Taarifa ya Bakhresa Group kuhusiana na Upotevu wa Makontena

Tatizo hapa kuna watu wanataka kulazimisha kwamba azam anakwepa kodi.maelezo yametolewa na kampuni na kwamba uchunguzi unafanywa kwa ushirikiano wa kampuni yenyewe na serikali na wahusika watawajibishwa na kodi italipwa sasa nashangaa mnaoanza malalamiko kwa kampuni ya azam.
 
umeeleweka vizuri...sema jukwaa hili sikuhizi lina std 7 pupils hawawezi kukuelewa...
 
Nguo za mtu zinapotelea kwako lazima utakua unamjua mwenye nazo,,, hivyo akitaja makontena in ya wafanyabiashara fulani na sisi ndo tuliyahifadhi kungojea yalipiwe kodi. Hivyo makontena yaliyopotea ni kua AZAM anajua wamiliki na dili ni moja....
 
Nilikuwa na mpango wa kususia bidhaa za kampuni hii, lin kila nikiangaliaaa sioni mbadala!

Sio kweli Mkuu... bidhaa za SSB ambazo ni Quality ni ile Ngano yake na Sembe pamoja na AZAM TV.. Nyingine hakuna kitu, poor and low low quality.. Nadhani ametengeneza kulenga watumiaji wa kawaida tu (low income earners)..
 
Nafikiri aliyeandika hiyo taarifa ameshindwa kufafanua vizuri. Mwisho wa siku ataleta contradiction zaidi sababu ya kukosa ujuzi wa kuandika kiswahili cha kueleweka. Yeye alitakiwa afafanue ishu ya kodi coz wengi wameshachukulia bakhresa kakwepa kodi sio wengi wanaofahamu kuhusu icd. Anapeleka ujumbe nyeti kwa raia wa kawaida bila kusimplify.
Wewe ndio umeshindwa kusimplify. Hiyo ni akili ya kuwafanya wananchi washindwe kuelewa nini kinaongelewa. Kama kuna ukweli basi lugha ngumu itasaidia watu kutoelewa kinachozungumziwa. Ukiacha na contradiction ndio inapendeza. Waulize watu wa PR kama hiyo imeandikwa kwa bahati mbaya.
 
Mkuu hivi unajua maana ya ICD? Ngoja nikusaidie kiduchu.

Manifesting Cargo to-Inland Container Depots.

Hiyo ndiyo maana ya ICD bandari kavu ambayo inamilikuwa na Bakhressa lakini shughuli zote humo zanafanywa na watu wa bandari na TRA.

Labda tufahamishe alipe kodi gani?


Hizo Container kama ni kweli zilitolewa hapo Depot kwake bila kulipiwa kodi, yeye pamoja na TRA Staffs wa hapo Depot kwake watawajibishwa/wana kesi ya kujibu... Na sio kwamba yeye ndiye kakwepa, lah hasha ila yawezekana Depot yake inatumika kukwepesha kodi..
 
Sasa ndio ameongea kitu gani hapo, makontena 54 ni ya kwao kati ya hayo 346, hapa dawa ni kulipa tu hiyo kodi waliyokwepa na wawajibishwe kisheria. Hapa kazi tu!
 
Huko ndijko kujambajamba......subiri uchunguzi

Natoa ufafanuzi kwako na viazi wenzako kuwa, Bakhresa anamiliki bandari kavu. Waliongiza mizigo kwa container wanahifadhi huko kama njia ya kuepusha msongamano katika bandari yetu.

Katika kila bandari kavu kuna maafisa wa TRA na mamlaka nyingine za Serikali ambazo zinasimamia kuhakikisha kodi ya Serikali inalipwa.

Shughuli ya Bakhresa ni kuhifadhi container na analipwa na mmiliki wa container kwa siku linazokaa hapo kwenye eneo lake.

Tukio la wajanja waliobamiza kodi limetokea kwenye eneo la Bakhresa, ndio maana anasema wahusika wakamatwe na wachukuliwe hatua.

Maana yake ni kwamba, maafisa wa serikali waliohusika na mchezo mchafu katika ICD ya Bakhresa ndio watakaoshughulikiwa.

Kuna swali?
 
Back
Top Bottom