TAARIFA: Maendeleo ya Afya ya Kibanda

TAARIFA: Maendeleo ya Afya ya Kibanda

Tunashukuru kwa taarifa na tunazidi kumwombea kwa Mungu ampe nafuu na apone haraka. Matukio haya yanalenga kuwanyamazisha waandishi wa habari msiripoti mambo muhimu ya maslahi kwa Taifa lakini msirudi nyuma kamwe, tunawaombea na ukweli utasimama daima.
 
Mwenyezi Mungu amsaidie apate kupona haraka.
 
Mungu aendelee kumlinda na kumponya ndugu yetu Kibanda!
Meena kwa nini mtu kama wewe usiwe verified user unatumia vivuli?
Poleni sana kwa yaliyo mkuta mwenzenu! Hakika wana habari hampo salama kabisa!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tofautisha uvumilivu na kutojitambua; Amini usiamini matukio ya kutekwa na kuteswa kwa waandishi wa habari na serikali ikiendeleza utamaduni wake wa kutoa majibu ya kukera, hayawezi tokea nchi yoyote ile isipokuwa Tanzania.

kama wangesimama kidete kwenye issue ya ulimboka na mwangosi wakaakisha ukweli aufinyangwi hili lisingeweza kutokea.mungu amjalie kibanda kupona haraka ila kama atakuwa na mpango wa kuanika ukweli asije fanya kama ulimboka
 
Shida yetu sisi Watanganyika ni kuandamania moyoni na kukiuka amri ya Mungu ya kulitajataja jina lake bure! Tuchukie hatua
 
Tunashukuru kwa taarifa na tunazidi kumwombea kwa Mungu ampe nafuu na apone haraka. Matukio haya yanalenga kuwanyamazisha waandishi wa habari msiripoti mambo muhimu ya maslahi kwa Taifa lakini msirudi nyuma kamwe, tunawaombea na ukweli utasimama daima.

usilitaje jina la Mungu ovyo! Chukua hatua
 
Inasikitisha sana Mungu atamjalia atapona haraka.
 
Mungu ampe afya njema. Wote waliodhulumu afya yake Mungu atawaadhibu.
 
Waliofanya kitendo hiki walaaniwe kuingia kwao na kutoka kwao,hivi waliwakosea nini wanyakyusa?loo!!mungu uliye hai nyosha mkono wako umguse mwanao.
 
Mungu akujalie afya ya roho na mwili upone haraka ujumuike na ndg, jamaa na marafiki katika ujenzi wa taifa.

Hakika kwa mwendo huu nakosa kujua mwisho wa siku haya mambo yataisha vipi, Nakumbuka kauli ya Waziri mkuu mstafu wa awamu ya tatu Mh. Fedrick T. Sumaye muda mfupi baada ya mchakato wa kumtafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2005 kuisha, Duh nakosa jibu.
 
Hivi wa Tanzani tunataka mpaka hawa jamaa watufanye nini? hivi kweli watu zaidi ya milioni 40 mpaka tunatiwa vidole na watu hata hawazidi 200. Kama tumelogwa basi nafikiri hata huyo mchawi amekufa!
 
Machi 08, 2013


Madaktari katika Hospitali ya Millpark, Afrika Kusini wamebaini madhara zaidi aliyopata Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef), Absalom Kibanda kutokana na unyama aliofanyiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia juzi.

Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alitekwa, kupigwa na kujeruhiwa vibaya na juzi alasiri alisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.


Habari zilizopatikana jana kutoka Afrika Kusini na kuthibitishwa na uongozi wa Tef zinasema madaktari wanaomtibu Kibanda walibaini madhara zaidi ambayo ni pamoja na kukatika kwa mfupa laini (fizi) unaounganisha pua na mdomo pamoja na kulegea kwa meno takriban sita.

Taarifa ya Tef iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Neville Meena imesema athari hiyo imesababishwa na nguvu na nyenzo walizotumia watesaji kumng'oa meno... "Kutokana na hali hiyo ana maumivu makali sana kwenye kinywa chake."


Kuhusu meno, Meena alisema hayo sita yaliyoelezwa kwamba yamelegea ni mbali na yale mawili yaliyong'olewa katika tukio la awali.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Tef, Kibanda alifanyiwa uchunguzi wa kitabibu na baadaye jana jioni, madaktari walikuwa wakitarajiwa kusoma taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo, ili kutafsiri maana ya matokeo yake kisha kutoa mwelekeo wa nini kinafuata au aina ya tiba inayopaswa kutolewa.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006), Hussein Bashe alisema madaktari walianza kazi hiyo baada ya Kibanda kufikishwa hospitali hapo juzi usiku.
"Tunashukuru walifika salama, tatizo lilikuwa Uwanja wa Ndege wa Johannesburg, walichelewa kama saa moja hivi kwa masuala ya Uhamiaji, lakini baada ya hapo alipelekwa hospitali."


"Kwa kuwa alipigwa sindano ya kutuliza maumivu pamoja na usingizi wakati anaondoka, sasa baada ya kuimarika kiakili, alipelekwa chumba cha upasuaji kuangalia jinsi gani ya kulihudumia jicho na hicho kilikuwa kitu cha kwanza na wakati huohuo alianza kufanyiwa uchunguzi ili kujua ameumizwa kiasi gani."


Katika hatua nyingine, uongozi wa Taasisi iitwayo Southern African Investigative Journalism Forum, jana ulimtembelea Kibanda hospitalini na kueleza masikitiko yake kuhusu yaliyomkuta.


Uongozi huo uliahidi kushirikiana na taasisi za kihabari za Tanzania, kuchunguza tukio hilo kwa lengo la kupata majawabu ya nini kilichojiri na sababu zake.
Leo Tef watakuwa na mkutano wa wahariri wote kujadili hatua zaidi za kuchukua kwa maana mbili; kwanza kuhusu matibabu na afya ya Kibanda na pili usalama wa waandishi wa habari kikazi.


Kibanda alitekwa na watu wasiofahamika ambao walimshambulia kwa nondo na mapanga na kumng'oa meno mawili, kucha na kumjeruhi jicho la kushoto usiku wa kuamkia juzi.

Mwananchi
 
Hii ndo tanzania, waandishi wa habari na wanaharakati hawana usalama tena,kwa nchi iitwayo kisiwa cha Amani!
 
1.JPG
 
Huwa najiona kama nipo ukimbizini katika nchi hii ambapo huwezi kupata tafsiri sahihi ya HAKI na UHURU!
 
masthead-logo.gif

Tanzanian journalist killed reporting police-opposition clash

* Photos of dead man uploaded onto Internet
* Editor blames police, who deny responsibility, say they opened investigation
* Opposition, activists demand independent inquiry
By Fumbuka Ng'wanakilala
DAR ES SALAAM, Sept 4 (Reuters) - A leading Tanzanian editor accused police on Tuesday of beating up and killing television journalist Daudi Mwangosi, who died on Sunday during clashes between anti-riot police and supporters of the opposition CHADEMA party.

A police commissioner denied police responsibility but said he had ordered a joint military-police inquiry into the killing. Photos of the victim were uploaded onto the Internet and published by local newspapers.


Opposition leaders and activists linked the incident to a wider trend of rapidly growing violence against dissent in Tanzania and called for an independent inquiry.


Mwangosi was killed in a village in the Iringa region, about 500 km (315 miles) west of the capital Dar es Salaam, while reporting the clashes between police and CHADEMA supporters.
It was the first time in modern Tanzanian history that a journalist had been killed while doing his job, the Tanzania Editors' Forum (TEF) said. "It was a deliberate move by the police, who clearly targeted this journalist. Eyewitnesses said the journalist was surrounded by police, beaten up and brutally killed," TEF secretary-general Neville Meena told Reuters.

Police fired a tear gas shell into Daudi's stomach at close range, Meena said. "Photos of fragments of Daudi's blown-up body hit the Internet less than one hour after the incident. We believe that the police are deliberately targeting journalists in a violent crackdown."

The police denied responsibility and said they had moved in to disperse an illegal gathering of opposition supporters. "Police deny any deliberate involvement in the death of the journalist," police commissioner of operations Paul Chagonja said in a statement. "A commission of inquiry comprising officials from the police and military has been formed to investigate the death of the journalist." Journalists at the scene uploaded images onto the Internet that they said showed Mwangosi's mutilated body lying on the ground, his abdomen ripped open and intestines spilling out.

Local newspapers published photos that showed a man lying on the ground, surrounded by anti-riot police officers who were beating him. The newspapers identified the man as Mwangosi, though the face was not recognisable.
"We condemn the killing ..." the Guardian newspaper of Tanzania said in an editorial. "It is unacceptable for the government and the public to rely on police investigations, knowing only too well that they are in this case one of the parties being blamed for the death of our colleague," it added.
Mwangosi's death came a week after one person was killed and several were wounded when police fired tear gas to break up an opposition protest in Morogoro town, a stronghold of the ruling CCM party. (Editing by Yara Bayoumy and Tim Pearce)
 
Back
Top Bottom