi kuwa Marekani haina njia ya kuwalinda, na haiwezi kuhakikisha usalama wake yenyewe.

Inawezekana kuwa huenda nyaraka hizo zimevujishwa kwa makusudi ndani ya Marekani, hususan kwa Wamarekani wanaoiunga mkono Rusia, ili kuilazimisha Marekani kuacha kuingilia mgogoro wa Ukraine haraka iwekekanavyo.

Ni wazi kuwa mtu ama watu ama taasisi iliyovujisha nyaraka hizo wanataka kuionya serikali ya Marekani kutojihusisha zaidi na mgogoro huo, jambo linaloweza kusababisha makabiliano ya moja kwa moja kati ya Marekani na Russia.

Pia, inawezekana kuwa, watu wenye taarifa sahihi nchini Marekani walipata nyaraka hizo na kuziweka wazi katika mitandao ya kijamii, jambo ambalo ni la kawaida nchini humo.

Jambo moja la wazi lililodhihirishwa na kuvuja kwa nyaraka hizo ni kwamba, Marekani ni nchi kubwa zaidi duniani ya inayopeleleza na kufuatilia nchi nyingine kwa karibu zaidi duniani. Marekani inapeleleza dunia nzima, sio tu wapinzani wake, bali hata washirika wake.

Baada ya tukio hili, washirika wa Marekani wanapaswa kufikiria kwa kina kuhusu kama Marekani ni mshirika halisi na anaweza kuaminiwa? Marekani inazungumza kuhusu itikadi, demokrasia, uhuru na thamani, lakini kipeumbele pekee cha masuala haya kinaelekezwa kwenye maslahi yake yenyewe.

Marekani hainaminiki, na ni muda mchache tu umebaki kabla ya nchi hiyo kuachana na washirika wake, tena katika wakati muhimu zaidi. Huenda kuvuja kwa nyaraka hizo ni jambo jema, kama vile Snowden alivyovujisha nyaraka nyingi za siri za Marekani, na kuilazimisha nchi hiyo kurekebisha sera zake.

Lakini bila kujali ni kiasi gani nchi hiyo itarekebisha sera zake, kamwe haitaacha kufuatilia nchi nyingize duniani. Alimradi Marekani inataka kushikilia ukuu wake wa dunia, inahitaji kufahamu kila kitu kinachoendelea duniani, na usimamizi ni njia muhimu ya kutimiza lengo hili.
 
Kwa hiyo zaidi imevuja uhusika wa marekani kuihami Ukraine? Kwani uhusika wa Russia huko nao unasema je?

Kwa hiyo ukilinganisha uhusika wa Russia, marekani na mataifa mengine Ukraine wewe unaona Russia ni mshirika mwenye kuaminika zaidi asiyeangalia maslahi yake mwenyewe ila ya wengine?
 
Marekani amegundulika kuwa huwa abaidukua simu ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres! Na Marekani anamuona António Guterres kama anaipwndelea Russia kuliko Ukraine.
Screenshot_2023-04-20-09-59-50-20_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg

Screenshot_2023-04-20-09-58-15-43_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_2023-04-20-09-59-50-20_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    Screenshot_2023-04-20-09-59-50-20_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    142.9 KB · Views: 3
View attachment 2593629

Vyombo vya habari vya nchini Marekani vimeripoti kuwa, nyaraka kadhaa za jeshi la Marekani zimevujishwa kwenye mitandao ya kijamii, zikiwa na taarifa kamili kama vile ramani ya Ukraine na sehemu ambazo askari wake wako na aina ya silaha walizonazo.

Moja ya nyaraka hizo imeandikwa “Siri Kuu” na ina kichwa cha habari kinachosema “Hali ya Vita mpaka Machi Mosi.”

Wachambuzi wanasema, kama hizo nyaraka ni za kweli, ina maana kuwa Marekani inahusika katika vita kati ya Russia na Ukraine, na inatoa taarifa za kiintelijensia kuunga mkono upande wa Ukraine kuliko ilivyofahamika awali. Sio hilo tu, kuna nyaraka zaidi ya 100 ambazo zimevuja, na licha ya suala la Ukraine, kuna taarifa nyingi za siri za kiusalama za Marekani kuhusu China, Mashariki ya Kati, Peninsula ya Korea, na eneo la Indo-Pasific.

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, katika kukumbusha kuwa Marekani inawachunguza hata na wale inaowaita washirika wake, waraka mwingine unaeleza kuwa Baraza la Usalama la Taifa la Korea Kusini mapema mwezi Machi lilishughulikia ombi la Marekani kuwa nchi hiyo itoe silaha kwa Ukraine, bila ya kugombana na Russia.

Mpaka sasa bado haijafahamika kama nyaraka hizo zilivujishwa kwa makusudi na intelijensia ya Marekani. Nyaraka hizo zilizovuja zinafumbua macho ya wengi kwa kuwa zinahusisha maeneo mengi, sio tu hali ya Ukraine, lakini pia masuala ya China, MAshariki ya Kati, Peninsula ya Korea na maeneo mengine.

Waraka wa mwisho kuvujishwa wa intelijensia ya Marekani ulikuwa ni ule wa PRISM uliowekwa wazi na Edward Snowden. Wakati huo, taarifa za Marekani kupeleleza nchi nyingine duniani, ikiwemo washirika wake, ziliwashangaza na kuwashtua washirikia hao, na Marekani yenyewe kukumbwa na aibu kubwa.

Safari hii, haijulikani imekuwaje mpaka taarifa hizo za kiintelijensia zimevuja, kuna penfo kubwa kiasi gani kwenye mfumo wa intelijensia wa Marekani, na kama tukio hilo limetokana na hitilafu za kiufundi katika taasisi za intelijensia za Marekani, ama ni taarifa zilizovujishwa kwa makusudi.

Lakini, kuvuja kwa nyaraka hizo kumewafanya washirika wa Maekani kuingiwa na wasiwasi kuwa Marekani haina njia ya kuwalinda, na haiwezi kuhakikisha usalama wake yenyewe.

Inawezekana kuwa huenda nyaraka hizo zimevujishwa kwa makusudi ndani ya Marekani, hususan kwa Wamarekani wanaoiunga mkono Rusia, ili kuilazimisha Marekani kuacha kuingilia mgogoro wa Ukraine haraka iwekekanavyo.

Ni wazi kuwa mtu ama watu ama taasisi iliyovujisha nyaraka hizo wanataka kuionya serikali ya Marekani kutojihusisha zaidi na mgogoro huo, jambo linaloweza kusababisha makabiliano ya moja kwa moja kati ya Marekani na Russia.

Pia, inawezekana kuwa, watu wenye taarifa sahihi nchini Marekani walipata nyaraka hizo na kuziweka wazi katika mitandao ya kijamii, jambo ambalo ni la kawaida nchini humo.

Jambo moja la wazi lililodhihirishwa na kuvuja kwa nyaraka hizo ni kwamba, Marekani ni nchi kubwa zaidi duniani ya inayopeleleza na kufuatilia nchi nyingine kwa karibu zaidi duniani. Marekani inapeleleza dunia nzima, sio tu wapinzani wake, bali hata washirika wake.

Baada ya tukio hili, washirika wa Marekani wanapaswa kufikiria kwa kina kuhusu kama Marekani ni mshirika halisi na anaweza kuaminiwa? Marekani inazungumza kuhusu itikadi, demokrasia, uhuru na thamani, lakini kipeumbele pekee cha masuala haya kinaelekezwa kwenye maslahi yake yenyewe.

Marekani hainaminiki, na ni muda mchache tu umebaki kabla ya nchi hiyo kuachana na washirika wake, tena katika wakati muhimu zaidi. Huenda kuvuja kwa nyaraka hizo ni jambo jema, kama vile Snowden alivyovujisha nyaraka nyingi za siri za Marekani, na kuilazimisha nchi hiyo kurekebisha sera zake.

Lakini bila kujali ni kiasi gani nchi hiyo itarekebisha sera zake, kamwe haitaacha kufuatilia nchi nyingize duniani. Alimradi Marekani inataka kushikilia ukuu wake wa dunia, inahitaji kufahamu kila kitu kinachoendelea duniani, na usimamizi ni njia muhimu ya kutimiza lengo hili.
umeandika vingi ila najibu kuwa Urusi hana haki ya kuingiza majeshi yake Ukraine hata kama Biden angehamia Ukraine , kama kwel Urusi analinda usalama awavamie latvia , estonia na Finland
 
Kwanini wanafanya kwa siri, si wakiwashe waziwazi tuone.Kuliko kuona nchi inakuwa kama uwaanja wa soka.
 
umeandika vingi ila najibu kuwa Urusi hana haki ya kuingiza majeshi yake Ukraine hata kama Biden angehamia Ukraine , kama kwel Urusi analinda usalama awavamie latvia , estonia na Finland
Ila Marekani anahaki kuivamia nchi nyingine?
 
Back
Top Bottom