TAARIFA KWA SERIKALI: Bugando HospitaL total tools down kuanzia sasa..

TAARIFA KWA SERIKALI: Bugando HospitaL total tools down kuanzia sasa..

Na hospitali ya Jeshi Lugalo mgomo unanukia....
sababu- zaidi ya nusu ya madokta wao (15) wamepelekwa Muhimbili wanalipwa laki 100,000/= kwa siku hali wao hawapumui na kazi zilizo walemea.

when you solve one problem blindly you creat seval problems!!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MGOGORO WA SERIKALI NA MADAKTARI (MGOMO WA MADAKTARI
Tarehe 21 Januari 2012, madaktari wanafunzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) walitangaza rasmi kuwa wangeanza mgomo baada ya siku tatu (24/01/2012) usio na kikomo hadi pale serikali itaposikiliza na kutekeleza madai kadhaa ya madaktari juu ya hali ya utoaji huduma za afya mahospitalini, hawawataki viongozi wa Wizara ya Afya,maslahi ya madaktari na ugumu wa maisha. Hata hivyo serikali haikuchukua hatua zozote zilizokidhi mahitaji ya madaktari hao na badala yake ikaonekana kana kwamba hakuna maelewano kati ya madaktari na Serikali kilichopelekea madaktari hawa kugoma rasmi kwa kuendeleza mkutano wao Hoteli ya StarLight. Baada ya malumbano ya takribani siku saba, Waziri mkuu aliingilia kati suala hili baada ya madaktari kukataa kuongea na Wizara ya afya. Majibu ya waziri mkuu ndio yaliyokuza hasira na chuki kwa jamii na madaktari. Kwa mfano Waziri Mkuu aliwashurutisha Madaktari warudi kazini ama sivyo watafukuzwa kazi na kuwa Madai ya maslahi ya madaktari ni makubwa mno serikali haiwezi kumudu kuyalipa. Aliahidi kuwa atapeleka madaktari kutoka Jeshini na JKT kama madaktari hawa hawatarudi kazini.
Kufuatia hili wanaharakati wakiongozwa na Kituo cha Sheria na haki za Binadamu na shirika la Sikika tuliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na kusisitiza umuhimu wa kufikia suluhu katika jambo hili. Pia Kituo na Sikika kiliitwa kwenye kamati ya Bunge ya huduma za jamii ili kuweza kutoa maoni yao. Tulichoweza kuieleza kamati ni kuwa kuna haja ya kuwa na Msuluhishi atakaye suluhisha mgogoro huu wa madaktari na Serikali. Pia tulichukuwa hatua ya juu ya kujaribu kuwatafuta wasuluhishi kutoka TEC, BAKWATA,CCT, na APHF ili kutatua suala hili. Cha kushangaza ni pale Serikali ilipokataa kushiriki kwa kusema kuwa iko tume iliyoundwa na Serikali kutatua mgogoro huo. Tarehe 6 Februari tumeshuhudia madaktari Bingwa nao wakiunga mkono mgomo huu hali iliyopelekea huduma kusimama kabisa na kurudisha wagonjwa majumbani.
AIDHA, kwa siku na hatua tofauti zilizofuata imejidhihirisha kuwa serikali na madaktari wameshindwa kupata muafaka. Hii inakuja huku pia juhudi za Bunge kujishirikisha kutatua tatizo hili zikionekana kutokuwa na lengo. Ikumbukwe kuwa:-
1. Ibara ya 14 ya Katiba inatoa haki ya kuishi kwa binadamu, hii ikizingatiwa kuwa kusitishwa kwa huduma zinazohitajika za afya kunaongeza/kunaweka watanzania mazingira ya kuipoteza haki hii,
2. Ibara ya 11 (1) ya Katiba inatoa Haki ya matibabu (pamoja na haki zingine) kwa raia huku ikiweka jukumu hilo mikononi mwa serikali;
3. Ibara ya 6(1) ya Mkataba wa Haki za Kiraia na Kisiasa (1966) ambao Tanzania iliridhia tangu 1976 inatoa haki asilia ya kuishi kwa kila binadamu na kuwa haki hii inapaswa kulindwa kasheria na hakuna atakayenyang’anywa haki hii kwa sababu yeyote.Ni jukumu kwa kila nchi mwanachama wa mkataba huu kuwa na jukumu la kulinda Haki ya Kuishi ya raia wake;
4. Ibara ya 12 ya Mkataba wa Haki za Kiraia za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni unazitaka nchi wanachama kutambua na kutekeleza Haki za kila binadamu kupata huduma bora zaidi za kiafya, kimwili na kiakili. Ikizingatiwa Ibara ndogo ya 12 (2) (d), ambayo inazitaka nchi kutengeneza mazingira kwa watoa huduma bora za afya wakati wa ugonjwa;
5. Ibara ya 91(1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inatoa jukumu kwa serikali kutumia rasilimali za nchi kutekeleza haki na matakwa ya jamii/raia;
Hii ikizingatiwa kuwa madai ya madaktari ni juu ya hali mbaya ya kutoa huduma mahospitalini na maslahi duni wanayopatiwa kwa kutekeleza wajibu wao. Tunazingatia pia kuwa migogoro ya maslahi na hali duni ya kutoa huduma za afya imekuwepo tangu miaka ya 1991 na kwamba utatuzi wa matatizo yaliyoainishwa haujafanyika; hapa kuna mifano ya kutoongezeka posho za kufanya kazi za ziada kwa madaktari ya Shs 10,000/= tangu mwaka 2002; mishahara duni na ambayo haiendani na hali halisi ya maisha kwa sasa huku maslahi ya kada zingine za umma na viongozi wa kisiasa zikiongezeka, huku;-
1. Ibara ya 23 (1) ya Katiba ikitoa haki kwa kila anayeajiriwa kupata mshara na maslahi ya haki toka kwa mwajiri.
Tumeona pia kuwa serikali imekuwa ikishughulikia suala hili bila kujali maslahi ya raia na Katiba, haswa pale Waziri Mkuu alipoamua kuwalazimisha madaktari kurudi kazini kinyume cha Ibara ya 25 (2) ya Katiba ianayopiga marufuku kazi za shuruti nchini.
Izingatiwe kuwa sehemu ya Katiba inayotoa Haki hizi (Sehemu ya Pili ya Misingi ya Katiba) inapiga marufuku mahakama kujihusisha na jukumu la kuamua juu ya haki hizi (ibara ya 7 (2) na hivyo kurudisha jukumu la kutetea haki hizi mikononi mwa wananchi wenyewe.
AIDHA Ibara ya 8 ya Katiba inatamka wazi kuwa Serikali itapata mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi. HIVYO BASI:
• KWA KUWA mgogoro huu umevunja haki kadhaa pamoja na haki ya kuishi kwa wananchi kadhaa na kuwa unahatarisha haki za raia wengine zaidi;
• KWA KUWA Serikali imeshindwa kutumia haki na mamlaka tuliyoipa kutekeleza wajibu wake;
• KWA KUWA Serikali imeshindwa hata kutumia rasilimali tulizoikabidhi kuatua tatizo hili linalohitaji utatuzi wa haraka;
• KWA KUWA Katiba inatoa jukumu la moja kwa moja kwa wananchi kuchukua hatua za kuiwajibisha serikali kutekeleza wajibu wake,
• Na KWA KUWA Ibara ya 26 ya Katiba inamtaka kila raia wa nchi hii kuilinda Katiba na sheria zingine za Nchi;
HIVYO BASI:
Kesho saa nne asubuhi tunakutana mnazi mmoja kuishinikiza serikali kutatua hili na au kujiuzuru kwa kushindwa kwake.
 
nami nawakilisha kama TONNY ALMEIDA BUGANDO TOOLS DOWN TOTALLY. tonny CTU unatuambiaje sasa?

CTU Parameter is secured.. TOTAL TOOLS DOWN..@SASA SERIKALI INAPASWA KUWAJIBIKA. ETI KUNA TAARIFA ULINZI UMEONGEZWA BMC SA SIJUI WANAMLINDA NANI.
 
oyaa ctu inatoa taarifa ma specialist hoi kwa call bugando. haa watakoma, washazoea kulala usiku. hee watagoma tuu hawawezi kazi
 
sijapata picha halisi ya nini kinaendelea hadi sasa.inawezekanaje binadamu aitwaye daktari anamuacha binadamu mwenzake aitwaye mgonjwa anafariki kwa sababu ya kukosa posho?

Mbona mnataka kuhamisha hoja kwa kuleta propaganda kuwa madai ya madaktari ni posho pekee? MBONA HILI LA KUOMBA MAZINGIRA BORA KWA WAGONJWA VIKIWEMO VITANDA KWA WANAOLALA CHINI NA VIFAA TIBA HAMLIFANYI KUWA HOJA YA MSINGI?

KIFUPI SERIKALI IMESHINDWA KUZUIA HUU MGOMO NA NJIA PEKEE YA SULUHISHO ILOBAKI NI KUTIMIZA MATAKWA YA MADAKTARI...
 
Mimi naona wana JF tuingie mtaani wenyewe labda wa tz watazinduka,maana kama ni nondo za uhamasishaji tukiwa kwenye keyboards tumezishusha mno lakini watz hawaelewi ndo kabisaaaa wengine wanaishia kusombwa na mafuso kwenda kula ubwabwa na wanaishia kutelekezwa.
 
oyaa ctu inatoa taarifa ma specialist hoi kwa call bugando. haa watakoma, washazoea kulala usiku. hee watagoma tuu hawawezi kazi

Nasikia hou ndo ul!kuwa miongoni mwa mikakati ya hawa madaktari ya kuwafanya hao madaktari bingwa wagome kwa sababu hawawezi kufanya kazi wenyewe.
 
Nani asiyejua kuwa sisiemu na serikali yake huneemeka kwa kafara za wananchi kufa kwa lukuki yao; tangu enzi za mkapa na sasa kikwete!!!!!!!!!!
Ukimya wa rais wa nchi kiasi hiki wakati nchi imeingia katika kipindi hiki cha kushangaza si jambo la kawaida! Mimi nadhani pindi kipimo cha kafara kitakapotimia mtaona mkuu anakuja na ufumbuzi wa kisanii kama kawaida yake tangu 2005 hadi leo hii!!!!!!!!!!!!!
Hii nchi ni ya ajabu. Ka5iba kisanii, posho ya wabunge kisanii, na sasa mgomo pia kisanii; uchaguzi wa 2010 kisanii; kila kitu kisanii!!!!!!!!!!! huo ndiyo mwendo waTz twende tu tutafika tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Aisee, nchi ina washirikina hii, no wonder we are developing backward.
 
Hebu niulize kitu, ndo kusema kwamba hali itaendelea namna hii na sisi kazi yetu kupost tu humu Jf?? Cant we take a next step??
 
Back
Top Bottom