kepler telescope
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 904
- 599
Hawa waliowafungia waganga wa jadi wanajiamini sana, labda wanae Mungu wa kweli. Jamaa wakicharuka na minguvu yao ya giza si wataisha? Haya.
Kivipi- elezeaUkisoma maelezo yote mwanzo mwisho utagundua kuwa kulikuwa na target ya mtu mmoja aliekuwa anatafutwa wengine wameingizwa kama mkumbo tu
Kivipi- elezea
Tusisahau hata wanaoenda India na kwingineko baadhi wanarudi wakiwa wamerest in peace!afadhali wafungiwe tu, afya ya mtu si ya kuichezea...
wanawake wenzangu kuliko kumwaga mihela kwa hawa matabibu ni bora uende kufanyiwa vipimo vya kisayansi ujue tatizo lako.
Mbona yule mwenye dawa alfulela ulela za kutibu kila ugonjwa duniani na kuwa na maduka ya dawa zake nchi nzima na matangazo lukuki; lakini mwenyewe alishindwa kujisaidia na akaanguka hadharani siku ya harusi yake hayumo? Hii siyo "double standard"?Ngoja waje hapa wenyewe
unataka kusema hadi tuone madhara ndio tuchukue hatua?Ulimbukeni wa kuamini zaidi matibabu ya dawa za kizungu ndio yanayo tutesa, hakuna alie lalamika kwa kupata madhara kwa nini watu wafungiwe? uko mahospital watu wanakufa hovyo kwa kukosa matibabu sahihi lakini inaitwa bahati mbaya, kweli ukoloni haujaondoka kwenye fikra za mtu mweusi.
Jina sio dini acha ujingaNgoja waje hapa wenyewe
We mburula Fadhil ni mkristo ,Toa ujinga na ushamba wako wa udiniNgoja waje hapa wenyewe
Mkuu sio kuwakatisha tamaa tatizo watu wengi waliopo kwenye hii tasnia wamekuwa matapeli. Hilo ni jambo baya. Pia unapo kuwa umetengeneza hiyo tiba asilia peleka kwenye wizara ili kuihakiki ndipo upewe go ahead ya kuisambaza na kuitangaza hiyo tibaMimi nimesoma kidogo na naishi maisha ambayo huwezi kuyaita duni (japo sio bora), nikiugua magonjwa yasiyoeleweka kama kuhisi malaria option yangu ya kwanza huwa ni herbs (mitishamba) na huwa zinanisaidia sana. Sana sana hospitali nakwenda kupima tu na pale daktari anapoona malaria ndio naweza kutumia vidonge huku vikenda simultaneously na mitishamba.
Sio busara kuwakatisha tamaa walioamua kuventure katika mitishamba maana hata makampuni makubwa kama Colgate yanahamia kwenye herbal na hata Glaxo wana dawa nyingi sasa za herbal.
Nakubaliana nawe mkuu lakini hapa tatizo ni elimu! Elimu tunayohitaji haitolewi na Dr. Mwaka bali inapaswa kutolewa na serikali na kwa vile haikuitoa hivyo kututumbukiza kwenye lindi hili la ujinga, sidhani kama kumzuia huyu Mwaka itasaidia bali msaada ilikuwa ni kumguide ili kuwapunguza hawa wahanga wa ujinga wetu!Mkuu sio kuwakatisha tamaa tatizo watu wengi waliopo kwenye hii tasnia wamekuwa matapeli. Hilo ni jambo baya. Pia unapo kuwa umetengeneza hiyo tiba asilia peleka kwenye wizara ili kuihakiki ndipo upewe go ahead ya kuisambaza na kuitangaza hiyo tiba