The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Mtoaji
The Hilden Charitable Fund, ni Taasisi isiyo ya Kiserikali ya utoaji wa ruzuku (Grant Making) iliyoko mjini London nchini Uingereza
Maeneo ya mradi
Taasisi itatoa ruzuku kwa miradi iliyojikita katika Maendeleo ya Jamii, Elimu,Afya na masuala ya Wasichana na Wanawake
Kiasi cha ruzuku
Wastani wa Euro 5000 na Taasisi itatoa fedha kwa mradi wa zaidi ya mwaka mmoja
Sifa za Taasisi
Taasisi zote zinazofanya shughuli zake katika nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi hizo. Pia taasisi lazima iwe ina muda wa kufanya shughuli zake zaidi ya kipindi cha miaka 5.
Namna ya uombaji
Taasisi husika inapaswa kuomba ruzuku kwa kujaza fomu inayopatikana mtandaoni.
Mwisho wa kutuma maombi
16 March 2017
Kwa maelezo zaidi watafute kupitia testing
YA MSINGI KATIKA KUOMBA RUZUKU
Kila mfadhili ana utaratibu au namna ya uombaji wa ruzuku, kwa The Hilden, uombaji ni rahisi kwa mtu mwenye uelewa na uzoefu katika masuala ya ruzuku (granting). Kuna vitu vya msingi vya kuzingatia katika fomu yao ya uombaji
1. Kutambua wanufaika wa mradi (target group/beneficiaries), ni vyema ukawatambua kwa namba; mfano Wanawake 150 kutoka kata ya Midizini .
2. Tathmini ya matokeo (Benefit/Impact evaluation), hapa mfadhili anataka umuonyeshe ni kwa kiasi na kwa namna gani mradi umeleta kile kilichokuwa kikitarajiwa?. Ni vyema ukatumia ushahidi wa kitakwimu, mfano namba ya wanawake waliowezeshwa na mradi katika eneo husika n.k
The Consult +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania