apolycaripto
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 644
- 225
Hii kweli siasa!Lema amekuwa mbumbu akidhani taarifa atakayowasilisha bungeni kulingana na maagizo ya Spika itamnusuru kwa Waziri Mkuu kuonekana kweli kadanganya Bunge na wananchi.Lema hatokuwa na cha ziada mbali na taarifa ileile iliyofahamika kama Tamko la Chadema juu ya Mauaji Arusha ambayo imekwisha tolewa na Viongozi wa Chadema na kutaka Nahodha na Mwema kujiuzuru.Mambo yatakuwa kama ifuatavyo:
1)Lema atawasilisha utetezi wake ambao nadhani hautakuwa na jipya mbali ya yale tuliyoyasikia katika media na wengine kujionea.Hapa msingi mkuu wa Lema itakuwa kusisitiza kuwa ilikuwa haki ya kikatiba chadema kuandama na kwa kuwa ilikuwa imekubalika na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha.Hapa kosa la Polisi ni kuuwa Raia japo mpaka sasa haijajibiwa kama wenzetu waliuwawa kabla ya kutolewa amri na Viongozi wa Chadema kwa wafuasi kwenda kuwakomboa Lema na wenzie ama baada ya kauli hiyo ya ukombozi.
2)Upande wa Serikali ni dhahiri sababu zao zimekwisha tolewa kuwa maandamano yalikuwa haramu isipokuwa mkutano ulikuwa halali kutokana na kauli ya IGP Mwema kabla ya kikao cha tarehe 5/1/2011.Polisi walilazimika kutumia nguvu pindi Chadema walipolazimisha maandamano na matukio ya vifo vya wenzetu yalitokana na uchochezi wa Viongozi wa Chadema hasa baada ya kuamuru Lema na wenzie wawe wamekombolewa kutoka katika kituo cha Polisi na kufikishwa katika viwanja vya Unga Ltd ndani ya saa moja.Polisi walitumia risasi kama final resolution baada ya kuona wanazidiwa nguvu na vijana wa Chadema waliokuwa na munkari wa hali ya juu wakitaka kuvamia kituo chenye silaha lukuki.Ni dhahiri hapa ndipo serikali inasema bahati mbaya wenzetu watatu waliuwawa.
Bungeni huu ni mtego tu ili haki ionekane kutendeka na Lema ameadhibiwa kwa kufungiwa kuhudhuria vikao visivyopungua vitano bungeni na kulazimika kufuta kauli yake.Na imani kwa bunge ninaloliona mchango wa kile atakacho kiwasilisha Lema uta kuwa ule wa Mudhihir na Zitto kabwe.Lema ata kama anadhani utetezi wake utakuwa extraordinary asitarajie maamuzi yatam-favour.
Hii kweli siasa!
Nionavyo mimi hatima ya suala hili ni pale tutakapo pata jibu la kuku na yai kipi kilitangulia?.