Taarab.....

Jestina

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
4,831
1,710
hivi kwa nini music wa taarab mara nyingi ujumbe wake ni wa kutambiana kuchukuliana mwanaume,utasikia 'huna mambo',hunirushi roho...utalijua jiji. nimesikiliza ni wanawake kutambiana kumchukua mume..hivi wale wanamusic wa taarab hawana ujumbe mwingine kama mgao wa umeme,maisha kupanda...huduma mbovu za nchi yetu au hainogi LOL.....
 
Last edited by a moderator:
mziki huuni wa kukusaidia kumkamata mmeo mama eeh!!!
wapo wenzako wanajua jinsi ya kukamata na kutunza....#
hutaki nenda magomeni kwa mama aziza!!!
 
Wizara husika ya maadili iliangalie hilo nalo na hasa lugha na maneno wanayotumia kwenye tungo za mistari yao.hongera sana kuliona hilo!
 
Hiyo sio Taarab hiyo ni rusha roho. Taarab ukiisikiliza unaona raha inafundisha, ina vina, ina mizani, hata music yake imetulia. Hiyo ya kupigwa lango la jiji nayo unaiita Taarab? Unanchekesha!
 
Faiza embu weka video ya Taarab,ili tujue kutofautisha...anyhow...hio rusha roho hawawezi rusha roho na mambo mengine zaidi ya 'mume'?? Lol
 
ya lango la jiji inaitwa aje?
 
sina mume mie bado,
hamna ujumbe mwingine mbona wote tunaimba kumkamata huyo mume?

ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu bi shosti!
Kule thread nyengine si umemwambia kongosho asikuchuze unaogopa kuachika?
Which is which sasa?
 
Hiyo sio Taarab hiyo ni rusha roho. Taarab ukiisikiliza unaona raha inafundisha, ina vina, ina mizani, hata music yake imetulia. Hiyo ya kupigwa lango la jiji nayo unaiita Taarab? Unanchekesha!

mnanchekesha sana nyie mabibi!
Kwa hiyo wewe ulitaka mpaka 2050 watu waendelee kuimba kwa kusinzia na kupiga 'midomo ya bata'?
Mambo huwa yanabadilika mpendwa, hiyo ya Lango la Jiji nayo ni taarab vilevile.
Siamini kama muziki wa Mohamed Ibrahim(1905) unafanana na wa Patricia Hilary(1980's), na kwanini isifanane, ishu ni simpo, muda!
 
Faiza embu weka video ya Taarab,ili tujue kutofautisha...anyhow...hio rusha roho hawawezi rusha roho na mambo mengine zaidi ya 'mume'?? Lol

siezi weka link, ila tafuta wimbo wa Mzee Yusuph ft. Hadija Yusuph - Undugu hazina yetu, pia cheki na wimbo wa Isha Ramadhani - Hayanifiki, Leila Rashid - Langu rohoni, nimekupa mifano michache isiyozungumzia kupokana waume, mwingine aweza kuongeza mingine.
Sawasawa?
 
Wizara husika ya maadili iliangalie hilo nalo na hasa lugha na maneno wanayotumia kwenye tungo za mistari yao.hongera sana kuliona hilo!

sio mbaya ukasema hayo maneno ili tuyatazame.
Usiwe kama viongozi wa chama fulani wanaosema 'tusipokuwa makini mbegu ya udini itatumaliza', bila kutwambia u wapi huo udini.
Sawasawa?
 
siezi weka link, ila tafuta wimbo wa Mzee Yusuph ft. Hadija Yusuph - Undugu hazina yetu, pia cheki na wimbo wa Isha Ramadhani - Hayanifiki, Leila Rashid - Langu rohoni, nimekupa mifano michache isiyozungumzia kupokana waume, mwingine aweza kuongeza mingine.
Sawasawa?

uko deep kwenye taarab, unaishi lango la jiji?
 
Back
Top Bottom