Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Tumeamua kugeuza siasa za Tanzania kuwa kama taarabu!!!?
Imekuwa sasa ni kitu cha kawaida watu kusubiria kuona nani kamnanga nani kisha nani kamjibu na kamjibu nini.Au watu kusubiria waone nani anamzodoa nani ili wajibu. Basi unaibuka ushabiki wa pande zote zinazodoana na siku zinaendelea kwenda. Kadhalika kuna kundi ambalo liko standby kuripoti nani kamzodoa nani na nani kamjibu.
Kwa bahati mbaya hata wale ambao wanatajwa kama wasomi; wengine wakiwa hata na shahada kadhaa, hukikuta kwenye mtego huo. Yaani hatimae tunajikuta kwa asilimia kubwa tunapofikiri na kujadili siasa za Tanzania, badala ya kujadili ni nini hatma yetu kama watanzania na Tanzania kwa ujumla; tunajadili jinsi tunavyozodoana tu! Zaidi ya hapo mambo ya msingi hakuna Mwenye muda wa kufikiri wala kujadili.
Nijuavyo Mimi kuzodoana ni Tania ya kwenye morden taarab kwa kuwa inalenga burudani, lakini hatupaswi kutumia akili, rasilimali na muda wetu wa thamani kufanya kazi ya kuzodoana tu kwani siasa ndio huamua hatma ya maisha yetu.
Hebu tulitafakarini hili kwa kina na tuone kama inafaa kubadilika ama la! Ila kwa maoni yangu tukiamua kubadilika itapendeza.
Aidha, silazimishi mtu kukubaliana na mawazo yangu ila kama mtaniunga mkono nitafarijika kwani naamini mabadiliko haya ni muhimu kwa ustawi wetu sote.
Wengi kuna vitu vingi hatuna ila angalau muda ni rasilimali muhimu ambayo wote Mungu katupa. Nafikiri inafaa kuutumia vyema kujadili mambo yenye maslahi mapana kwetu sote na nchi yetu kwa ujumla. Nchi zilizoendelea na jamii zake kusrawi vyema aghalabu hutumia muda wao vyema.