TAARIFA; Serikali ya Muungano Tanzania inawajibika kutoa kauli madhubuti sakata la Meli za Iran | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAARIFA; Serikali ya Muungano Tanzania inawajibika kutoa kauli madhubuti sakata la Meli za Iran

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Jul 3, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]
  TAARIFA KWA UMMA
  [/FONT]  [FONT=&amp]KAULI JUU YA MELI ZA IRAN KUTUHUMIWA KUTUMIA BENDERA ZA TANZANIA
  [/FONT]


  [FONT=&amp]KWA takribani muda wa juma moja sasa kumekuwepo na taarifa katika vyombo vya habari na njia mbalimbali za upashanaji habari, kuwa kampuni moja ya meli inayodaiwa kutoka Iran, inayojulikana kwa jina la NITC (National Iranian Tanker Company), inatumia bendera ya Tanzania, isivyo kihalali na kinyume kabisa na sheria za nchi na zile za kimataifa, kwa malengo ambayo hayajulikani.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa taarifa kwenye Baraza la Wawakilishi tarehe 2 Julai 2012 kukanusha taarifa hizo, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Uchukuzi kutoa taarifa kwa umma juu ya hatua ilizochukua kuchunguza madai hayo.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ieleze iwapo utaratibu huo umezingatia kwa ukamilifu United Nations Convention law of the Sea, kifungu cha 91, Geneva Convention of Registration kifungu cha 6 na maazimio mengine ya kimataifa kuhusu usajili wa meli kubwa pamoja na usafirishaji wa mafuta.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Maelezo yaliyotolewa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayoongozwa na CCM na CUF yanaibua maswali kutokana na kampuni ya Philtex ya Dubai inayoelezwa kupewa uwakala na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini- Zanzibar Maritime Authority (ZMA) kufanya kazi na makampuni mengine hivyo taarifa hizo hazijitoshelezi katika kuondoa uwezekano kwamba meli za NITC zilipeperusha bendera ya Tanzania.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Ili kujisafisha juu ya tuhuma hizo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilipaswa kushirikiana na Serikali ya Muungano kufanya uchunguzi wa kubaini msingi wa tuhuma hizo na kuchukua hatua iwapo meli za NITC zilipeperusha bendera ya Tanzania bila ridhaa ya serikali zote mbili.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Ikumbukwe kwamba hii si mara ya kwanza kwa baadhi ya maofisa wa ZMA kutuhumiwa kuruhusu vitendo vilivyo kinyume na sheria kama ilivyojitokeza wakati wa kashfa ya kuzama kwa meli ya Spice Islender.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Kwa upande mwingine, Serikali ya Muungano nayo haiwezi kukwepa kuwajibika kwa kuzingatia kuwa kuwa baadhi ya taarifa hizo katika vyombo vya habari vimewanukuu mawaziri wa serikali wakionekana kujikanyanga na kujikanganya juu ya suala hili nyeti la bendera ya taifa, ambayo ni moja ya utambulisho wetu rasmi kama Watanzania, kutumika kwa malengo yasiyojulikana na kampuni ya nje.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Moja ya vyombo vya habari hapa nchini, vimewanukuu mawaziri husika, Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe, juu ya suala hilo. [/FONT]

  [FONT=&amp]
  Wakati Waziri Mwakyembe amenukuliwa akisema kuwa anazo taarifa za suala hilo, lakini asingeweza kulitolea kauli mpaka Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Tanzania Zanzibar azungumze, Waziri Membe yeye mbali ya kukiri kuwa kitendo hicho ni kosa kisheria, anasema habari hizo zilikuwa za kushtushwa na ngeni kabisa, huku akisema kuwa vyombo husika vitalichunguza kwa makini.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Ukimya wa serikali yetu ambayo kwa hakika unatokana na udhaifu wake katika kuchukua maamuzi, sasa umesababisha kitendo hicho kutafsiriwa kuwa Tanzania inaibeba na kuisaidia Iran kukwepa vikwazo ambavyo nchi hiyo inatishiwa na mataifa ya Magharibi, hasa Marekani na Umoja wa Ulaya, kutokana na malumbano ya muda mrefu ambayo yanatokana na mataifa hayo kutumia mabavu na vitisho kuzichagulia baadhi ya nchi nyingine duniani, nini cha kufanya na rasilimali zake mathalani mzozo unaoendelea na Iran kuhusu urutubishaji wa madini ya urani. [/FONT]

  [FONT=&amp]
  Si nia ya CHADEMA kuingia katika mgogoro wa Iran na Mataifa ya Magharibi hapa kupitia mjadala wa madai hayo yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari; lakini CHADEMA kinatoa tamko kufuatia ukimya na kigugumizi kinachoikumba Serikali ya CCM, kila inapohitajika kufanya maamuzi ya haraka, hasa kuwalinda watu wake na hadhi ya utaifa wao na nchi yao ndani na nje ya nchi.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Ni kutokana na udhaifu wa serikali hii, ambayo umekuwa ukijidhihirisha pia kwa kushindwa kupanga bajeti inayojitegemea hasa kwa kutumia utajiri mkubwa wa rasilimali ambazo nchi hii imebarikiwa, hali inayotufanya tuonekane taifa ombaomba na kupoteza heshima mbele ya mataifa makubwa na madogo, kuwa hatuna uwezo wa akili kuweza kujitegemea. [/FONT]

  [FONT=&amp]
  Utegemezi huu umefanya baadhi ya raia wa Nchi nyingine mathalani Mbunge aitwaye Howard Berman wa Bunge la Marekani, akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Nje, kupata uwezo wa kuandika barua ya dharau na kejeli kwa Rais Jakaya Kikwete, juu ya suala hilo la Meli za NIT kutuhumiwa kupeperusha bendera za Tanzania.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Kupitia tamko hili, CHADEMA tunaitaka serikali kutoa kauli madhubuti juu ya suala hilo ambalo tayari limechukua sura ya mjadala wa kimataifa usiokuwa na tija yoyote kwa mustakabali wa Watanzania. Suala la bendera ambayo ni utambulisho wa taifa letu, haliwezi kuwa suala la mchezo tu, ambapo mawaziri wazima hawawezi kutoa kauli za kina na kuchukua hatua zinazostahili, huku serikali nzima ikishindwa kutoa kauli madhubuti na mwafaka.[/FONT]


  [FONT=&amp]Imetolewa tarehe 2 Julai 2012 na:[/FONT]

  [FONT=&amp]Hamad Mussa Yussuf[/FONT]
  [FONT=&amp]Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, Zanzibar[/FONT][FONT=&amp].[/FONT]
   
 2. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  President Jakaya Kikwete, a handsome smiling dictator is a hidden fundamentalist Muslim who has been always embraced by both western and Islamic countries with much economic support! Tanzanians are unfortunate because although they are blessed with a good number of natural resources, their country is still in a pathetic vicious cycle of poverty.

  Corruption has become the daily lifestyle in his country although this man is known as the most professional beggar. His secret meetings with Iranian officials have led Tanzania to fall under the influence of Moslem radicals. As a consequence, Uamsho (a terrorist group) supported by Iran has emerged in the Island of Zanzibar.


  The group is aiming at separating Zanzibar from the Union with Tanganyika/mainland and intends to make Zanzibar an Islamic state. With a humble smile, the president is so quiet, leaving terrorists free to do whatever they want! And activists, who question about the vision of their country, are always frightened with a deceitful political proclamation of "peace and harmony". They remain silent! This is really jugglery. Shame on you Mr President!
   
 3. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Dhaifu.
   
 4. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,285
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Tumefika kwasababu ya udhaifu wa Rais na .............na nna uchungu miee
   
 5. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  huyu jamaa wallah ipo siku atatutoa kafara! hivi anafanya nini ikulu mpaka sasa??? aarrrrggghhhh!!!
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  [O ye who believe! Take not the Jews and the Christians for your friends and protectors: They are but friends and protectors to each other. And he amongst you that turns to them (for friendship) is of them. Verily God guideth not a people unjust.] (Al-Ma'dah 5: 51)
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Usituondowe kwenye mada, hapa mada ni hawa magaidi wa Iran kutumia nchi yetu kama kichaka cha kukwepa vikwazo walivyowekewa na Marekani na EU. Usituletee tabia za Kishoga hapa.
   
 8. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Idumu Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Tanganyika walie tu.
   
 9. l

  lum JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 343
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  awa chedema wamechanganyikiwa nini?
  kuna sheria gani ya kimataifa iloiwekea vikwazo iran au kuizuiya zanzibar isisajili meli za iran. hivyo vikwazo vya mabasha na mashoga wa ulaya na marekani kwa taifa la kiislamu la iran ss TZ inatuhusu nini, kenya wamesema wataendelea kununua mafuta ya irani kwani vikwazo havijapitishwa na UN.
  waziri wa mawasiliano Zanzibar kashasema hilo si jambo la muungano, mawaziri membe na mwakyembe na washuhulike na bei za vivuko kigamboni uko, wakome kuingilia mambo ya znz.
  na hata uyo kikwete hawezi kingilia hilo halimuhusu
   
Loading...