TAARIFA KWA SERIKALI: Bugando HospitaL total tools down kuanzia sasa..

Kanisa ndio linatibu?
serikali imeingia mkataba na hospitali za dini katika kutoa huduma za kiafya {public private partnership} katika muungano huo serikali inatoa ruzuku,kusupply madawa pamoja na kuajiri madaktari.kwa hiyo madaktari walioko kcmc pamoja na bugando ni waajiriwa wa wizara ya afya na wanafanya kazi chini ya muongozo wa wizara kwa hiyo na wao ni victims wa madhira yanayowapata madaktari wengine ndo maana nao wako katika mgomo.kwa hiyo hapa swala si kanisa
 
Kumbe migomo ni bora kuliko maandamano!! Polisi na mabomu yao ya machozi hawana kazi!!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MGOGORO WA SERIKALI NA MADAKTARI (MGOMO WA MADAKTARI
Tarehe 21 Januari 2012, madaktari wanafunzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) walitangaza rasmi kuwa wangeanza mgomo baada ya siku tatu (24/01/2012) usio na kikomo hadi pale serikali itaposikiliza na kutekeleza madai kadhaa ya madaktari juu ya hali ya utoaji huduma za afya mahospitalini, hawawataki viongozi wa Wizara ya Afya,maslahi ya madaktari na ugumu wa maisha. Hata hivyo serikali haikuchukua hatua zozote zilizokidhi mahitaji ya madaktari hao na badala yake ikaonekana kana kwamba hakuna maelewano kati ya madaktari na Serikali kilichopelekea madaktari hawa kugoma rasmi kwa kuendeleza mkutano wao Hoteli ya StarLight. Baada ya malumbano ya takribani siku saba, Waziri mkuu aliingilia kati suala hili baada ya madaktari kukataa kuongea na Wizara ya afya. Majibu ya waziri mkuu ndio yaliyokuza hasira na chuki kwa jamii na madaktari. Kwa mfano Waziri Mkuu aliwashurutisha Madaktari warudi kazini ama sivyo watafukuzwa kazi na kuwa Madai ya maslahi ya madaktari ni makubwa mno serikali haiwezi kumudu kuyalipa. Aliahidi kuwa atapeleka madaktari kutoka Jeshini na JKT kama madaktari hawa hawatarudi kazini.
Kufuatia hili wanaharakati wakiongozwa na Kituo cha Sheria na haki za Binadamu na shirika la Sikika tuliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na kusisitiza umuhimu wa kufikia suluhu katika jambo hili. Pia Kituo na Sikika kiliitwa kwenye kamati ya Bunge ya huduma za jamii ili kuweza kutoa maoni yao. Tulichoweza kuieleza kamati ni kuwa kuna haja ya kuwa na Msuluhishi atakaye suluhisha mgogoro huu wa madaktari na Serikali. Pia tulichukuwa hatua ya juu ya kujaribu kuwatafuta wasuluhishi kutoka TEC, BAKWATA,CCT, na APHF ili kutatua suala hili. Cha kushangaza ni pale Serikali ilipokataa kushiriki kwa kusema kuwa iko tume iliyoundwa na Serikali kutatua mgogoro huo. Tarehe 6 Februari tumeshuhudia madaktari Bingwa nao wakiunga mkono mgomo huu hali iliyopelekea huduma kusimama kabisa na kurudisha wagonjwa majumbani.
AIDHA, kwa siku na hatua tofauti zilizofuata imejidhihirisha kuwa serikali na madaktari wameshindwa kupata muafaka. Hii inakuja huku pia juhudi za Bunge kujishirikisha kutatua tatizo hili zikionekana kutokuwa na lengo. Ikumbukwe kuwa:-
1. Ibara ya 14 ya Katiba inatoa haki ya kuishi kwa binadamu, hii ikizingatiwa kuwa kusitishwa kwa huduma zinazohitajika za afya kunaongeza/kunaweka watanzania mazingira ya kuipoteza haki hii,
2. Ibara ya 11 (1) ya Katiba inatoa Haki ya matibabu (pamoja na haki zingine) kwa raia huku ikiweka jukumu hilo mikononi mwa serikali;
3. Ibara ya 6(1) ya Mkataba wa Haki za Kiraia na Kisiasa (1966) ambao Tanzania iliridhia tangu 1976 inatoa haki asilia ya kuishi kwa kila binadamu na kuwa haki hii inapaswa kulindwa kasheria na hakuna atakayenyang’anywa haki hii kwa sababu yeyote.Ni jukumu kwa kila nchi mwanachama wa mkataba huu kuwa na jukumu la kulinda Haki ya Kuishi ya raia wake;
4. Ibara ya 12 ya Mkataba wa Haki za Kiraia za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni unazitaka nchi wanachama kutambua na kutekeleza Haki za kila binadamu kupata huduma bora zaidi za kiafya, kimwili na kiakili. Ikizingatiwa Ibara ndogo ya 12 (2) (d), ambayo inazitaka nchi kutengeneza mazingira kwa watoa huduma bora za afya wakati wa ugonjwa;
5. Ibara ya 91(1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inatoa jukumu kwa serikali kutumia rasilimali za nchi kutekeleza haki na matakwa ya jamii/raia;
Hii ikizingatiwa kuwa madai ya madaktari ni juu ya hali mbaya ya kutoa huduma mahospitalini na maslahi duni wanayopatiwa kwa kutekeleza wajibu wao. Tunazingatia pia kuwa migogoro ya maslahi na hali duni ya kutoa huduma za afya imekuwepo tangu miaka ya 1991 na kwamba utatuzi wa matatizo yaliyoainishwa haujafanyika; hapa kuna mifano ya kutoongezeka posho za kufanya kazi za ziada kwa madaktari ya Shs 10,000/= tangu mwaka 2002; mishahara duni na ambayo haiendani na hali halisi ya maisha kwa sasa huku maslahi ya kada zingine za umma na viongozi wa kisiasa zikiongezeka, huku;-
1. Ibara ya 23 (1) ya Katiba ikitoa haki kwa kila anayeajiriwa kupata mshara na maslahi ya haki toka kwa mwajiri.
Tumeona pia kuwa serikali imekuwa ikishughulikia suala hili bila kujali maslahi ya raia na Katiba, haswa pale Waziri Mkuu alipoamua kuwalazimisha madaktari kurudi kazini kinyume cha Ibara ya 25 (2) ya Katiba ianayopiga marufuku kazi za shuruti nchini.
Izingatiwe kuwa sehemu ya Katiba inayotoa Haki hizi (Sehemu ya Pili ya Misingi ya Katiba) inapiga marufuku mahakama kujihusisha na jukumu la kuamua juu ya haki hizi (ibara ya 7 (2) na hivyo kurudisha jukumu la kutetea haki hizi mikononi mwa wananchi wenyewe.
AIDHA Ibara ya 8 ya Katiba inatamka wazi kuwa Serikali itapata mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi. HIVYO BASI:
• KWA KUWA mgogoro huu umevunja haki kadhaa pamoja na haki ya kuishi kwa wananchi kadhaa na kuwa unahatarisha haki za raia wengine zaidi;
• KWA KUWA Serikali imeshindwa kutumia haki na mamlaka tuliyoipa kutekeleza wajibu wake;
• KWA KUWA Serikali imeshindwa hata kutumia rasilimali tulizoikabidhi kuatua tatizo hili linalohitaji utatuzi wa haraka;
• KWA KUWA Katiba inatoa jukumu la moja kwa moja kwa wananchi kuchukua hatua za kuiwajibisha serikali kutekeleza wajibu wake,
• Na KWA KUWA Ibara ya 26 ya Katiba inamtaka kila raia wa nchi hii kuilinda Katiba na sheria zingine za Nchi;
HIVYO BASI:
Kesho saa nne asubuhi tunakutana mnazi mmoja kuishinikiza serikali kutatua hili na au kujiuzuru kwa kushindwa kwake.

Mkuu hawa walotoa hii ni taasisi gani?
 
kitakachofuatia ni kwa wananchi wote nchi nzima kugoma tuone nani atasalimika wake za madaktari wawagomee,watoto wao wawagomee na watoa huduma nyingine zoote nao wagome eeeh tuone sasa nani atakuwa kwenye safe side!!
 
Kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa kikao cha Madaktari wakazi (Resident) na Interns ambao bado walikuwa wanaona wagonjwa wa dharura sasa wameamua kuacha kila kitu na kuamua kutoa mtangazo.

Kkatika mbao za matangazo kuwa leo hakuna kazi huku kukiwapo na taarifa Madaktari bingwa wa hospitali hii wamekuwa wakionekana katika makorido ya hospitali hiyo wakijadili mgomo na kuwepo kwa tetesi kuwa walikuwa na mpango wa kukaa kikao cha kujadili mgomo na kuweka tool down..


NAOMBA KUWASILISHA


attachment.php

Asante kwa justification mkuu. Big up.
 
nakumbuka prof. Sarungi alipick tools kipindi cha ajali moja hivi!
Dr. David Mwakyusa halikadhalika huwa anapick-up tools katika majanga, why not how Dr. JMK.....!


uyo kilaza ataweza wapi wakati walipeana na mshikaji wake kwenye viwanja vya muhimbili?
 
nakumbuka prof. Sarungi alipick tools kipindi cha ajali moja hivi!
Dr. David Mwakyusa halikadhalika huwa anapick-up tools katika majanga, why not how Dr. JMK.....!

prof. sarungi ni orthpedic surgeon(daktari wa mifupa). aliingia mjengoni wakati wa ajali treni
 
Ee Mungu mjalie babu wa Loliondo dawa mpya ili twende kwa babu kupata matibabu.
 
Mgomo wa madaktari haushangazi ni hatua iliyochelewa sana. Mimi wakati namaliza chuo kikuu mwaka 1970, Baada tu ya kufuzu chuo kikuu Maaktari alikuwa na mshara mkubwa kuliko wote, wakifuatiwa na Wahandisi na halafu Wanasheria. Leo mambo ni kinyume maana wenye ushawishi mkubwa wa kupanga maslahi ya wafanyakazi ni watu wa 'human resources', wanasheria na wanasiasa na si ajabu wametumia nafasi hii kuweka mambo upside down kwa kuweka maslahi yao kwanza. Muda wote huu wataalamu madaktari na wahandisi wao wako katika 'field' na serikali imechukua uvumilivu wa kitanzania kuacha mambo yaendelee licha ya malalamiko yao ya mara kwa mara na kwa kweli tumefika mahala watu kupata haki sharti kwanza wagome ndipo wasikilizwe - fire brigate kind of affair.
 
hali kwa sasa ni ngumu sana kiuchumi na nasikia walimu wako njiani kugoma
 
Tanzania ina kila kitu,.....
Ila haina watanzania tu.

Ndo maana kila mtu ananoa kisu akate nyama aende kwao.

uko sahihi mwanajamii............
wangekuwepo hao kwenye red, nchi isingekuwa hivi hii...............
 
Inabidi sasa pinda achukue madaktari wengine toka magereza,..
wengine toka FFU,....
wengine toka zimamoto,...
wengine toka mgambo,...
na kwingne alikodai atapata sijui CUBA,.....

Upuuzi kweli kujidai wewe ndio wewe na bila wewe hakuna kinacho wezekana.
Nawapongeza sana madaktari ingawa binafsi ni mhanga wa mgomo wenu lakini
potelea mbali.

Pinda show us what you've got now.
Wataalam wako wa JWTZ na JKT vipi wameweza?

Mkuu yaani umechukia, umeteseka, umehangaika, imekukera, imekuudhi mpaka umesahau kutaja madaktari toka jeshi la mgambo!
 
hivi inakuaje star T.V inareport mambo ya muhimbili halafu mambo ya Bugando hayasemwi?mmehongwa nini?
 
Back
Top Bottom