TAARIFA KWA SERIKALI: Bugando HospitaL total tools down kuanzia sasa..

bungando sio ya kanisa? hivi wanakuwa wauji kiasi hichi? Bora tu huu makataba wa MOU uvunjwe

Bugando, kama ilivyo KCMC na Peramiho Hospital...ni za kanisa, lakini zinaendeshwa kwa MoU kati ya kanisa na Serikali. Hivyo katika hospitali hizo kuna maDaktari wenye mkataba na kanisa (yaani wameajiriwa na kanisa) ambao ni wachache, na wenye mkataba na serikali (yaani wameajiriwa hapo na serikali) ambao ni wengi. Kanisa linaweza kuwabana waajiriwa wao, lakini serikali je?!
 
poleni sana WATANZANIA WENZANGU, lakini hakuna namna , lazima tupitie mambo magumu kuelekea ukombozi kamili

404284_342205012469229_100000391994771_1103093_1884948629_n.jpg

thanks mkuu, umezipanga zikapangika.
maisha ya kila siku bila JF ni kazi bure.
 
Kauli ya Mkuu wa Nchi na Serikali. Anayo kauli mkuu kweli akose kauli.

Hivi kweli Bugando si ni hospitali ya Kanisa imekuwaje na wao wanagoma tena?

Unajua mkataba wa interns doctors huwa ni baina yao na nani?uliza kabla ya kuropoka!
 
Inasikitisha sana, hata mimi nilitegemea kuwa hospitali za kidini ndiyo zitakuwa kimbilio kwa watanzania lakini nako sasa mambo ni hovyo! Madaktari ambao kabla ya kazi mnafanya sala, iweje mnashindwa kumuogopa Mungu na nyie mnageuka kuwa wauaji?
Usichanganye mambo ya dini kwenye migomo,kumbuka hata hizo za kidini zitazidiwa ikiwa za serikali ziko kwenye mgomo cha muhimu ni serikali kuwalipa madr kutimiziwa haja zao siasa kuwekwa kando kwenye mambo ya kitaalam.
 
Wabongo bwana!
Tumeisha toka kwenye topic, sasa tunang'ang'aniana kwa vitu vya kipumbaf kabisa.

Hebu, mtoa mada atupe updates za Bugando, au kama kuna mmoja wetu yupo maeneo hayo atujuze kinachoendelea.
Na ikiwezekana atupatie picha za hayo matangazo. Nimeishachoka na porojo nani anamiliki hosp. gani. Bull shit @#$%#$^^%$&@!
 
bugando ni hospitali ya kanisa! Inatuhusu nini sisi? Chukueni michango ya waumini muwalipe madaktari mmezoea kuchukua pesa za serikali kushughulikia kanisa. Soon mtarealize kuwa mwisho wenu waja,
everything will come to an end. Imeanza kwa russia na china veto yao dhidi ya wauaji wa magharibi, sasa itakuja hapa bongo mtafute pa kwenda
attachment.php
 
Bugando na KCMC ni hospitali za kanisa naomba maelezo wanaingiaje kwenye mgomo huu sambamba na Muhimbili na hospiali zingine za umma? Napata shida kupata tafsiri yake.



akili za kipipi jojo ni mbaya sana hivi unaelewa sababu za mgomo? hivi unajua madaktari wote wa bugando, interns na wauguzi wanalipwa na nani?

na wengine wote wenye mirengo kama yako muanze kwa kuanagalia kila huduma yenye kutolewa na makanisa mkatae na muende huko kwenye umma.
 
kwa Ishu ya madaktali Ilipofikia kweli serikali hii Imezidi ULEGELEGE? sakata hili lilivyoanza kulikuwa hakuhitajiki ubabe wa kauli za mh Pinda....hivi kulikuwa na ugumu gani waziri mkuu kusema' madaktali sisi kama serikali kilio chenu tumekisikia pls ludini kazini sisi tunashughulikia madai yenu ya maslahi lkn hili laviongozi wawizara nimewashauli wajiuzulu haraka pia mh Rais akiludi toka safali nitamshauli afanye mabadiliko makubwa ndani ya wizara hii" au wameshindwa kuchukua hatua kwasababu wao wanaenda India?
 
kwa taarifa ya kuaminika kutoka vyanzo vya habari mgomo wa madktari umepata sura mpya na unaonekana kuwa na kasi mpya kama ya rais wetu jk...............................jana ilikuwa muhimbili leo Bugando sijui huko kwingine kwa hali ya kawaida nimezoea kuona wagonjwa wanatoka nyumbani wanapelekwa hospitali lakin sasa ni kinyume kwa mara ya kwanza leo nimeona wagonjwa wanatoka hospitali wanarud nyumbani......................jaman jk tunaomba tamko malizaneni na hao madaktari
 

Attachments

  • Photo-0033.jpg
    Photo-0033.jpg
    79.5 KB · Views: 3,044
Inabidi sasa pinda achukue madaktari wengine toka magereza,..
wengine toka FFU,....
wengine toka zimamoto,...
wengine toka mgambo,...
na kwingne alikodai atapata sijui CUBA,.....

Hao wa jeshini wenyewe kupima malaria kwa vyombo vya kisasa walikuwa wanababaika
 
Back
Top Bottom