Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Aug 21, 2012.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Napokea kwa unyenyekevu pongezi zilizotolewa na wachangiaji mbalimbali hapa JF lakini izingatiwe kuwa michango yangu bungeni ni matokeo ya heshima mliyonipa ya kuwawakilisha. Aidha yapo maoni machache ambayo yametoa tafsiri tenge kuhusu kazi ya mbunge na wengine mmetaka nieleze nimefanya kazi gani za maendeleo jimboni Ubungo.

  Tarehe kama ya leo 21 Agosti 2005 nilianza mchakato wa kuwa kugombea ubunge nikiwa kwenye chakula na watoto yatima, tarehe kama hiyo mwaka 2010 nilianza kampeni za uchaguzi mitaani Ubungo, tarehe hii hii kwa mwaka huu wa 2012 naomba niitumie kutoa taarifa fupi ya utekelezaji kwa masuala ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2011/2012 uliomalizika tarehe 30 Juni 2012;
  http://mnyika.blogspot.com/2012/08/taarifa-fupi-kuhusu-kazi-za-maendeleo.html kuhusu elimu, ajira, miundombinu, maji, usalama, uwajibikaji, ardhi na afya; taarifa ya kina ya utekelezaji nitaitoa nitakapotimiza miaka miwili ya utendaji.

  Hivyo, ufanisi wa ubunge wangu upimwe kwa kuzingatia msimamo huu kuhusu kazi nne za mbunge katika kuwezesha maendeleo:
  http://mnyika.blogspot.com/2010/03/natangaza-rasmi-dhamira-ya-kugombea.html ambao niliwaeleza wananchi wakati wa uchaguzi hivyo nilichaguliwa ikifahamika wazi kuwa huo ndio wajibu ambao nitautekeleza katika kipindi cha miaka mitano.

  Bado naendelea kuamini kwamba jimbo la Ubungo na taifa kwa ujumla tutapiga hatua ya haraka zaidi ya maendeleo kupitia mabadiliko katika mifumo yetu ya mgawanyo wa rasilimali na usimamizi wa matumizi ya fedha za umma na pia kwa kuweka mazingira bora ya kisera, kisheria na kiutendaji wa sekta binafsi.Tuliyoyafanya mpaka sasa ni sehemu tu katika mahitaji makubwa ya maendeleo kutokana na pengo la miaka 50 ukilinganisha na fursa ambazo taifa letu linazo; hata hivyo naamini miaka mitatu iliyobaki itafanya miaka mitano ya kuisimamia Serikali iliyopo madarakani hivi sasa pamoja na udhaifu wote uliokuwepo kuleta tofauti katika maendeleo majimboni.

  Ni katika muktadha huo wakati mwingine tunazimika kuwakilisha na kuwasilisha matakwa ya wananchi namna hii:
  http://www.youtube.com/watch?v=ES4OMOD_xME tukiamini kwamba watawala wenye dhamana kwa sasa ya kukusanya kodi watasikiliza na kuzingatia vipaumbele vya maendeleo vya wananchi.Aidha, baada ya kazi mkutano wa nane wa bunge naomba kutumia fursa mjadala utakaofuatia taarifa hii kupata maoni yenu kuhusu masuala ninayopaswa kuyapa kipaumbele katika kuwawakilisha na kuwatumikia jimboni katika kipindi cha mwezi Septemba mpaka Oktoba 2012 kabla ya kuanza kwa mkutano wa tisa wa bunge na pia kuhusu maandalizi ya mwaka 2013.

  Kero nyingi zinazoendelea kuwepo kwa sasa ni neema iliyojificha (blessing in disguise) ili tuendelee kuunganisha nguvu ya umma kuendeleza wimbi la mabadiliko. Narudia tena kuwakumbusha kuwa nguvu ile ile tuliyoitumia kwenye kutafuta kura na kulinda kura ndio naiomba toka kwenu katika hatua hii ya kufanya kazi za kuwezesha maendeleo kwa kutimiza wajibu kila mmoja wetu kwa nafasi yake, kuisimamia serikali na kuunganisha rasilimali za wadau wengine; Maslahi ya Umma Kwanza.
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Kamanda.inatia moyo sana sana
   
 3. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh. Mnyika, kwanza natoa pongezi kwa kututoa dukuduku cc waumini wa siasa za Nchi hii kupitia hapa JF. Lakini pia kwa kua 90% ya waliokupa kura zao 2010 ni raia wa kawaida wasiojua au hawajapata fursa ya kujua kutumia mitandao ya kijamii nahitaji ujumbe huu uwafikie wao kwani ndio wanaojua utendaji wako hasa katika jimbo la Ubungo.

  Ni mkakati gani ulionao ili taarifa kama hizi ziwe katika ncha za vidole vyao?
   
 4. P

  Pokola JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  You are the visionary.
  No More to say.
   
 5. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mungu akusimamie na iwe kama unavyoamini......kila la kheri.

  Ingekua vyema na wenzio wakajitoa na kuelezea nini walichofanya/wanayoendelea kufanya kwenye majimbo yao especially Halima Mdee.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongera sana John.Taarifa yako imenikumbusha kwanini wewe ni mbunge bora zaidi kwa kuwa na michango mingi bungeni.Lakini niwapongeze viongozi wetu wakuu Mbowe na Dr Slaa kwa kukupika na ukapikika.Hongera John vijana tunakujivunia....
   
 7. D

  DOMA JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Big up mkuu
   
 8. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kazi ulizofanya, ofcourse nyingi sana nazijua lakini hata kama perfomance ya jimboni isingekuwa kubwa, bado kazi unazofanya bungeni ingenifanya nikuunge mkono tena kwa nguvu zote 2015 kama tulivyokuwa 2010. Bravo.
  Hata hivyo, jiandae pia kupokea maoni ya Ritz & co.
   
 9. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,714
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  watakuja na kejeri zao muda c mrefu!!!!!!!!!!!! hongera mhe.
   
 10. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  "I am proud of you Mnyika kuwa mbunge wangu"
   
 11. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Naomba kuunga mkono hoja hii kwa nguvu sana.
  Nashauri ripoti hii uichapishe na kuisambaza ktk jimbo lote. Viongozi wote wa chama ktk ngzi kata na tawi waipate ili wawaeleze wananchi.Ofisi zote za chama iwe na nakala.

  Pili, Ni ukweli kwamba wagombea watarajiwa wa vyama vyote wanaeneza taarifa za uwongo huko mtaani kuwa wewe ni mbunge wa magazeti na mjengoni. Ukisambaza taarifa hii utakuwa umekata mzizi wa fitina.

  Tatu, si vibaya kama utawaambia wengine kupitia vyombo vya habari. Well, wako watakaosema unatafuta cheap popularity, lakini ndivyo walivyomsema mbowe na helikopta yake 2005 lakini baadaye nao wakamwiga.

   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Wale wanafiki wanaokupinga wataishia kunawa tu....we maji ya moto na ni moto wa kifuu
   
 13. m

  mgosiwakaya Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  safi sana mkuu tulianza na ww kwa kulinda kura na tutamaliza na ww katika kusaidiana kuleta maendeleo siyo ubungo tu bali tanzania kwa ujumla kwan ww ni mbuge wa kitaifa!
   
 14. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mkuu Mnyika,
  Kazi yako ni hakika kila mtu anaikubali labda awe kuadi wa UFISADI. Tunashukuru leo upo nasi hapa kwenye forum. Nina ombi kwako mkuu wangu. Kwa niaba ya wapigakura wako wa Msakuzi/Makabe ninaomba kwa heshima na taadhima sasa ututembelee tusaidiane kutatua baadi ya changamoto ambazo zinatishia ustawi wa jamii yetu. Mambo ambayo tunataka utusaidie kusukuma ni;
  1. UMEME: Mh. ni kwamba tunaishi msakuzi, njia ya kuelekea Mpiji magoe. Kitongoji chetu kina nyumba zaidi ya mia moja. Pia kuna nyumba/makazi ya watawa wa Katoliki pamoja na shule ya chekechea. TANESCO waliplan kuleta umeme maeneo hayo na tayari walileta na nguzo, cha ajabu nguzo zimeanza kuoza huu mwaka wa pili sasa umeme haupo. Cha ajabu maeneo ya jirani kuna umeme na tunazuiliwa kuunganisha umeme kutoka maeneo hayo kwa kisingizio cha kuw tuko kweye mradi mkubwa. Hivyo mkuu tunaomba ututembelee ili tupange pamoja nawewe namna ya kutusaidia.
  2. Maji. Tunaomba ufatilie kwa kwa nini maji ya Ruvu juu yanatoka mbombani kwa wiki mara moja tuu na tena kwa mgao. Angalia isije ikawa ni hujuma dhidi yako ili wananchi wakuchukie kuwa huwatetei. Nadhani njia nzuri ni kututemeblea ili upate kero za wananchi

  Ahsante

  Mpigakura wako
   
 15. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kudos!
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Hivi wabunge wangapi wanaweza kujipima ubavu na utendaji wao kwako?....nadhani ni wachache sana wanaoweza kuvaa viatu vyako pamoja na kuwa mgeni kabisa ktk ulingo wa siasa
   
 17. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mnyika yale yote ulioahidi hujatekeleza hata moja, ila kwa kupiga domo bungeni hilo umefanikiwa, nia yetu ya wakazi wa ubungo ni kutekeleza uliyotuahidi vinginevyo 2015 ukae mguu sawa ukalime.
   
 18. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  nachukua fursa hii kukupongeza kwa kazi nzuri uayofanya pia nakuomba uongeze jitihada katika kuwateta wananchi wanyonge wanaoonewa na taasisi a kiserikali kama vile TANROAD. mwaka 2007 bunge lilipitisha sheria mpya ya barabara na kanuni zake mwaka 2009 ambazo zinztaja hifadhi ya barabara kuwa ni mita 30 badala ya 22.5 kwa barabar zote kuu kila upande toka katikati ya barabara, na Mita 60 badala MIta 120 kwa barabara ya kuu ya Morogoro.

  Lakini hadi sasa watendaji wa TANROAD hawataka kukubali mabadiliko haya ya sheria waliyoyapitisha wenyewe na kupitishwa na bunge pia. Hali hii inawaathiri kiuchuni wananchi wanaoishi kandokndo ya barabara kuu ya Morogoro. hivyo unatakiwa kuwashinikza TANROAD waweke mipka mipya ya hifadhi ya barabarayaani Mita 60toka katikati ya barabara ili wananchi waweze kuitumia ardhi yao kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kukuza ajira
   
 19. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Kimbunga mnyika yupo online sasa hivi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Well said, well done JJ..Big UP!
   
Loading...