TAARIFA: Maendeleo ya Afya ya Kibanda

TAARIFA: Maendeleo ya Afya ya Kibanda

Polisi watakuwa wanavuta bangi jamani!! mtu keshalala na amezungukwa na polisi wapatao kumi kwa nini umuonyeshee mtutu?
1.JPG
 
Hii nchi inatakiwa waombaji wa kuomba toba juu ya matendo haya machafu na mabaya. Mungu ni mwema atatusikia. Amen
 
Taarifa ya maendeleo ya afya ya Kibanda jioni hii....

Habari za jioni wakuu,

Muda umekwenda lakini nimeona ni vyema tukashirikishana taarifa fupi tulizopata kutoka Afrika Kusini anakotibiwa Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda kama nilivyoahidi.

1. Tangu walipowasili jana katika hosipitali ya Milpark, Kibanda amekuwa akiendelea na matibabu kwa maana ya kufanyiwa vipimo mbalimbali vikiwamo CT Scan na X Ray hasa kichwani na sehemu nyingine za mwili ambazo zilipata majeraha.

2. Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo, jopo la madaktari wenye ujuzi wa aina tofauti, walikuwa akitarajiwa kukutana ili kusoma taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo, ili kutafsiri maana ya matokeo hayo kisha kutoa mwelekeo wa nini kinafuata au aina ya tiba anayopaswa kupata Kibanda.

3. Taarifa nyingine ni kwamba, imebainika kwamba mfupa laini (fizi) uliopo kati ya pua na mdomo ni kama umekatika. Hii natokana na nguvu na nyenzo walizotumia watesaji kumg’oa meno. Kutokana na hali hiyo ana maumivu makali sana kwenye kinywa chake.

4. Pia imebainika kwamba meno kama sita hivi katika kinywa cha Kibanda yamelegea. Haya ni tofauti na yale mawili yaliyong’olewa katika tukio la awali.

5. Kesho Ijumaa Jukwaa la Wahariri litakutana katika mkutano wa wahariri wote ili kujadili hatua zaidi za kuchukua kwa maana mbili; kwanza ni kuhusu matibabu na afya ya Kibanda na pili usalama wa waandishi wa habari kikazi.

6. Uongozi wa Taasisi iitwayo Southern African Investigative Journalism Forum umemtembelea Kibanda katika hosipitali ya Milpark na kueleza masikitiko yake kuhusu yaliyomkuta. Wameahidi kushirikiana na taasisi za kihabari za Tanzania, kuchunguza tukio hilo kwa lengo la kupata majawabu ya nini kilichojiri na sababu za unyama huo.

Tutaendelea kuwaarifu hatua kwa hatua jinsi tutakavyokuwa tukipata taarifa kutoka Afrika Kusini.

--

Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

Mkuu, wewe ni ndugu wa familia? mbona wakati ulimboka anatibiwa siri za matibabu yake hazikuvuja? AU MNAFANYA hayo yote kwa lengo la kuchochea maandamano. mimi ni Daktari na maadili yetu ya kazi haituruhusu kutoa siri za mgonjwa kwenye public. ninaamini hata madaktari wa South Afrika hawana tofauti na hapa kwetu kwani fani ni moja tu na tunafuata international standards code of conduct. ninaamini hizo si taarifa za kidaktari bali ni za watu ambao hukaa pembeni kuzusha mambo ili watu wote tuelekeze fikra huko
 
Asante kwa taarifa hii, tuendelee kumwombea mwenyezi Mungu ampe nguvu ya kuvumilia mateso anayopata Ndugu yetu Kibanda. Get well soon Kibanda.
 
mkuu, wewe ni ndugu wa familia? Mbona wakati ulimboka anatibiwa siri za matibabu yake hazikuvuja? Au mnafanya hayo yote kwa lengo la kuchochea maandamano. Mimi ni daktari na maadili yetu ya kazi haituruhusu kutoa siri za mgonjwa kwenye public. Ninaamini hata madaktari wa south afrika hawana tofauti na hapa kwetu kwani fani ni moja tu na tunafuata international standards code of conduct. Ninaamini hizo si taarifa za kidaktari bali ni za watu ambao hukaa pembeni kuzusha mambo ili watu wote tuelekeze fikra huko
wewe ni daktari uchwara full stop.umetrain chuo gani?
 
Mungu atakuponya Mr. Kibanda.
Inasikitisha, Tanzania tunaelekea wapi... nani atatusemea kama mdomo wa wanyonge (wanahabari) unashonwa kwa mnyororo wa chuma....

watatumaliza....
 
Pole sana Kaka yetu. Mungu wetu ni mwaminifu sana. Get well soon.
 
mkuu, wewe ni ndugu wa familia? Mbona wakati ulimboka anatibiwa siri za matibabu yake hazikuvuja? Au mnafanya hayo yote kwa lengo la kuchochea maandamano. Mimi ni daktari na maadili yetu ya kazi haituruhusu kutoa siri za mgonjwa kwenye public. Ninaamini hata madaktari wa south afrika hawana tofauti na hapa kwetu kwani fani ni moja tu na tunafuata international standards code of conduct. Ninaamini hizo si taarifa za kidaktari bali ni za watu ambao hukaa pembeni kuzusha mambo ili watu wote tuelekeze fikra huko
wewe ni daktari uchwara full stop,hapa ndio umeandika nini sasa bwana ?doctor
 
KOVA yuko tanganyika perkas anatafuta waliomtesa kibanda wakato wanaenda kutubu kwa mchungaji gwajima,fara kweli lakini malipo ni hapa duniani muache atumike kama condomu
 
Mkuu tofautisha uvumilivu na kutojitambua; Amini usiamini matukio ya kutekwa na kuteswa kwa waandishi wa habari na serikali ikiendeleza utamaduni wake wa kutoa majibu ya kukera, hayawezi tokea nchi yoyote ile isipokuwa Tanzania.

......

Hayo ndo majibu ya "sirikali sikivu" Mungu si dhalimu..., ipo siku mambo yatakuwa hadharani.
 
Ahsante kwa taarifa. Mungu amjalie pona ya haraka.
waandishi mue kitu kimoja katika hatua yoyote mtayokubaliana kuichukua..wachache wenye uwezo mkubwa wa kujipendekeza wasiwavunje moyo acha wajiabishe.
 
Mkuu, wewe ni ndugu wa
familia? mbona wakati ulimboka anatibiwa siri za matibabu yake
hazikuvuja? AU MNAFANYA hayo yote kwa lengo la kuchochea maandamano.
mimi ni Daktari na maadili yetu ya kazi haituruhusu kutoa siri za
mgonjwa kwenye public. ninaamini hata madaktari wa South Afrika hawana
tofauti na hapa kwetu kwani fani ni moja tu na tunafuata international
standards code of conduct. ninaamini hizo si taarifa za kidaktari bali
ni za watu ambao hukaa pembeni kuzusha mambo ili watu wote tuelekeze
fikra huko

Huyu katumwa! Mwogopeni kama ukoma. Anaongea kwa jazba kwa lengo la kuficha siri.... Hana uchungu wowote!!!
 
Mkuu, wewe ni ndugu wa familia? mbona wakati ulimboka anatibiwa siri za matibabu yake hazikuvuja? AU MNAFANYA hayo yote kwa lengo la kuchochea maandamano. mimi ni Daktari na maadili yetu ya kazi haituruhusu kutoa siri za mgonjwa kwenye public. ninaamini hata madaktari wa South Afrika hawana tofauti na hapa kwetu kwani fani ni moja tu na tunafuata international standards code of conduct. ninaamini hizo si taarifa za kidaktari bali ni za watu ambao hukaa pembeni kuzusha mambo ili watu wote tuelekeze fikra huko

Umesema sawa kua madaktari hamruhusiwi kutoa taarifa za mgonjwa kwenye public but huyu aliezitoa si daktar so hiyo international standard code of conduct haim-bani, hiyo moja, bt pili, daktar anaweza kutoa taarifa za mgonjwa kwa public kama mgonjwa mwenyewe ameridhia kufanyika kwa hilo... af kwann umekuja na jazba?labla ungeanza kwa kuuliza kama ana ruhusa ya mgonjwa au ndugu zake ya kutoa hizi taarifa...na pia cheo chake + ruhusa vinamruhusu kutoa taarifa hii au???
udaktari wako ni kama wa kina maji marefu au km wa ------?
 
Get well soon Kibanda, na namwomba Mungu wetu sote akaseme na nyoyo zetu mmoja mmoja tukakumbuke kwamba tusiwatendee wenzetu yale ambayo tusingependa kutendewa, pia tukumbuke faida na furaha tunayoitafuta kwa kuwakanyaga na kuwadhulumu wenzetu ni nya muda na mola hatasita kutupatiliza:crying:
 
ROMA alishasema tanzania 2na uoga ha2na aman.
2zidi kumshirikisha mungu ktk uta2zi wa matatizo haya
watanzania 2kopamoja ktk kipind hik kigumu, 2tazidi kukuombea.
 
Pole sana Bw Kibanda na tunashukuru kwa TAARIFA.
 
ROMA alishasema tanzania 2na uoga ha2na aman.
2zidi kumshirikisha mungu ktk uta2zi wa matatizo haya
watanzania 2kopamoja ktk kipind hik kigumu, 2tazidi kukuombea.

Hapa Mjukuu wangu umeandika kidigitali zaidi. HakyaMungu!
 
Back
Top Bottom