Taarifa kwa vyombo vya habari (uchomaji mabanda moto zanzibar) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa vyombo vya habari (uchomaji mabanda moto zanzibar)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHIBUU, May 20, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kumekuwa na kauli nyingi tokea kamati ya bunge kuja Zanzibar, kukusanya maoni kuhusuru rasimu ya marekebisho ya katiba. Na wazanzibar wakaonesha msimamo wao kuhusu mustakbal wa nchi yao , na kuukataa mswada huo,Imekuwa ni kosa mpaka viongozi wa Dini wakaitwa wahuni.

  JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
  للجنة الدعوة الإسلامية
  THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
  P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- E-Mail: jumiki@hotmail.com MKUNAZINI- ZANZIBAR

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  18/05/2011

  Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma.Rehma na amani zimshukie kipenzi chetu Mtume (S.A.W.) na ahli zake na jamaa zake na waliowema katika Uslamu.

  Kutokana na matukio yaliojitokeza katika nchi na ambayo yanaweza kuleta mgawanyiko,chuki,na nchi kuingia katika mgogoro usio wa lazima,jumuiya ya UAMSHO imeona ichukuwe nayo nafasi kuelezea uoni wake juu ya hayo yaliojiri.

  Kimsingi kuna matukio matatu yaliotokea Zanzibar ambayo sasa yanaonekana kuwa gumzo Zanzibar na Bara.

  • Kwanza . Suala la kuchomwa moto kwa mabanda ya biashara huko pwani mchangani
  • Pili. Suala la serikali ya S.M.Z chini ya mfumo wa umoja wa kitaifa.
  • Tatu. Maoni ya Zanzibar kuhusu mswada wa mapendekezo ya marekebisho ya katiba.

  1. Suala la tukio la pwani mchangani la kuchomwa moto mambanda ya wafanya biashara linapotoshwa kwa makusudi na watu wasioitakia Zanzibar kheri.
  2. Sikweli kama mabanda hayo yaliochomwa ni 70. kama livyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, idadi ni 29.
  3. Wamiliki wa mabanda hayo si wabara kama inavyo elezwa 27 ni ya wazanzibar na mawili tu ndio ya wabara.
  4. Sikweli kua tukio hilo ni la kisiasa bali ni la kijamii baada ya malalamiko ya wananchi kulalamika kutokana na vitendo vya ubakaji,umalaya,ulevi,mauaji, biashara ya unga,
  5. Si suala la kuvunja muungano kwani baada ya malalamiko hayo na kuthibitishwa na vyombo husika serikali za mitaa iliwataka wafanya biashara hao kuondoka katika eneo hilo ifikapo tarehe 01/05/2011 wawe wameondoka katika eneo hilo sasa je serekali za mitaa zilitaka kufunja muungano?
  6. Sikweli kuwa wabara wanafukuzwa au kunyanyaswa Zanzibar ,wapo wafanya biashara wengi mji mkongwe marikiti wauza njugu,wanaofanya kazi mashambani za kulima mbona hawa hawajabughudhiwa?
  7. Jibu hawajafanya vitendo au biashara za uhuni unga,ulevi, nk.Na hii hoja ya kuwa wazanzibari wapo bara mbona habughudhiwi suala ni wazanzibar gain wanaofanya biashara ya ulevi,unga ubakaji,ukahaba,halafu serikali ikawaachia kwa kisingizio cha muungano?
  8. Suala nani kachoma na kwanini kachoma liko mahakamini tuiwachie mahakama iamumuwe kwa mujibu wa sheria.
  Masikitiko yetu makubwa na yenye masuala mengi bila jawabu ni kauli ya waziri wa mambo ya ndani mh:Shamsi Vuai Nahodha kukurupaka na kuwa hawa waliochoma ni wahalifu ,wanataka kufunja muungano na yeye kama waziri atahakikisha waliohusuka wanachukuliwa hatua.

  Sasa suala kuhusu hawa wafanya biashara kharamu,ambao wanachi na vyombo vya serikali vimeamua wahame,je mbona hawa hakutaja sababu zilizopelekea kupewa amri ya kuhama?

  Kauli za Mh:Nahodha zimewachukiza waislamu na wazanzibar na wameanza
  Kumtafsiri kuwa ni miongoni mwa wasioitakia mema Zanzibar .

  Tunawasihi waislamu na wananchi kwa jumla kutokubali katika kipindi hichi kupokea fitna za kutaka kuwagawa na kupandikiza chuki baina yetu.
  Pili tunaiyomba serikali kuchukuwa khatua zinazo faa kwa gazeti la NIPE HABARI, kutokana na taarifa zake za kuhatarisha amani ya nchi za tarehe 13-19 mei 2011 kwa taarifa zake zilizopewa nafasi ya mbele UZANZIBARI,UZANZIBARA SASA WANUKIA ZANZIBAR. Ni taarifa zinazo weza kulitia taifa katika khatari ya vita vya kikabila na dini,

  Pili: suala la serikali ya S.M.Z. yenye kufuata mfumo wa umoja wa kitaifa.
  Kumeanza kujitokeza watu kutaka kujenga fitna ili wazanzibar wanze chuki na viongozi wao na kuidhofisha serikali na kuirejesha nchi ya Zanzibar katika matatizo yale ya nyuma.

  Kidogo tukumbushe angalau watu wajielewe tunapo toka na tulipo sasa

  Kwa miaka 46.kuanzia mwaka 1961 hadi mwaka 2005, Zanzibar imeshaingia katika chaguzi sita zinazohusisha vyama vingi vya siasa, lakini matokeo ya chaguzi zote hizo ni kudhalilika kwa waislamu,dini yao na utamaduni wao.

  Hakuna uchaguzi wowote wa vyama vingi ambao umepita Zanzibar, bila ya kuwacha athari mbaya kwa wazanzibari.matokeo yake ni kuwa kila uchaguzi mmoja unapofanyika huwa msingi umechimbwa kwa jengo la mateso na mfarakano kwa uchaguzi ujao.

  Kwa mfano, uchaguzi wa pili wa juni 1961, chuki ya utumwa na ubwana,na Uarabu na Uafrika iliyopandikizwa kwa makusudi,ilipelekea waislamu zaid ya 70 kuuliwa huku watoto wa kiislamu katika kijiji cha bambi wakateketezwa kwa moto kwenye tanuri la mbata katika kijiji cha bambi.

  Uchaguzi wa 1995 uliofanyika baada ya miaka zaidi ya 30 tangu mapinduzi ya 1964 na kufutwa kwa vyama vingi,haukupunguza chochote katika madhila ya waislamu wa Zanzibar,isipokuwa kuongeza.

  Fitina ya upemba na uunguja ilipaliliwa na taasisi za dola na matokeo yake yakawa ni kuwafanya waislamu wan chi hii waangaliane kwa misingi ya maeneo wanayotoka na sio kwa Mungu Mmoja wa Haki wanayemuuamini na kumuuabudu. Badala ya kusimama na kalima tukufu ya laa ilaah illallah,muhamadarasuulullah, waislamu wa Zanzibar wakawa wanasimama na kauli za upemba na uunguja,uarabu na uafrika na ubwana na utumwa!
  Uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005 mambo yakawa ni yale yale.

  Tena majeshi yakamwagwa mitaani yakiwa na silaha za kivita. Rais wa wakati huo wa Tanzania, ambaye ni Amiri jeshi mkuu,Benjamin mkapa, alipoulizwa na waandishi wa habari sababu za kupeleka majeshi na vifaru Zanzibar,naye aliwauliza kulikuwa na sababu gain kwa wamarekani kupeleka wanajeshi iraq.

  Kwa hivyo nchi ya waislamu ya Zanzibar ikawa imevamiwa na majeshi ya kigeni kama vile iraq ilivyokuwa imevamiwa na marekani. Matokeo yake ikawa ni muendelezo wa kile Rais Jakaya kikwete alichokuja kukiita "mpasuko" wa Zanzibar .

  Hata baada ya matokeo ya chaguzi hizo na matokeo kutangazwa, waislamu wakawa wakifuatwa majumbani na misikitini kupingwa na kudhalilishwa kupita kiasi. Matokeo yake, makundi ya vijana wa kiislamu wakaanza kuhama visiwa hivi na kukimbilia ughaibuni,ambako wameselelea hadi leo.

  Miongoni mwa athari za vijana hao wa kiislamu wa kizanzibari kuselelea ugenini ni kupoteza kwa maadili ya dini yao na hivyo kuudhoofisha Uislamu.
  Kwetu sisi huu ni mpasuko baina ya Waislamu, ambao mashiko yake hayako katika uislamu lakini athari zake zinawapata waislamu wa Zanzibar, tunaamini kwamba Zanzibar inapigwa vita kwa sababu ya Uislamu wake.

  Tukumbuke kulijitokeza taasisi za kigeni jumuiya ya madola na pia kamati ya vyama vya siasa vyote vilishidwa kuziba mpasuko huo.hii imetokana na wengine hawakuwa na nia nzuri na Zanzibar.

  Baada ya madhara yote haya ambayo yamegharimu maisha ya watu, mali kupotea na mateso ya kila aina, wanzanzibar wenyewe wenye uchungu na nchi yao wakaona huku inakoelekea Zanzibar ni kubaya na wakuionea huruma Zanzibar ni wenyewe.

  Mh: Amani Karume na Mh: Maalim Seif wakaamua kuzika yale yote tulioyaeleza kwa ufupi yakaja maridhiano, na nia ni kujenga Zanzibar mpya yenye amani utulivu umoja na maendeleo.sote tukakubali kufuta tafauti zetu na kujenga umoja na tukaahidi kushirikiana na viongozi kujenga Zanzibar mpya yenye maendeleo. Na hilo litafanikiwa kwa kuwepo serikali ya umoja,wengi wa wazanzibari wakawafiki hilo .

  Sasa matunda ya maridhiano tumeanza kuyaona katika uchaguzi mkuu 2010 namna ya amani utulivu ulivyo tawala na hata baada ya matokeo wote wazanzibari walisherehekea kwa pamoja. Hakuna aliyepingwa,kubakwa,kuuliwa,wala kuharibiwa mali.haya ndio maamuzi ya wazanzibar.

  Sasa kumeanza kujitokeza watu kutaka kuidhofisha juhudi hii yote kwa kisingizio cha kuwa serikali iliyopo haina la maana.na kuanza kuwakashfu viongozi wa juu kuwa waregevu. Hawa tunawahisabu ni maaduwi wa Zanzibar .

  Na upo wasisiwasi kuwa baadhi ya viongozi wa bara hawakupendezewa na hali hii na wengine wakataka kuwafurahisha kwa vitendo na kauli ili waonekane wao wema, au bora kuliko wengine.

  Na hii imetutia wasiwasi zaidi baada ya afisa wa ubalozi wa marekani alioko Zanzibar kuanza kupita kuhoji watu kuhusu uwoni juu ya serikali na tukio la pwani mchangani.

  Hatua ya afisa huyu, inaweza kusababisha mgawanyiko, tuko macho na hatua za ya afisa huyo, na tukibaini kuna uchochezi au fitna hatuto weza kumvumlia.

  Tunatamka wazi hatuko tayari kumnyamazia kiongozi au yoyote awe wa nje au ndani kutaka kuleta fitna na mgawanyiko miongini mwetu
  Suala la ugumu wa maisha kupanda kwa bei bidhaa,bserikali inalielewa na tunaamini Rais wa Zanzibar na baraza lake wako makini kulitafutia ufumbuzi, huku tukiamini mabadiliko yatapatikana.

  Si kweli kwamba serikali haina la maana inalofanya wanaosema hivyo wanataka kujenga fitna kwa wazanzibar waanze kuchukia serikali yao .
  Tunasema nafasi hiyo haipo tena Zanzibar .

  Wito wazanzibar tuwe macho na maaduwi

  Suala la Tatu : Kuhusu Muungano

  Kumekuwa na kauli nyingi tokea kamati ya bunge kuja Zanzibar , kukusanya maoni kuhusuru rasimu ya marekebisho ya katiba. Na wazanzibar wakaonesha msimamo wao kuhusu mustakbal wa nchi yao , na kuukataa mswada huo, imekuwa ni kosa mpaka viongozi wa Dini wakaitwa wahuni.

  Mengi yamesemwa na hoja mbali mbali zinatolewa kulazimisha wazanzibari kukubali Muungano, tunasema miaka 47 ya Muungano huu umedumu kwa heshima na ustahamilivu wa wazanzibar, na kwa muda wote wamezibwa watu mdomo kuhoji au kukosowa kuhusu Muungano.

  Tunasema karne hizo zimekwisha.

  Muungano huu tokea kuundwa kwake umekuwa na kasoro nyingi na kuundiwa tume 21 na bado kasoro zipo pale pale.
  Nasaha zetu iko haja kujadiliwa upya muungano na pande zote mbili na kushauriwa watanganyika na wazanzibar kuhusu mfumo wa muungano wanaoutaka.

  Kinyume na hivyo kunaweza kukazuka mgogoro mkubwa na unaoweza kuleta uvunjifu wa amani

  Mwisho
  Tunatowa wito kwa serikali ya Zanzibar kulitatuwa tatizo la wafanya biashara wa jua kali ambao kwa muda wa miezi mine maduka yao yamefungwa, ingawa shauri lao lipo mahakamani.

  Serikali ifikirie njia ya kuwaokowa wafanya biashara hao ili kuondosha dhana potofu na maaduwi wakapata njia ya kuitia sumu jamii.

  WABILAH TAUFIQ

  AZZAN KHALID HAMDAN
  NAIBU AMIRI (JUMIKI)
   
 2. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  SASA nyie taasisi ya Dini mnahusikaje, au inakuwaje muwajibike kutoa hii ripoti...
  au mlihusika? haya ni mambo ya kiutawala, viachiwe vyombo husika, kama polisi na mahakama vishughulikie..
   
 3. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kulingana na hayo yaliyoandikwa, hao jamaa wao ni kila kitu. Watafiti, wanasiasa, mahakama na kila kitu.
   
 4. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Nyie mna issue nyingi sana kuliko tunavyofikiri...

  Nimesikitishwa na kauli yenu kama taasisi ya kidini kuwaona wabara kama ni watenda dhambi kuliko wazanzibar. Mnataka kutuambia wabwia unga, malaya (makahaba) na mashoga, wote ni wabara?? na je wanayafanya hao peke yao kama wabara bila kushirikiana na wazinzabar...

  na nyie kama taasisi ya kidini kwa nini msiwahuburie wabadilike, kuliko kuwachomea mabanda yao..Mngewaua basi, tujue moja..
  Nia yenu ni kuitangaza Zanzibar kama Islamic state, ni bora mfanye hivyo kuliko kuzunguka point..
  Pia mnatudhalilisha 'wabara' kwa kauli zenu chafu za kutuona sisi ni watenda dhambi sana..
   
 5. K

  Kaboya Kenneth Senior Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 110
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Ahsante kwa habari za upande wa wachomaji, lakini jifunzeni kutuhumu na si kuhukumu.
   
 6. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,420
  Trophy Points: 280
  Mbona hawajasema kwa nini JK ameipongeza Marekani kwa kumuua Sheikh Osama
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  is zanzibar an Official Islamic Republic !!???
   
 8. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  These Zanzibaris want to eat their cake and still have it!! Haiwezekani!
   
 9. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,877
  Trophy Points: 280
  Kwani hii jumuiya inatoa tamko kama nani au kwa niaba ya nani?
   
 10. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Hii inatoa tamko kama nijumiya ya waislamu zanzibar kwa kuwakilisha wanachi kama ni organization ambayo isiyo ya kiserikali na inapambana na mabo ya kijamii,zanzbar asimilia 99 ni waislamu fahamu hilo. Tunawaheshimu sana hawa vongozi wetu.
   
 11. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Sasa hii LHRC ni chombo cha kiutawala au vipi? JUMIKI ni Taasisi iliosajiliwa rasmi na ina haki ya kutoa maoni yake. Huo ni uhuru wao wa Kikatiba (yetu, sijui yenu).
   
 12. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  UPUUZI MTUPU!↲
   
 13. Rangi Mbili

  Rangi Mbili Member

  #13
  May 20, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uhuru wenu ndo unawafanya muwatukane 'wabara' (watanganyika)??? Mmesajiliwa kama taaisisi ya kidini au ya kijamii?

  Yaani nyie wazanzibari mnajichanganya wenyewe tu
   
 14. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanganyika wametukanwa wapi na nani?
   
 15. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,602
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  Hao Jumiki wangetusaidia kutueleza, ni mafundisho yepi katika uislamu yanaruhusu Raia kujichukulia sheria mkononi bila kufuata mamlaka ya nchi?.
  Watueleze tujifunze, ni mafundisho gani ya uislamu yanaruhusu kuharibu mali ya "mkosaji", bila ya kuleta mashahidi, na kesi mbele ya "kadhi" au mamlaka ya sheria?, maana hata huo uzinifu lazima ulete mashahidi wanne ati!.

  Hao Jumiki wanaleta Siasa mbele ya mambo ya kisheria, nadhani hao si wa kuwatilia maanani katika suala hili.
  Sheria ichukue mkondo wake, na Wazanzibari waache Ubaguzi!.
   
 16. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono mkuu, kwakuwa 99% ni waislam hakuna haja ya kutii mamlaka ya kiserikali, mtu akifanya ndivyosivyo anaadhibiwa mara moja na al-shabab kwa maagizo ya kiongozi wa kiislam. Nashangaa kwanini serikali inapoteza pesa nyingi kuchagua viongozi wakati watu hawawatii. Nashauri viongozi wote wa kisiasa na kiserikali waondolewe wabaki mashehe na maimam waongoze nchi.
   
 17. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Ingelikuwa vizuri iwe islammic state,,,,Nyerere alitupindua mwaka 1964 alihofia zanzibar kuinuka kiunchumi,na kuona choyo kabisa,pia kuwa ni islamic state katika east africa mashariki,na nyerere alikuwa mkatoliki,ilikuwa ni zamira zake ku distory uislamu east africa mashariki,ikiwa sehemu hizo , zanzibar na ilikuwa uganda wakati wa eddi amini,usilamu ulitanda katika nchi ya uganda kabla nyerere hakupindua serikali ya eddi amini.

   
 18. Rangi Mbili

  Rangi Mbili Member

  #18
  May 21, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ina maana wewe hujasoma hiyo habari hapo juu??
   
 19. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na hilo la kutaka Sheria ichukue mkondo wake ndio JUMIKI inalotaka lifanyike na sio nyinyi kuanza kupandikiza chuki.

  JUMIKI inatahadharisha, isitolewe hukumu kabla uchunguzi kamili kufanyika.

  Pili kuwaonya viongozi wa kisiasa kutoa hukumu wakati kesi iko Mahkamani.(refer matamshi ya Makamo wa Pili wa Rais na Waziri wa Mambo ya Ndani).

  Au mkitaka mpate nafasi ya kuwavunjia maduka hao mnaowaita Wapemba mpate kuwaibia?

  Angaieni sana, msije mkakosa pa kukopa tu.
   
 20. DON KILLUMINATI

  DON KILLUMINATI Senior Member

  #20
  May 21, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  duh, ilim madrasa kaaaz kwel kwel
   
Loading...