Taarifa kwa Umma kutoka CCM

TAARIFA KWA UMMA.

Dar Es Saalam.

Chama cha Mapinduzi kinachukua nafasi hii kuwapongeza wafanyakazi kwa tamko lao la kuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan juu ya nyongeza ya mshahara alilolitoa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Mkoani Dodoma 1 Mei 2022.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA amesema walikutana na Rais siku moja kabla ya sherehe za Mei Mosi na kukubaliana juu ya ajenda hiyo ambapo Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwahakikishia kuwa serikali itapiga mahesabu na nyongeza hiyo itapatikana katika mwaka mpya wa fedha unaoanza mwezi wa Julai 2022.

Katika taarifa yao TUCTA imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa hatua hiyo lakini pia imempongeza kwa kukubali wafanyakazi waliyofukuzwa kazi baada ya kukutwa na vyeti bandia walipwe stahiki zao, kitendo ambacho kimedhihirisha wazi namna Mhe Rais Samia Suluhu Hassan alivyokuwa muumini wa Haki, huruma na mapenzi mema kwa kila mtanzania.

Majibu haya ya TUCTA ni muafaka kwa wanasiasa wasio na maslahi na wafanyakazi wala nchi yetu ambao wanaumizwa na mazuri yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan nawao hupenda kubadili mazuri kuwa mabaya ili wajijengee umaarufu na ushawishi wa kisiasa kwa wananchi.

Katika kipindi cha miaka mitano (2020-2025) Chama Cha Mapinduzi kiliahidi kupitia ilani yake ya uchaguzi ibara ya 130 kuwa serikali itakazoziunda zitaendelea kuweka mazingira rafiki ya utendaji wa vyama vya wafanyakazi ili viendelee kuwa nguzo muhimu katika kujenga mahusiano mahala pa kazi na kuboresha masilahi na haki za wafanyakazi ikiwemo uboreshaji wa mishahara ya watumishi wa umma ili waweze kumudu gharama za Maisha kwa kuzingatia ukuaji wa uchumi wa Taifa na tija ya wafanyakazi. Hivyo anachokifanya Rais Samia Suluhu Hassan sio porojo au utashi wake bali ni utekelezaji wa ilani, Chama Cha Mapinduzi kinampongeza sana kwa umakini wake katika kuitekeleza ilani kwa vitendo.

Watanzania ni watu makini sana wanajua, wanafahamu na wanaona jitihada za serikali ya Chama Cha Mapinduzi awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan jinsi anavyoingiza furaha katika mioyo yao.

Ni ajabu kwa baadhi ya wanasiasa “Kupayuka” bila kufanya utafiti. Tunawahakikishia kuwa CCM itaendelea na jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wakiongozwa na Jemedari shupavu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan, kazi anayoifanya na timu yake imewafilisi ajenda za kisiasa wanasiasa wa upande pili na sasa wana ng’ang’ania ajenda ya Katiba Mpya.

Tumuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika mfumo wake wa uongozi kuliongoza Taifa letu kwa Maridhiano, Kuvumiliana, Mabadiliko na Kulijenga upya Taifa

Shaka Hamdu Shaka
Katibu Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi na Uenezi
02 Mei 2022

View attachment 2208844

View attachment 2208845
Da mimi nilijua mjambiani kafa nianze kushangilia
 
Kwisha habari yenu…2025 kifo cha mende…kwa kizungu cockroach…miguu juu
 
Back
Top Bottom