Taarifa kwa Umma kuhusu maombi ya Udahili wa Machi 2020 ngazi ya Astashahada na Stashahada

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,401
73,998
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI YA UDAHILI WA MACHI 2020 (MARCH INTAKE) KWA WAOMBAJI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129 ili kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi katika Vyuo ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini. Jukumu mojawapo la Baraza ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vya Ufundi nchini yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
=
Baraza linapenda kuufahamisha umma kuwa udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote isipokuwa Ualimu umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 15 Januari, 2020 na utakuwa wazi hadi tarehe 20 Februari, 2020. Hata hivyo, udahili wa Machi, 2020 (March Intake) hautahusisha programu za Afya kwenye vyuo vya Serikali.

Maombi ya kozi/ programu mbalimbali yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika. Aidha Vyuo vitapokea maombi ya udahili na kufanya Uchaguzi kwa wanafunzi wenye sifa na kisha kuwasilisha NACTE majina ya waliochaguliwa kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuyatangaza. Vile vile Vyuo vinaelekezwa kuzingatia taratibu za udahili kama zilivyotolewa na Baraza katika mwaka wa masomo 2019/2020.

Baraza linawashauri Wahitimu wa Elimu ya Sekondari na Vyuo kwa ujumla kuhakikisha kuwa wanatuma maombi kwenye Vyuo vinavyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2019/2020 (Admission Guidebook for 2019/2020 Academic Year). Mwongozo wa Udahili unapatikana katika tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz).

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 15/01/2020
 
Back
Top Bottom