TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Jul 21, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Isambazwe Mara Moja

  Alhamis, Julai 21, 2011


  KUITISHWA KWA MAANDAMANO YA AMANI NA MKUTANO WA WAZI
  Mahali: Uwanja wa Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam
  Tarehe: 1 Agosti 2011


  Nikiwa kama Mtanzania, mpenda amani, raia wa KUZALIWA, Mzalendo Halisi mwenye kuipenda nchi yake, na kiongozi wa asasi-huru ya X Foundation yenye makazi yake Jijini Dar es Salaam, napenda kutoa taarifa kwamba, X Foundation inawaalika Watanzania wote waishio Dar es Salaam na kwingineko, kwamba, kutakuwa na Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi, siku ya Jumatatu, Agosti Mosi, 2011, kuanzia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke hadi Uwanja wa Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam. Watanzania mnaombwa kukusanyika KWA AMANI, kwenye eneo la wazi, nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, kuanzia saa 2 asubuhi. Maandamano yataanza rasmi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, takriban saa 4 kamili hadi Uwanja wa Mwembeyanga, Temeke, na yanatarajiwa kupokelewa na Mhe. Beatrice Matumbo Shellukindo (MB, Kilindi, CCM), akishirikiana na viongozi wa vyama mbali mbali vya kisiasa na kijamii, ambao watakuwa wamealikwa kuhudhuria.

  Dhumuni la Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi, tukio ambalo litafanyika kwa amani, linachagizwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, toleo la mwaka 1977, kama ifuatavyo:


  1. Msingi na Mustakabali: Serikali na Watu, Sheria ya 1984, Na. 15, ib. 6, kama ifuatavyo:
  8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
  (a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
  (b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
  (c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
  (d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.  1. Uhuru wa Mawazo: Uhuru wa Maoni, Sheria ya 1984, Na. 15, ib. 6, kama ifuatavyo:
  18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.


  1. Uhuru wa Kushirikiana na Wengine: Sheria ya 1984, Na. 15, ib. 6, kama ifuatavyo:
  20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

  1. Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa.


  1. Ulinzi wa Mali ya Umma: Sheria ya 1984, Na. 15, ib. 6, kama ifuatavyo:
  27.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.

  1. Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.

  Kutokana na mustakabali huu, mimi, nikiwa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninao uhuru, haki na wajibu wa kuzingatia masharti haya yaliyotajwa hapa juu, kama ifuatavyo:


  1. Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania imekuwa katika hali ya jumla ya kuyumba kwa uchumi wake, kuanzia mnamo mwaka 1994, wakati janga la nakisi ya nishati ya umeme lilipoikumba Jamhuri kwa mara ya kwanza, na kusababisha athari mbaya za kiuchumi
  2. Wizara ya Nishati na Madini ndiyo taasisi kuu ya Serikali ya Tanzania, ambayo, kwa mujibu wa Ibara ya 8-(1) ya Katiba, ibara ndogo ya (b), inatamkwa kwamba "wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii", kwa hiyo, Wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho ya kuamua mustakabali wa utendaji wa viongozi wa Wizara hiyo, ambayo ni taasisi yao, wao wakiwa wenye kutoa "madaraka na mamlaka" kwa Serikali.
  Kwa msingi huo mkuu, pamoja na misingi mingine iliyotajwa hapo juu, ninao uhuru, haki na wajibu wa kuitisha Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi, kwa lengo la kuwashinikiza viongozi watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini, yaani, Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu, kujiuzulu mara moja, ili kuwezesha utendaji wa Wizara hiyo kutendeka kwa ufanisi zaidi, kwani imeonekana dhahiri kwamba, katika kipindi cha uongozi wao wa Wizara hiyo, kipindi cha kwanza kikiwa cha 2005-2010, na cha pili kikiwa 2010-2015, hali ya ugavi wa nishati ya umeme imezidi kuwa mbaya kiasi cha sio tu kuathiri uchumi wa nchi, lakini pia, kuathiri vibaya zaidi maisha na mustakabali wa Watanzania kwa ujumla.

  Kutokana na usimamiaji mbovu wa utendaji wa Wizara, pamoja na mipango mizuri iliyowekwa hapo awali, na pia, kutosikiliza maoni ya Wabunge, hususan maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya inayohusika na sekta ya nishati, viongozi hawa walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, wamepuuza kabisa ushauri wa wataalam na wabunge, na katika utendaji wao mbovu, wameitia hasara kubwa Jamhuri hii, hivyo kusababisha upotevu wa mabilioni ya Shilingi, sio tu kutokana na Serikali kukosa kukusanya mapato kutokana na shughuli mbali mbali za uzalishaji kutoka kwenye viwanda, vingi ambavyo sasa vimefungwa, lakini pia, Serikali kukosa kukusanya mapato kutoka kwa wajasiriamali wadogo na wakati, hivyo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi mzuri zaidi.

  Kwa kuzingatia Masharti yaliyowekwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 27-(1) na (2), ninao uhuru, haki na wajibu wa kulinda mali ya umma, ikiwa ni pamoja na uchumi wa Jamhuri, lakini pia, kwa kuzingatia Ibara ya 18-(1) na 20-(1) na (2), ninao uhuru, haki na wajibu wa kutoa maoni yangu, na pia kushirikiana na watu wengine katika kutoa maoni hayo, ikiwa ni pamoja na kwenye hadhara, kupitia, kwa mfano, maandamano ya amani na mikusanyiko ya wazi, nikiwa na uhuru wa kutoingiliwa kati kwenye mawasiliano hayo ya amani.

  Leo, Alhamis, Julai 21, 2011, ninatamka, kwa faida ya Watanzania wote, kwamba, ifikapo tarehe 1 Agosti 2011, sisi Watanzania, tutakusanyika kwa amani na tutaandamana kwa amani, kama ilivyotajwa hapo juu, na tutafanya mkutano wa wazi na wa amani, ili kuweka bayana maoni na hisia zetu kuhusu janga hili kuu lililoifika nchi yetu.

  Tuhuma zinazowakabili watendaji hawa, wa kutaka kutoa hongo ya takriban Shilingi Bilioni Moja za Kitanzania, zitazungumziwa kwa undani na watu wenye taarifa kamili zaidi kwenye mkutano huo utakaofanyika Mwembeyanga, Temeke. Tunatoa maombi ya ushirikiano mwema kwa Watanzania wote katika maandalizi ya maandamano hayo na mkutano huo, ili kuleta ufanisi mzuri zaidi, kwani, penye umoja kuna nguvu, na penye wengi hapakosi mazuri.

  Watu wote wenye nia nzuri na nchi yetu wanaombwa kuwasiliana nami kwa njia ya simu na/au barua pepe kama inavyoainishwa hapa chini. Mimi ni mhamasishaji, ninao uhuru, haki na wajibu huo, lakini mustakabali wa nchi yetu ni wetu wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, au imani zetu za kidini, au rangi za ngozi zetu au makabila yetu, kwani, Tanzania ni moja, ni yetu wote, kila mtu anayeitwa Mtazania ana haki ya kuitetea na kuilinda nchi yake, akishirikiana na wenzake.

  Asanteni kwa Ushirikiano wenu.


  MwanaHaki

  Simu selula: +255-786-019019 na +255-786-019019

  Barua pepe: misterx@qi.co.tz
   

  Attached Files:

 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Huenda nikawepo
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  bado unatarajia ufumbuzi wa matatizo ya tanzania kutoka kwa ccm! hebu tudokeze, shelukindo alizuiwa kusema jambo lolote bungeni ili sasa aje kutuhutubia hapo m/yanga? kabla hujanishawishi weka jamvini b. shelukindo aliipataje barua iliyowalenga wakuu wa idara. mimi naona kama majukwaa ya sarakasi yanapangwa tayari kwa vikundi mbali mbali kuanza maonyesho ya sarakasi bin gimnastic.
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Mantiki na uwepo wa hayo maandamano ni nini? nimelisoma tamko lakini sijaona ni maandamano hayo ni ya nini? kupinga hayo kwenye katiba? kutaka yabadilishwe? au? nisaidieni kuelewa.
   
 5. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi kumbe wewe ni CCM? Nilikuwa sijuiiiii,,,, unauliza maandamano ya nini?
   
 6. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kama anaepokea maandamano hayo ni B shelukindo, halafu itatoka taarifa rasmi juu ya Jairo. Hayo ni maandamano ya CCM chini ya Shelukindo. Hao X foundation ni kivuli tu.
   
 7. C

  Chintu JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,402
  Likes Received: 856
  Trophy Points: 280
  Nafikiri lengo liwe kushinikiza serikali nzima ijiuzuru kwa sababu;
  Waziri mkuu kakiri bungeni kuwa hakuwa na taarifa kuhusu barua ya Jairo kuchangisha pesa. (tafsiri yangu ni kwamba, pamoja na mabilioni yanayotengwa kwa ajili ya usalama wa taifa ambayo Mh Mnyika (CHADEMA) aliyalalamikia sana na yakatetewa mno na Chikawe (CCM), lakini bado serikali ( yaani president, PM, na mawaziri wake wanakosa taarifa za kiintelijensia mpaka Beatrice anawashitua bungeni?????????)
  Kama wabunge wanaweza kupata taarifa za kiintelijensia kirahisi namna hii. iweje PM ashtushwe bungeni au ndo usanii wake kuwadanganya watanzania?
  Tatizo sio Ngeleja, wala Malima. maana kabla yao walikuwepo akina Karamagi, Msabaha nk. wakajiuzuru, lakini wapi. Tatizo ni system nzima. Usalama wa taifa hivi sasa kazi yao ni kuishughulikia CDM tu na kutafuta taarifa za kiintelijensia kuzuia maandamano yao. Inawezekana vipi tukaibiwa mabilioni yetu BoT na makampuni feki, na transactions zilizowazi kabisa kutiliwa shaka, lakini usalama wa taifa haujui bali Dr Slaa akajua??
  Richmond tumeibiwa Lowasa kajiuzuru, (tunaambiwa kastaafu)na hivyo bila shaka anakuwa treated kama mstaafu kwa maana ya marupurupu kama kawaida., Mnafiki Sitta na mwenzake Mwakyembe walituficha ukweli unaotutesa hadi leo. Ni Ukweli tu utakaotuweka huru watanzania na si propaganda za maandamano ya kukata matawi badala ya kungoa mzizi. mzizi huo ndio ule ukweli waliotuficha akina Mwakyembe na hoja kuzimwa na mnafiki Sitta.
   
 8. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Taarifa zimefika mkuu...
   
 9. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  We faza fox mbona madhumuni na malengo yamewekwa wazi

   
 10. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mh! ntarudi baadae maana huyu mama Shellukindo amekua kigeugeu na tunajua huo mkutano mratibu mkuu ni Lowassa na unaenibishia hili unatakiwa usome alama za nyakati kwa usahihi zaidi.
   
 11. V

  Vonix JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Shelukindo!!hapana atanizidishia machungu ni mmoja kati ya wale walioikimbia hoja ya Richmond wakatuacha kwenye mataa atakuja na nini zaidi ya kujishaua tu.
   
 12. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kama lengo ni kujadili matatizo ya umeme whats the problem.
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  MwanaHaki

  Simu selula: +255-786-019019 na +255-786-019019

  Barua pepe: misterx@qi.co.tz
   
 14. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  MwanaHaki

  Unaweza kutudokezea angalau kidogo misimamo ya viongozi wafuatao kama mmewasiliana nao au tayari wamepata mwaliko

  1. CCM- Mukama, Nape, Mkuchika, Lowassa
  2. Chadema- KUB, Slaa, Zitto,
  3. CUF- Lipumba, Seif, Mtatiro
  4. NCCR- Mbatia, Kafulila

  Wanaharakati wa Jamii
  1. Ananilea Nkya
  2. Kiwanga
  3. J. Ulimwengu
  4. .........nk
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Hapo kenye RED ndo umekosea hutoweza kupata mtu
  Maandamano ni ya kimagamba magamba
   
 16. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Maandamano ya kimagamba magamba zaidi

  naona anarudia number zake
   
 17. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nadhani tuandamane kuondoa tatizo la jumla kwa nchi yetu. Tatizo si umeme wajameni, tatizo ni "CCM", mkubali mkatae hilo ndio tatizo kuu. Bila kuiondoa CCM matatizo hayatokwisha. Loliondo wanalia kuuzwa kwa ardhi yao, kauza Ally Hassan Mwinyi (Kaua misingi ya uongozi, kabinafsisha makampuni ya umma kizembe, kauza ardhi yenye madini kwa wageni, katuingiza kwenye mikataba mibovu ya umeme wa dharula - IPTL na uoza mwingi tu. Ilifika wakati akageuza ikulu kuwa gulio), Kaingia Benjamin William Mkapa (Kamlinda mtangulizi wake, kaendeleza sera ya ubinafsishaji mashirika ya umma, kauza ardhi yenye madini kwa wageni, kaingiza nchi kwenye wizi wa fedha za umma - EPA, kaingia mikataba ya kitapeli - RADA, matumizi ya anasa yasiyo na tija - NDEGE YA RAIS, na uozo aina aina), sasa Jakaya Mrisho Kikwete (kaendelea na utamaduni wa CCM wa kulinda wanaccm wenzake, kasamehe wezi tena hadharani - EPA, kashindwa hata kurekebisha mikataba mibovu aliyoikuta, kaingia mikataba mibovu kuliko watangulizi wake - TRL, RICHMOND, DOWANS & BUZWAGI, kashiriki matumizi ya anasa mara elfu ya watangulizi wake, kazunguka dunia nzima kwa mwaka mmoja kisha kaanza tena kuizunguka weeeee mpaka leo bado anaizungukia, hali za maisha ya watanzania zinazidi kuwa mbaya chini ya utawala wake, ni rais legelege kuliko rais yoyote aliyewahi kuongoza nchi hii, na nadhani huenda akakamata nafasi ya kwanza ya rais legelege wa karne).
  Tukizidi kuilegezea CCM itazidi kuuza nchi na kututia utumwani. Tuandamane kuiondoa CCM na si Ngeleja wala malima, kwani wao wanatekeleza sera za CCM.
   
 18. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  nimekata shauri, SIJI, SITAKUJA WALA SITASHIRIKI, SITAKI KUWA SEHEMU YA SARAKASI ZA CCM kuwapofusha watz
   
 19. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu umezunguka sana. Hata ungekariri vifungu mia vya katiba unadhani hawa NGUNGURI watakuelewa???. Na isiitoshe unataka kumpa promo bure huyo Mama Shelukindo. Kinachotakiwa sio watu wa Dar peke yao waandamane..yaan kama ni kuhamasisha iwe nchi nzima manake btatizo la umeme ni la kitaifa. Unachofanya ni kutafuta 'CHEAP POPULARITY' mie siji bwana natumia kibatari
   
 20. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Nami naungana na watanganyika wenzangu kukataa hayo maandamano kama mpokeaji wake ni Bi Shelukindo. Hakuna chema chochote kutoka CCm. Ukitaka nami nije kwenye hayo maandamano, mgeni rasmi asitoke CCM ama chama chochote cha siasa, viongozi wa taasisi za kiraia ndio wayaongoze na kuhutubia wananchi, pili yasifanyike Mwembeyanga, kwa nini huko pembezoni mwa mji? ama yaishie Jangwani ama Mnzi mmoja, huku ndiko serikali iliko. Hao wana CCM wa design ya Shelukindo ni wale wale akina Sitta na Mwakyembe walioifuta agenda ya Richmond bungeni na kuwaacha watuhumiwa wakiendelea kudunda. Hapana! CCM hapana. Mwisho maandamano yawe ya kumtaka JK mwenyewe ajiuzulu na si Ngeleja wala Malima. JK ndiye tatizo kubwa nchi hii kwani ameleta serikali lege lege.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...