Taarifa ya Kikao Cha Baraza Kuu- CHADEMA by Mnyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya Kikao Cha Baraza Kuu- CHADEMA by Mnyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, May 1, 2012.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  BARAZA Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limesema kuwa mabadiliko ya baraza la mawaziri yanayotarajiwa kufanyika wakati wowote si suluhu ya kupunguza au kumaliza ubadhirifu serikalini kwa madai kuwa ufisadi ni sehemu ya mfumo wa utawala wa CCM.

  Aidha kuvunjwa kwa baraza la mawaziri kwa kuepuka ushauri wa wabunge na kutumia kauli ya Kamati Kuu ya CCM, ni matokeo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kuhofia nguvu ya umma.

  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alibainisha hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari akielezea maazimio ya baraza hilo lililomaliza kikao chake juzi.

  Mnyika alieleza kuwa mabadiliko hayo hayataleta mageuzi ya maana kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete bado atateua sehemu kubwa ya mawaziri waliopatikana kifisadi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  “Kauli ya CCM kuwa watawapeleka mahakamani mawaziri na watendaji wote waliohusika katika ubadhirifu ni siasa tupu, kwani ushahidi uko wazi kuwa mpaka sasa serikali hiihii chini ya chama hichohicho haijawapeleka mahakamani mawaziri waliopatikana na kashfa na kulazimika kujiuzulu mwaka 2008 na wameshindwa kuwafukuza kwenye chama.

  “Zaidi ya hayo, kuna orodha ndefu ya mafisadi iliyotolewa hadharani mwaka 2007 na mafisadi wakuu hawajagushwa,” alisema.

  Alieleza kuwa CCM iliitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu na kutoa tamko juu ya baraza la mawaziri baada ya kusikia kuwa Baraza Kuu la chama hicho linakutana na kuanza maandalizi ya kuunganisha nguvu ya umma kushinikiza mabadiliko ya kiutawala na mfumo.

  “…ni wazi kuwa CCM na Rais Jakaya Kikwete wamekubali kufikia hatua hiyo wakihofia nguvu ya umma.

  “Baraza Kuu limeazimia kuwataka Watanzania kutambua kuwa kwa muda mrefu sasa baraza la mawaziri limekuwa kielelezo kamili cha mfumo wa ubadhirifu, rushwa na ufisadi katika utawala wa nchi hii chini ya CCM,” alisema Mnyika.

  Alisema chama hicho si cha msimu wala matukio na kwamba wanahitaji uwajibikaji mkubwa nchini na kuongeza kuwa operesheni za chama hicho nchi nzima hazitakwisha.

  “Operesheni zetu ziko palepale, tunahitaji mabadiliko ya mfumo, kwani kuna uozo mkubwa kwenye safu za uongozi,” alisema Mnyika wataunganisha nguvu ya umma na kujenga chama katika operesheni hizo.

  Hali ya uchumi

  Mnyika alisema kuwa baraza hilo limebaini kuwa hali hiyo inasababishwa na uongozi dhaifu wa serikali ya CCM ambayo imeshindwa kudhibiti matumizi mabaya katika serikali na idara zake na kushindwa kuchochea uzalishaji wa chakula na nishati nchini.

  Alisema kuwa baraza hilo limeuagiza uongozi wa taifa wa CHADEMA pamoja na wabunge kuwahimiza wananchi kuendelea kuishinikiza serikali kutimiza wajibu wake.

  Pamoja na hilo, alisema baraza hilo limewataka wananchi kujiandaa kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi na utawala katika chaguzi zijazo, kwani kikwazo kikubwa cha maendeleo nchini ni CCM inayoendesha serikali kwa mfumo wa rushwa na ufisadi.

  Mnyika aliongeza kuwa mabadiliko ya kweli nchini yatapatikana kwa kuiondoa CCM madarakani.

  Mauaji ya wanachama

  Baraza hilo limelaani mauaji ya wanachama wake huku jeshi la polisi likishindwa kuchukua hatua zozote za maana.

  “Baraza Kuu limelaani mauaji ya Mwenyekiti wa Kata ya Usa River yaliyotokea Aprili 28 mwaka huu na pia limeeleza kusikitishwa na jeshi la polisi kwa kushindwa kuchukua hatua za maana dhidi ya watu waliohusika na mauaji ya wanachama wa CHADEMA ambayo yamekuwa yakitokea tangu uchaguzi mdogo wa Igunga,” alisema.

  Kutokana na hali hiyo, alisema baraza hilo limeuagiza uongozi wa chama hicho kuanzisha mchakato wa kulishtaki jeshi la polisi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake.

  Aidha pamoja na hayo, alisema baraza hilo limeagiza chama kusukuma hoja ya kuwapo kwa uchunguzi huru dhidi ya matendo ya kidhalimu yanayofanywa na Jeshi la Polisi na kutolea mfano Arusha, Mwanza, Ruvuma Mbeya na Mtwara (Tandahimba).

  Uchaguzi ndani ya chama

  Mnyika alisema kikao hicho kimepanga uchaguzi ndani ya chama hicho kufanyika kuanzia Juni mwaka huu kwa ngazi ya msingi na kukamilika Oktoba mwakani kwa ngazi ya taifa.

  alisema katika kudhibiti rushwa katika uchaguzi huo, baraza kuu limeiagiza Kamati Kuu kuandaa mwongozo wa kudhibiti hali hiyo, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa uadilifu na maadili.

  Masuala ya kijamii

  Aidha alisema baraza hilo limeitaka serikali ya CCM kutekeleza tamko la chama hicho kutatua migogoro ya makundi ya kijamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wakulima hasa katika masuala ya ardhi na maslahi ya wafanyakazi.

  Alisema kuwa mpaka sasa serikali bado haijapandisha mishahara ya wafanyakazi na kusema kuwa hali hiyo ndiyo inayochangia kuwapo kwa migogoro ya mara kwa mara.

  “Tunaamini rasilimali na mapato ya nchi yakitumika vizuri yanaweza kutekeleza mambo haya na wafanyakazi wakawa na maslahi bora,” alisema.
   
 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Operation za chama zifuatazo :

  Operesheni sangara - Zitaendelea

  Operesheni twanga kotekote - zitaendelea

  MOVEMENT FOR CHANGE (M4C) - itaendendelea

  hiki si chama cha msimu THANX

   
 3. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,782
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280

  Exactly hapo kwenye
  red - ndicho kiini cha matatizo ya taifa letu - UFISADI NI SEHEMU YA MFUMO WA CCM huo ndio ukweli japo mchungu kuukubali. Mwaka huu CCM inafanya chaguzi ngazi ya matawi lakini mchakato wenyewe umegubikwa na UFISADI wa kutisha. Kila "kiongozi" ana wajumbe na watu wake kwa ajili kujihakikishia kura katika chaguzi za juu.

  UFISADI ni uhai wa CCM hivyo kuuondoa maana yake ni kuiua CCM. Tusitegemee hata mara moja kwamba ufisadi ndani ya CCM au katika serikali yake kumalizwa na CCM, ni lazima nguvu kutoka nje ya CCM iingilie kati.
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,782
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Tatizo lingine hilo hapo kwenye red - CHAGUZI ZA KIFISADI chini ya MAMLAKA ZA KIFISADI zilizowekwa na SERIKALI YA CHAMA CHA KIFISADI huzaa Bunge hatimaye serikali na hatimaye TAIFA LA KIFISADI kama tunavyoshudia hivi leo.

  Hii "vicious circle" si lelemama. Zinahitajika nguvu za ziada kweli kweli kupamba nayo wakati mwingine hata baadhi ya wapiganaji kupoteza maisha yao.
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,782
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Ninaanza kuwa na mashaka na hicho kinachoitwa KATIBA MPYA inayoratibiwa na serikali iliyojaa mawaziri na watendaji MAFISADI. Sitegemei CCM kutuletea Katiba ya maana ya nchi.
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ufisadi ndiyo unao iua CCM

  Ufisadi ndiyo unao iua nchi yetu ya Tanzania

  Ufisadi umeota kuanzia juu hadi ngazi ya chini nao wanajua kuwa ufisadi ni sehemu ya maisha yao na utawala
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Well said Mnyika. UFISADI ndio ROHO ya CCM. No ufisadi no CCM.
   
 8. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mi nlikuwa ktk ban cna mchango wa taifa humu wiki 2.So mbona nimeckia mwema ka2ma makachero meru? Wa kudhibiti uvamizi wa mashamba ama kuchunguza mauaji?
   
 9. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Kama wanaona CCM ni mafisadi, wana mpango gani hao vilaza wa Chadema?
  .
  "WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
   
 10. M

  Mkira JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  chadema mmechelwa sana kuishitaki serikali tena wanachama wenu wataanza kuogopa KABISA WATU WANAUKUFA MMEKAA KIMYA, KWA VILE POLISI WETU WAMESHINDWA KUWAKATAMA HATA WALIOWAKATA MAPANGA WABUNGE WENU,

  MSICHELEWE TENA PELEKENI KESI HII THE HAUGUE UHAOLANZI MAHAKAMA YA ICC MSHITAKINI IGP MWEMA KWA KUANZIA

  IGP MWEMA NA KESI YA KUJIBU,


  (MAUAJI ARUSHA SONGEA, WABUNGE KUKATWA MAPANGA MAUAJI ARUMERU, ARUSHA NK, FANYENI HRAKA VINGINEVYO VIONGOZI FANYENI TAKAFAKRI KAMA MNAFAA KUWEPO AU LA!!
   
 11. s

  shumbi Senior Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 180
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  We si unapenda kuliwa na CCM.
  Hatukunyimi kuliwa, endelea kuwapa tu.
  Unatetea ushenzi!!!
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nimeangalia juu nukakuta haijapostiwa na Mnyika kama ilivyo kawaida. Nimeangalia chini nikakuta haina ule signature ya JJ Mnyika Mkurugenzi wa Habari na Uenezi. Sijaisoma yote naogopa isije ikawa siyo official press release ya CDM.
   
 13. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu unadandia Treni kwa Mbele ndiyo maana wameku BAN, Huu mchango wako mbona hauhusiani na huu UZI
   
 14. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu usiwe na Hofu source Tanzania Daima ya Leo.
   
 15. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naona unaingia kinyume nyume kwenye BAN, usijelalamika
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  serikali ipandishe mishahara ya wafanyakazi wake na wasiseme kua hawana hela maana report ya CAG inaonyesha kabisa kua hela zipo sema zinaishia kwa wakubwa...hizo hela zilizopotea zingetosha kuongeza mishahara kwa walimu, madaktari etc...
   
 17. M

  Maskini Jeuri Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ooh yes! You are right Dudus! Quite right. Kakuna vile kiongozi Atakalia kiti isivyo haki na atende haki. Ni kama kusubiri maziwa aliyokamuliwa chui! Obviously hakuna Kitu hapo! Fumua mfumo= ondoa Ccm.
   
 18. S

  STIDE JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu mtotowamjini, wewe unataka wapandishe mishahara alafu waibe wapi!!? Matumbo yao yajazwe na nini!!?

  Mimi huwa nasema hakuna kupandisha mishahara, maisha yazidi kuwa magumu, watuue zaidi yaani kwa ufupi watukamue hadi maji ya kunywa yakose, ili kila mtanzania kufikia 2015 awe anajua anachokifanya!

  Ukiiangalia mi-polisi, mikanda ruksi zinarukana lakini eti utayakuta barabarani yamekomaa na virungu kuzuia maandamano ya wadai haki!!!!

  Sijui Tanzania tumerogwa na nani!!!
   
 19. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  nimependa sana nukuu yako, naomba iwe hivi, no ccm no ufisadi, kwa maana kuwa tuiondoe ccm then ufisad
  utajiondoa tu.
   
 20. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  una elimu ya std gani? ivi ni chama gani kina wanachama na viongozi(wabunge) wasomi?
  ivi profesa yakuoga marefu anaelimu gani? labda kama unamaanisha ccm ni chakula cha cdm
  apo sawa, na mtaliwa sana tu pamoja na magamba yenu
   
Loading...