Taarifa ya Bakhresa Group kuhusiana na Upotevu wa Makontena

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,030
x4.jpg


Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.

Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena (ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.

Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.

SSB Group of Companies
Corporate Affairs Department
November 29, 2015
 
Ameanza kuweweseka na hapa kazi tu. JK hakutendea haki kauli mbiu ya nguvu mpya, kasi mpya na Ari mpya.
 
Niliuliza hili swali kwanini bakharessa hajakanusha?

By the way unahifadhi vipi mali za wizi?
 
Isipokuwa kuna kontena zimepotea hapo icd kwao!!
Hapo ndo palipo na tatizo

Nafikiri aliyeandika hiyo taarifa ameshindwa kufafanua vizuri. Mwisho wa siku ataleta contradiction zaidi sababu ya kukosa ujuzi wa kuandika kiswahili cha kueleweka. Yeye alitakiwa afafanue ishu ya kodi coz wengi wameshachukulia bakhresa kakwepa kodi sio wengi wanaofahamu kuhusu icd. Anapeleka ujumbe nyeti kwa raia wa kawaida bila kusimplify.
 
Jamani mnatakiwa kuelewa pale yanahifadhiwa makontena ya wateja wenye mizigo yao kwa hyo sio mali za uwiz kwa hyo walio husika ni hao wateja waliohifadhiwa makontena .....kwa hyo na bandar nao wanahifadh mali za uwiz jaribun kuelewa jaman
 
Mbona kama sijaelewa alichokanusha huyo Bakhressa.......
Mtaani habari inayoongelewa sana ni kwamba yale makontena yote 300 ni ya bakhresa na bakhresa anadaiwa kodi bil 80. Ndicho anachokanusha, japo naona kama hajaeleweka namna alivyo kanussha
 
Jamani mnatakiwa kuelewa pale yanahifadhiwa makontena ya wateja wenye mizigo yao kwa hyo sio mali za uwiz kwa hyo walio husika ni hao wateja waliohifadhiwa makontena .....kwa hyo na bandar nao wanahifadh mali za uwiz jaribun kuelewa jaman

Wasituyeyushe hao SSB, kwani kontena /mizigo ikiingia kwao hakuna records? sasa wanalipwaje na TPA Kama hawana records ya mizigo inayoingia?
 
Back
Top Bottom