Taarifa ya serikali juu ya mgomo wa madaktari

Anasema madaktari wanapata mshahara mkubwa kuliko watumishi wengine wote wa serikali
 
kuhusu kima cha chini cha madaktari, kwamba wanapata mshahara mzuri kuliko watumishi wengine wa umma. Kwa sasa ni 951,700 kwa mwezi ila mdoc wanataka iwe 3,500,000
 
serikali inasema bungeni madaktari wanalipwa laki 9 wanataka walipwe mshahara wa milioni 3.5
 
Serikali inafanyia kazi suala la posho za mazingira hatarishi kwa madaktari...
Muda gani tangu ianze kufanyia kazi?
 
serikali ilipata mkopo wa kujenga nyumba 700 za madaktari kutoka global bank na ujenzi umeanza.
 
anasema majibu ya madaktari kuwa hawataweza kukutana j2 wakutane j3 YALIPELEKWA KWENYE OFISI NDOGO YA WAZIRI MKUU SAA 3 USIKU.
 
jamani huyu waziri ni kiazi kweli, sijui mkuu wa kaya alimuokota wapi huyu mpogoro/mndamba
 
madaktari wakianza kazi wanalipwa laki 9 na nusu tofauti na madai kwamba wanalipwa laki 7. Mhandisi akianza kazi analipwa laki 6 na mhasibu laki 4
 
hiyo hutuba inatofauti gani na ya PINDA si ndo ileile jamani, hv mlidhani atatoa mpya kweli?
 
Jamani mwenzenu niko mbali na TV nimejaribu kutoka kidogo kusaka TV lakini sehemu niliyoenda watu wanaagalia Taarabu na bongo felva tu,nimehamia sehemu ya pili nikakuta wamezima kabisa,nimekwenda Saloon nikakuta wanaangalia breaking news ITV kuhusu Misri wananchi wameandamana kuilaani serikali kwa kutokuzuia mauaji yaliyotokea uwanjani,nikashawishi kuweka TBC hola,ikawa haipatikani,nikajaribu Star Tv nikaona mahojiano ya Dr Ulimboka,hivyo wakuu tunaomba japo mtupe Update wale mnaoangalia na ikibidi mtuwekee Taarifa nzima ya Serikali kuhusu mgomo
 
Waziri amesema Ulimboka sio daktari na anashangaa alipataje kuongoza kamati ya kudai haki za madaktari. Alifukuzwa mwaka 2005 na kuomba msamaha kwa Rais hakufafanua kama alipewa au la. Waziri anamwita bw. Ulimboka kwa sababu si Dk.
 
Back
Top Bottom