Taarifa ya Kikao Cha Baraza Kuu- CHADEMA by Mnyika

Bahati nzuri nawafanyia kazi Wahindi, najua vile Mzee mwinyi anakula gawio kwa kushinikiza kutolewa kibali kwa properties kujengwa kwenye Mapito ya wanyama kinyumu cha sheria. He gets 20% since year 1992. Huyu mwajiri ameajiri Wa Tanzania Kama 700, kiburi alicho nacho Ni kutoa ajira tu and nothing more! Mtanzania analipwa 600000 thou maximum mkenya $2000 US minimu
! Mzungu $5000 minimum forget about all other benefit fringes wanapata!
Matumbo Yao Ni moto sana vile Ezekiel Maige ataondoshwa kwenye system, they are crossing their fingers ili Mtu atakaewekwa kwenye mfumo awe mdhalimu kwa kuwa favour wao!

Sitegemei chochote cha maana kutoka Ccm ya Leo! Nipo nimejichokea lakini Nina tumaini.

NB: kampuni inaitwa Sopa management Ltd!

Faida kwa siku Ni kati ya dollar 1000000 (lakimoja) Hadi 700000! What a shame! Wanatudharau na hakuna wakusimama kutetea Hilo!

Question to you!
 
Bora kilaza mmoja anayechukia ufisadi kuliko magamba milioni wanaotetea ufisadi kama wewe. Pole sana kwa kuwa nahisi usomi wako hauna tija kwa maskini wengi wa nchi hii tajiri :love:
 
BARAZA Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limesema kuwa mabadiliko ya baraza la mawaziri yanayotarajiwa kufanyika wakati wowote si suluhu ya kupunguza au kumaliza ubadhirifu serikalini kwa madai kuwa ufisadi ni sehemu ya mfumo wa utawala wa CCM.

Aidha kuvunjwa kwa baraza la mawaziri kwa kuepuka ushauri wa wabunge na kutumia kauli ya Kamati Kuu ya CCM, ni matokeo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kuhofia nguvu ya umma.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alibainisha hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari akielezea maazimio ya baraza hilo lililomaliza kikao chake juzi.

Mnyika alieleza kuwa mabadiliko hayo hayataleta mageuzi ya maana kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete bado atateua sehemu kubwa ya mawaziri waliopatikana kifisadi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

“Kauli ya CCM kuwa watawapeleka mahakamani mawaziri na watendaji wote waliohusika katika ubadhirifu ni siasa tupu, kwani ushahidi uko wazi kuwa mpaka sasa serikali hiihii chini ya chama hichohicho haijawapeleka mahakamani mawaziri waliopatikana na kashfa na kulazimika kujiuzulu mwaka 2008 na wameshindwa kuwafukuza kwenye chama.

“Zaidi ya hayo, kuna orodha ndefu ya mafisadi iliyotolewa hadharani mwaka 2007 na mafisadi wakuu hawajagushwa,” alisema.

Alieleza kuwa CCM iliitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu na kutoa tamko juu ya baraza la mawaziri baada ya kusikia kuwa Baraza Kuu la chama hicho linakutana na kuanza maandalizi ya kuunganisha nguvu ya umma kushinikiza mabadiliko ya kiutawala na mfumo.

“…ni wazi kuwa CCM na Rais Jakaya Kikwete wamekubali kufikia hatua hiyo wakihofia nguvu ya umma.

“Baraza Kuu limeazimia kuwataka Watanzania kutambua kuwa kwa muda mrefu sasa baraza la mawaziri limekuwa kielelezo kamili cha mfumo wa ubadhirifu, rushwa na ufisadi katika utawala wa nchi hii chini ya CCM,” alisema Mnyika.

Alisema chama hicho si cha msimu wala matukio na kwamba wanahitaji uwajibikaji mkubwa nchini na kuongeza kuwa operesheni za chama hicho nchi nzima hazitakwisha.

“Operesheni zetu ziko palepale, tunahitaji mabadiliko ya mfumo, kwani kuna uozo mkubwa kwenye safu za uongozi,” alisema Mnyika wataunganisha nguvu ya umma na kujenga chama katika operesheni hizo.

Hali ya uchumi

Mnyika alisema kuwa baraza hilo limebaini kuwa hali hiyo inasababishwa na uongozi dhaifu wa serikali ya CCM ambayo imeshindwa kudhibiti matumizi mabaya katika serikali na idara zake na kushindwa kuchochea uzalishaji wa chakula na nishati nchini.

Alisema kuwa baraza hilo limeuagiza uongozi wa taifa wa CHADEMA pamoja na wabunge kuwahimiza wananchi kuendelea kuishinikiza serikali kutimiza wajibu wake.

Pamoja na hilo, alisema baraza hilo limewataka wananchi kujiandaa kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi na utawala katika chaguzi zijazo, kwani kikwazo kikubwa cha maendeleo nchini ni CCM inayoendesha serikali kwa mfumo wa rushwa na ufisadi.

Mnyika aliongeza kuwa mabadiliko ya kweli nchini yatapatikana kwa kuiondoa CCM madarakani.

Mauaji ya wanachama

Baraza hilo limelaani mauaji ya wanachama wake huku jeshi la polisi likishindwa kuchukua hatua zozote za maana.

“Baraza Kuu limelaani mauaji ya Mwenyekiti wa Kata ya Usa River yaliyotokea Aprili 28 mwaka huu na pia limeeleza kusikitishwa na jeshi la polisi kwa kushindwa kuchukua hatua za maana dhidi ya watu waliohusika na mauaji ya wanachama wa CHADEMA ambayo yamekuwa yakitokea tangu uchaguzi mdogo wa Igunga,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, alisema baraza hilo limeuagiza uongozi wa chama hicho kuanzisha mchakato wa kulishtaki jeshi la polisi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Aidha pamoja na hayo, alisema baraza hilo limeagiza chama kusukuma hoja ya kuwapo kwa uchunguzi huru dhidi ya matendo ya kidhalimu yanayofanywa na Jeshi la Polisi na kutolea mfano Arusha, Mwanza, Ruvuma Mbeya na Mtwara (Tandahimba).

Uchaguzi ndani ya chama

Mnyika alisema kikao hicho kimepanga uchaguzi ndani ya chama hicho kufanyika kuanzia Juni mwaka huu kwa ngazi ya msingi na kukamilika Oktoba mwakani kwa ngazi ya taifa.

alisema katika kudhibiti rushwa katika uchaguzi huo, baraza kuu limeiagiza Kamati Kuu kuandaa mwongozo wa kudhibiti hali hiyo, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa uadilifu na maadili.

Masuala ya kijamii

Aidha alisema baraza hilo limeitaka serikali ya CCM kutekeleza tamko la chama hicho kutatua migogoro ya makundi ya kijamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wakulima hasa katika masuala ya ardhi na maslahi ya wafanyakazi.

Alisema kuwa mpaka sasa serikali bado haijapandisha mishahara ya wafanyakazi na kusema kuwa hali hiyo ndiyo inayochangia kuwapo kwa migogoro ya mara kwa mara.

“Tunaamini rasilimali na mapato ya nchi yakitumika vizuri yanaweza kutekeleza mambo haya na wafanyakazi wakawa na maslahi bora,” alisema.


:smile-big:tunashuru kwa taarifa
 
Back
Top Bottom