Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA)

ivi taarifa au tathmni ya utendaji wa mbunge inafanywa na yeye mwenyewe tena kwa kupenda/hiari, #ChangeTanzania.

Mkuu,
Kwa mujibu wa katiba na sheria zetu hakuna mtu anayetathmini kazi ya mbunge ndio maana watu wengi wanakimbilia huko. Ukiona mtu analeta tathmini ya kazi yake ujue anajiamini sana. Kama huna cha kutathmini una ingia mtini miaka 5 na hakuna wa kukuuliza. Kisha unaibuka na Rushwa ya kuhonga wapiga kura ndani ya chama na nje, then unarudi bungeni au unakwama. life goes on.
Hiki kizazi cha kina mnyika ndio kinataka kufungua ukurasa mpya. Ina maanisha kuwa tuna kitu cha kuandika kwenye katiba mpya kuhusu utaratibu wa kutathmini wabunge na ukomo wao.
Pili, si lazima mbunge akae miaka 5 kama ameshindwa. La kwa sasa no way, ndo hivyo.

 
mh mbunge wangu mnyika mm ni mkazi wa kibangu mbona sisi barabara yetu mbovu???? sijawahi kukuona hata ukija ubungo kibangu kila siku naskia ww na kimara, kimara na wewe!! hiyo namba ya cm kila cku imezimwa! na ikiwa wazi haipokelewi sasa nikueleweje, yaani sasa mpaka kanisa limeamua kujenga au niseme kukarabati barabara no mbunge no diwani, kwa anayekaa kibangu barabara iendayo jeshini atasema kama mm nadanganya! jitahdi baba, watu wamechoka na magamba sasa wasije pata hasira jtahd sana kuja na kibangu walau tushee mawazo tufanyeje! maji ni kero kubwa hata sijui nianzie wapi, kila siku kwangu maji natumia elf 5!!!!
nawakilisha!

Nimepita hii njia kuelekea makoka, kila maji yanapotoka (kwa mgao) utadhani mvua imenyesha maji yanavyotiririka barabarani. Hivi kama wananchi tunachukua hatua gani kuhakikisha tunalinda na kutunza miundo mbinu yetu?
Inakua ajabu kama wengine wanakosa maji wakati maji yanaishia ardhini kutokana na mabomba kukatika na hatua za haraka kutochukuliwa, itakuwa vizuri tukijiwekea utaratibu wa kuchukua hatua kutatua tatizo kuliko kutegemea mbunge atufanyie kila kitu
 
Nimepita hii njia kuelekea makoka, kila maji yanapotoka (kwa mgao) utadhani mvua imenyesha maji yanavyotiririka barabarani. Hivi kama wananchi tunachukua hatua gani kuhakikisha tunalinda na kutunza miundo mbinu yetu?
Inakua ajabu kama wengine wanakosa maji wakati maji yanaishia ardhini kutokana na mabomba kukatika na hatua za haraka kutochukuliwa, itakuwa vizuri tukijiwekea utaratibu wa kuchukua hatua kutatua tatizo kuliko kutegemea mbunge atufanyie kila kitu

Ndugu, hizo ndizo akili za watanzania. Yaani they like shifting burdens! Just because there is Mnyika basi wao wanakaa na kurelax. Nadhani kuna sehemu hapo mwanzo tulikosea. Dhana ya uwajibikaji haikutiliwa mkazo katika taifa. Hatimae sasa tuna kizazi kisichopenda kazi
 
Narubongo nimesoma yooote lakini ni yaleyale ya kila siku. Barabara ya Korogwe-Kilungule-external iko taaabani! Barabara ya baruti-kilungule iko taabani, barabara ya kiwanjani-kibanda cha mkaa-kibangu iko hoi, barabara ya Kimara mwisho - vyumba vinane -kwa beka iko hoi, barabara ya makoka kwa mama mzaire-kwa kichwa ipo oama haipo!Barabara ya maramba mawili kuelekea Kinyerezi hoi, mitaa ya Ubungo national housing iko taabani maji taka yanatiririka kila mahala. Maji safi hakuna.

Ndugu Mnyika ungana na Madiwani wako mhamasishe maendeleo. Hivi grader la manispaa liko wapi siku hizi. Wewe ni mbunge una sauti kwenye council omba grader hamasisha wananchi wachangie mafuta wape grader lichonge barabara za kimara zipitike utakuwa umeua tembo kwa ubua. Wewe ng'ang'ania tu blog uone mwisho wake manake watu hawaangalii blog wala JF watu wanataka maeneo yapitike. Kwa sababu ya barabara mbovu wananchi wa jimbo lako wanaamka saa kumi usiku kwenda kujikusanya morogoro road ili wapate usafiri.

mkuu Kimbunga pole sana kwa matatizo, hii baraabara ya Korogwe-Kilungule-external ilisababisha gari yangu kukata spring kati ya April/May. Mvua ikishanyesha ndio hapatamaniki kwa tope na mashimo,sasa kuna siku mvua ilinyesha masaa matatu tu! ilibidi tuwalipe vijana 3000/= kwa kila gari ili kutuongoza tusipotee njia.. maana barabara yote ilikuwa imefunikwa na maji na na tope zito
 
Last edited by a moderator:
Bahati nzuri hayo maeneo yote nayajua wewe unataka niongelee eneo moja tu.

Tusiangalie maendeleo ya ubungo pekee nakati serekali kila kukicha tunasikia hatuna hela,Tuwe na wabunge wenye kutoa mchango wa ni njia gani za kupata hela/kukusanya kodi,kusimamia matumizi ya hela ,kusimamia rasilimali za taifa,kuzuiya mianya ya rushwa,uwajibikaji,ufisadi,utoroshwaji wa hela na kwenda kuziweka nje ya nchi ambako zimekaa tuu na kunufaisha nchi tajiri,na tuwe na wabunge wazalendo kama ambao tumewasikia katika kikao cha bunge kilicho isha.Tukisha fikia hatua hii ndipo tuhoji nikipi kilicho fanywa cha maendeleo katika jimbo langu,tusiridhike tuu kwa kupigiwa greda barbara na kuwekewa calvat na vikao vya kupewa pilau na T-shert then tunaridhika mapema kumbuka kupigiwa barabara greda ktk barabara za halmashauri sii level yetu tungepashwa ziwekewe lami.Kwahiyo mheshimiwa Mbunge usikatishwe tamaa,kuibua ufisadi wa MABILIONI na kupigiwa greda kwa shilingi million moja kipi boraa? Nyie akina Ritz nawauliza kipi bora?katika hayo mabilioni yanayo fichuliwa na kurudishwa unajua yamesaidia majimbo mangapi?shule ngapi na mahospitali mangapi?na kwanini mnahoji kwa wabunge wa CDM pekee wamefanya nini?Juzi kati hapa kulikuwa na uzi uliokuwa unahoji Mdee kafanya nini jimboni kwake?mbona sioni wakiuliza waziri katufanyia nini au serekali imefanya nini?Kumbuka wabunge hawakusanyi kodi
 
Mkuu,
analysis yako ni nzuri sana, lakini tatizo dogo hujasoma ripoti yake yote kwa undani. Baadhi ya maeneo au barabara ulizotaja ameelezea kwa urefu kuhusu hatua ambazo zimefikiwa ktk ufuatiliaji wake na nini kinategewa kufanyika lini.

Mkuu nimesoma na hiyo taarifa ni ya muda nrefu. Shida yangu ni kwamba Mnyika awashirikishe wananchi ili wachonge barabara kwa kutumia grader jipya la manispaa ya kinondoni. Tufanye hayo ili barabara ziwe passable wakati tunasubiri MCHAKATO
 
mkuu Kimbunga pole sana kwa matatizo, hii baraabara ya Korogwe-Kilungule-external ilisababisha gari yangu kukata spring kati ya April/May. Mvua ikishanyesha ndio hapatamaniki kwa tope na mashimo,sasa kuna siku mvua ilinyesha masaa matatu tu! ilibidi tuwalipe vijana 3000/= kwa kila gari ili kutuongoza tusipotee njia.. maana barabara yote ilikuwa imefunikwa na maji na na tope zito

Mkuu Narubongo ndio maana mimi napiga kelele humu kuhusu jimbo la Ubungo. Jimbo hili lina changamoto nyingi sana na ni kubwa mno. Njia nzuri ya kuyakabili matatizo ya Ubungo ni kushirikisha wananchi na halmashauri ya manispaa ili barabara zipitike. wanaosema ati Mnyika akae tu na kuisimamia serikali hatafika kokote kwa kuwa serikali siku zote tunaambiwa haina ndururu!
 
Last edited by a moderator:
Mwita Maranya mimi sina chuki na Mnyika hata kidogo. Najua wazi kwamba Mnyika ana hoja nzuri sana za kulisaidia taifa hili. Michango yake ni muhimu sana bungeni lakini hoja yangu ni kwamba akumbuke jimbo pia. Watu wake tunataabika. Abalance mambo. Jimbo la Ubungo lina changamoto nyingi bila kujiandaa na kujizatiti kuzikabili changamoto za jimboni Mnyika ataumia.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu, hizo ndizo akili za watanzania. Yaani they like shifting burdens! Just because there is Mnyika basi wao wanakaa na kurelax. Nadhani kuna sehemu hapo mwanzo tulikosea. Dhana ya uwajibikaji haikutiliwa mkazo katika taifa. Hatimae sasa tuna kizazi kisichopenda kazi

1. Elimu
2. Elimu
3. Elimu

kweli tunahitaji hivi vipaumbele, maana bila kubadili jinsi tunavyofikiri kazi ya kusonga mbele itakuwa ngumu sana
 
Nimesoma kazi ulizofanya, ofcourse nyingi sana nazijua lakini hata kama perfomance ya jimboni isingekuwa kubwa, bado kazi unazofanya bungeni ingenifanya nikuunge mkono tena kwa nguvu zote 2015 kama tulivyokuwa 2010. Bravo.
Hata hivyo, jiandae pia kupokea maoni ya Ritz & co.

Mara nyingi Ritz, na Rejao thread kama hizi huwa wanaingia dakika ileile baada ya mtoa hoja. Na mara zote wakishafanya hivyo wameshawajua kuwa nyinyi JF mtakurupuka kutoleta post za msingi na kuishia kurumba na wao.

Aisee, huwa wanafaulu sana kwa hili na sijui mtawagundua lini.

Sasa, ukishafika thread ya nane kama hii post yako basi kama walijisahau basi huwa inakula kwao maana wanajua wengi tu hawasomi post zote na hivyo wanaweza kabisa usiwaone labda kama wametajwa kama ulivyowataja.
 
Kwa akili zako huna Jeuri ya Kuishi Ubungo

Wewe kwa akili yako wadhani jimbo la ubungo ni ile sehemu ya ubungo tu! Ubungo ni kubwa sana na huyu jamaa aliahidi maji na umeme.. kuna maeneo ya ubungo hizo ahadi hajatimiza amejikita kuimarisha chama na kusahau jimbo lake... Aanze na kero ya maji apunguze maneno mengi
 
That is very true,
Na hapa ndipo mafisadi ya ccm yanapomiss lead watu kwa makusudi.
Kati ya majukumu makubwa 3 ya mbunge hakuna jukumu la kutumia fedha zake kuwaendeleza wananchi bali kuisimamia serikali ili itumie kodi vizuri. Kama tunampima Mnyika kwa kuangalia majukumu ya Mbunge kikatiba, na siyo kwa mazoea ya magamba he has done all the beyond my expectation, to be honesty.


Ni kweli lakini at list atembelee jimboni kwake.. wana ubongo wanalalamika anaishia kimara na pia vipi kuhusu pesa za maendeleo ya jimbo anazopewa mbunge .. ?? Tusidanganyane eti sio kazi ya mbunge while kuna pesa Za maendeleo ya jimbo wanapewa?!
 
Wewe kwa akili yako wadhani jimbo la ubungo ni ile sehemu ya ubungo tu! Ubungo ni kubwa sana na huyu jamaa aliahidi maji na umeme.. kuna maeneo ya ubungo hizo ahadi hajatimiza amejikita kuimarisha chama na kusahau jimbo lake... Aanze na kero ya maji apunguze maneno mengi

Unaona donge Mnyika akikijenga chama chake!? Mbona maDC na maRC wameidhinishwa rasmi na liwalo na liwe kujenga chama chao cha mabwepande kwa mgongo wa kodi zetu.
 
hongera sana kwa hakika tunaikubali mikakati na jitihada zako. Tupia macho pia suala la barabara ya kwenda Msakuzi kupitia mbezi mwisho. bara bara ni mbovu sana, kila wakati mashimo kwa wingi. Big-up Keep UpP tell them you are up.
 
MAJI:
Katika kufuatilia masuala ya maji nilianza kwa kufanya Kongamano la Maji katika Jimbo la Ubungo mwanzoni mwa mwaka 2011 ili kuwakutanisha wananchi, mamlaka husika na wadau wengine katika kuunganisha nguvu kupata ufumbuzi.


Hatua nyingine zote nilizochukua baada ya hapo zilikuwa ni za ufuatiliaji kuwezesha utekelezaji wa haraka. Nikiri kwamba katika hatua za awali ushirikiano kutoka DAWASA, DAWASCO na Wizara ya Maji ulikuwa mdogo kwa kiwango cha kuamua kuwaunganisha wananchi kupitia ‘maandamano ya maji' kwenda DAWASCO. Toka wakati huo ushirikiano umeongezeka kwa upande wa DAWASCO ambapo nimeshafanya nao ziara ya kikazi ya kata mbalimbali ya kutembelea maeneo yenye matatizo na hatua zimechukuliwa ambazo zimewezesha baadhi ya maeneo kuanza kutoka maji.


Pia, wakati wa hatua hizo nimewaonyesha DAWASCO biashara haramu ya maji iliyokuwa ikiendelea na baadhi ya maeneo wamechukua hatua ikiwemo kwa watendaji wao. Hata hivyo, udhaifu wa kimfumo uliopo ni mkubwa kuliko hatua ambazo zimeweza kuchukuliwa mpaka sasa. Katika mazingira hayo nilianza pia kutaka hatua za DAWASA na tayari nao nimefanya nao ziara ya kikazi kwenye vyanzo vya maji pamoja na matenki ya maji, na kutaka hatua za haraka za ushirikiano kati ya DAWASA na DAWASCO.


Kwa maana ya miradi ya muda mrefu ya mwaka 2013/2014 kumetengwa fedha kuanzia mwaka 2012/2013 zaidi ya bilioni 200 kutokana na fedha za MCC na Mkopo wa India kwa ajili ya upanuzi wa vyanzo vya Ruvu Juu na Ruvu Chini, ujenzi wa Bwawa la Kidunda na ujenzi wa mabomba mengine miradi ambayo itagusa wananchi wa Ubungo. Hata hivyo, hatua hizi za muda mrefu hazileti matumaini bila hatua za haraka ambazo zilipaswa kuchukuliwa katika mwaka wa fedha 2011/2012.


Katika kuwezesha hatua za haraka kwa mwaka wa fedha 2011/2012 nilifuatilia ratiba ya mgawo wa maji kuweza kutolewa kwa mbunge na kwa ngazi za kata na mitaa na kufuatiliwa ili mgawo uwezeshe kuheshimiwa bila ya upendeleo wa baadhi ya maeneo au hujuma kwa ajili ya kuwezesha biashara haramu ya maji. Ofisi ya mbunge wakati wote imetaka kupatiwa taarifa pale mamlaka husika au ngazi tajwa zinaposhindwa kufuatilia ratiba husika ili kuweza kuingilia kati. Kuanza kuweka miundombinu ya maji katika maeneo yaliyorukwa kwenye awamu ya kwanza ya uwekaji wa mabomba, tayari utekelezaji umeshaanza katika maeneo ya Mbezi na maeneo mengine utafanyika kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2013 kwa mujibu wa ahadi zilizotolewa na DAWASCO/DAWASA kwa mbunge.


Katika kutekeleza ahadi ya kuhamasisha ujenzi wa visima kwenye maeneo ambayo hayafikiki kirahisi na mtandao wa maji ya bomba kama suluhisho la muda, huku tukifuatilia ufumbuzi wa kudumu katika maeneo hayo, mbunge amefuatilia uchimbaji wa visima uliokuwa umesimama katika maeneo ya Mavurunza/Bonyokwa, Kilungule na King'ongo kwa kwenda maeneo husika, kuziandikia mamlaka zinazohusika na kuhoji kwenye vikao vya manispaa, bungeni na kufanya ziara za ukaguzi wa maendeleo ya miradi.


Uzinduzi kwa miradi ya Mburahati ulifanyika mwanzoni mwa mwaka 2011 na hatimaye sasa uzinduzi wa maeneo yaliyotajwa utafanyika katika mwaka huu wa 2012 kwa kuratibiwa na DAWASA na Wizara ya Maji.


Aidha, uchimbaji wa visima kama hivyo unaendelea katika maeneo ya Saranga na Malambamawili. Aidha, kupitia miradi ya Manispaa ikiwemo mradi unaofadhiliwa na benki ya dunia mbunge amefuatilia uchimbaji katika maeneo ya Mpiji Magohe, Msakuzi, Makoka na Msumi ambao unasuasua kutokana na udhaifu wa kiutendaji.


Mbunge ameunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau wengine wa maendeleo Jimboni Ubungo katika masuala ya maji hususani Shirika la Kibelgiji (BTC) katika maeneo ya Kwembe na Kibamba na amewasiliana na DAWASA/DAWASCO kwa ajili ya hatua za kusaidia miradi husika na TANESCO kwa upande wa kuweka transfoma yenye uwezo mkubwa zaidi ili kuwezesha pampu za maji kwenye maeneo husika ziweze kufungwa. Orodha ya maeneo mengine yaliyochimbwa visima vidogo ipo katika Ofisi ya Mbunge.


Mbunge amefanikiwa kufanya suala la maji kuwa moja ya masuala yanayojadiliwa mara kwa mara kwenye vikao vya Manispaa ya Kinondoni hali ambayo haikuwepo kabla. Aidha alipendeza na hatimaye ukafanyika ufuatiliaji wa miradi iliyo chini ya jamii au mamlaka za ngazi ya chini iliyokwama kwa muda mrefu na hivyo kukosesha wananchi maji katika maeneo mbalimbali ambayo hayapewi huduma ya moja kwa moja na DAWASA/DAWASCO. Kati ya miradi hiyo baadhi imefufuliwa kama wa Msewe Golani na mingi inaendelea kusuasua ikiwemo ya kata ya Goba. Mbunge amependekeza kwa DAWASA kwamba maeneo ambayo hayakuwa yakihudumiwa na DAWASCO ikiwemo ya kata ya Goba yachukuliwe moja kwa moja na mamlaka husika kwa kuwa kutokana na ongezeko la watu maeneo hayo hayawezi kuhudumiwa kwa ufanisi na kamati za maji kama ilivyokuwa miaka ya zamani.


Mbunge amefuatilia pia masuala ya bei na ubora wa maji na kuitaka bei ya maji inayotozwa kwenye Viosk inaendana na viwango vilivyopangwa na mamlaka husika (EWURA), kufuatia hatua hizo operesheni zimefanyika katika maeneo ambayo yanatoza maji kinyume na bei iliyotangazwa na DAWASCO imeingia mikataba na waendeshaji wa vioski husika kuhusu bei elekezi. Hata hivyo, changamoto imeendelea kuwa ni usimamizi wa utawala wa sheria katika kuhakikisha bei inayotozwa ni ile inayopaswa kutoswa kwa mujibu wa maagizo ya EWURA. Katika kipindi husika mbunge ametaka pia EWURA itoe bei elekezi kwa upande wa maji katika jiji la Dar es salaam kwa upande wa sekta binafsi ili kudhibiti pia biashara holela ya maji ya kwenye malori. Katika mwaka wa fedha 2011/2012 EWURA iliahidi kutoa kanuni za kudhibiti biashara husika hatua ambayo mpaka sasa haijachukuliwa, suala ambalo mbunge atalifuatilia katika mwaka wa fedha 2012/2013.


Mheshimiwa JJ,
Kwanza nikupe hongera kwa kazi kubwa unayoifanya bungeni. Wanaubungo tunajivunia wewe kuwa Mbunge wetu
Ila hapa kwenye ishu ya maji bado sijaona kama umefanya mambo makubwa sana kwani serikali ilitumia pesa nyingi kwenye mradi wa kusambaza mabomba kwenye eneo kubwa la Jimbo la Ubungo. Sasa cha ajabu mradi ule umetelekezwa na mumeanza kuchimba visima huku mkiacha yale mambomba yakioza aridhini. Kama chanzo cha maji kinauwezo mdogo na maji yanatolewa kwa mgao mbona vioski vinapata maji kila siku na tunaendelea kulanguliwa kwa 15,000/ kwa meta ya ujazo moja huku bei ya Dawasco haizidi 2,000/=??????? Hili linatuumiza kwani huduma ya maji ni muhimu na haina mbadala

USHAURI WANGU

Mheshimiwa tafadhali hii biashara ya maji ingepigwa marufuku AU huo mpango wa kudhibiti bei uje haraka kwani tunaumia sana. Maji yanatosha kwani haya tunayoyatumia majumbani kwetu ndiyo hayo hawa walanguzi wanayabypass kwenye vioski ili waje watulangue. TUMIA RUNGU TULILOKUPA 2010
NB: hawa walanguzi tunasikia wana pesa ndefu sana ukiwagusa tu.......
 
Ni kweli lakini at list atembelee jimboni kwake.. wana ubongo wanalalamika anaishia kimara na pia vipi kuhusu pesa za maendeleo ya jimbo anazopewa mbunge .. ?? Tusidanganyane eti sio kazi ya mbunge while kuna pesa Za maendeleo ya jimbo wanapewa?!

Pesa za maendeleo Mnyika ameshatolea hesabu vizuri sana, soma ripoti yake. Halafu huu ***** wako Mnyika hawezi kujibu labda akuonee huruma, maana nimeona akijibu baadhi ya hoja.
 
Mara nyingi Ritz, na Rejao thread kama hizi huwa wanaingia dakika ileile baada ya mtoa hoja. Na mara zote wakishafanya hivyo wameshawajua kuwa nyinyi JF mtakurupuka kutoleta post za msingi na kuishia kurumba na wao.

Aisee, huwa wanafaulu sana kwa hili na sijui mtawagundua lini.

Sasa, ukishafika thread ya nane kama hii post yako basi kama walijisahau basi huwa inakula kwao maana wanajua wengi tu hawasomi post zote na hivyo wanaweza kabisa usiwaone labda kama wametajwa kama ulivyowataja.

Nikupataje, nakubaliana na wewe.
Yaani ktk hoja hii ya Mnyika, nimefuatilia sana, Mnyika walijaribu kumtoa nje ya Mada wakakwama. Wakaleta masuala ya Singida Mnyika akawachunia, Aweda akaweka maelezo sawa kwa hoja na kurekebisha uwongo wao. Machizi Akina Ritz na Rejeo wakaingia mitini.
 
....[/QUOTE]

Mheshimiwa, ipo shida kubwa na ni sugu ya maji katika maeneo yote ya Kimara, wananchi walio maeneo ya Kimara walikuchagua kwa lengo kuu la kutatua kero hiyo ambayo ilionekana kumshinda mh. Keenja, hivyo, fanya yote usipotekeleza hilo hakika utakuwa na kipindi kigumu sana katika eneo la Kimara.
 
Pesa za maendeleo Mnyika ameshatolea hesabu vizuri sana, soma ripoti yake. Halafu huu ***** wako Mnyika hawezi kujibu labda akuonee huruma, maana nimeona akijibu baadhi ya hoja.


Oh! God ! There are some really thick people humu JF hapo kwenye RED Bilionea one you've been missing your meds... yeye kama nani anionee huruma!..? huruma ninayohitaji ni from my almighty Allah ni si kutoka kwa politician


 
Someone wrote this in 2010 as an advice for John Mnyika. It is very important. Please mheshimiwa Mnyika...usisahau maneno haya na yatumike kwa chama chote.

Anonymous said...
Kaka hongera sana, ila ujue tu una kazi ngumu sana. Vyama vya upinzani inabidi muendeshe kampeni zenu kistaarabu na mjue kuwa washindani wenu wanahakikisha kuwa wanawafrustrate kila hatua na nyie mnajisahau na kuishia kwenye jazba. Hii inawafanya ku overeact na matokeo yake wananchi wengi wanawaona hamfai uongozi.
Wakati wa kampeni zako achana na vijana wasiokuwa na kazi wale wa mtaani ambao uelewa wao ni mdogo, kwani mara nyingi ni watu wa fujo zisizokuwa na msingi na inaharibu image ya chama na hata candidate. Nakuhakikishia kuwa huu ni wakati wa kudeal na issues na si majina ya viongozi wa CCM kwani hakutakuwa na ile uniqueness ya kambpeni. Nakushauri uendeshe kampeni in a very professional manne, you can borrow a leaf kutoka Obama ana Hilari Clinton campaigns kuanzia sasa ili ujipange mzee.
Ni wakati wa kuanza kutumia blog, utube, sms, fm radio station kueneza sera zako jijini DSm. ikiwezekana tumia TV, shiriki talk shows nyingi au organize talk shows kwenye FM radio from now on na mada zilenge issues zinazowaface wakazi unatarajia kuwatumikia. Epusha kulalamika na kulaumu, ila njoo na mtizamo mpya.
Nikutakie kampeni safi, nimeifuraia blog yako.
Mungu akusaidie,

March 23, 2010 7:10 AM
 
Back
Top Bottom