Je taarifa hii ni ya kweli
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwapo na Taarifa kwa umma inayodaiwa kutolewa na wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania kuhusu Maandamano ya Julai 7, 2026 na kuonesha imetolewa Julai 6, 2026.
Taarifa hiyo inaendelea kueleza kuwa inawahimiza wanafunzi wa chuo kushiriki maandamano hayo ka upande wao yakiwa na Ajenda mbili, ya kwanza ni utolewaji wa mikopo a elimu ya juu na ya pili ni kulaani mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa IFM, James Temba.
Taarifa hiyo ina baadhi ya dosari ikiwemo kutokuonesha imetolewa na nani ama kiongozi wake, lakini pia haina sahihi ya aliyetoa Taarifa hiyo na badala yake imekuwa ni ya jumla. Sambamba na hilo imetumia nembo ya Taifa pekee ambayo si kawaida kutumika nje na shughuli za serikali.
Aidha Jumuiya ambayo inafahamika ya wanayuo ni jumuiya ya wanafunzi Taasisi za elimu ya juu (TAHLISO) ambayo haijachapisha ama kutoa tamko lolote linalofanana na hilo kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya mawasiliano.