Taaluma/Fani/Biashara zinazoenda kupungua na kufa miaka 20 ijayo

Elon Musk anasema tishio kubwa la Binadamu ni kupungua watu duniani.
Japan wapo mbele sana kitekilojia employment rate yao ipoje?
Kila kitu kina create new job opportunity tena nyingi tu.
Ila Africa bado kama mdau alivyosema hapo juu tv bado ni Anasa Africa.
Tanzania magari mengi ni ya miaka 15 iliyopita.
Mitumba tupu
 
Kuna kitu kimoja unasahau.
Binadamu tunategemeana.
Ikiwa wewe kazi yako imechukuliwa na robot utapata wapi hela ya kununua Hilo robot likufanyie kazi zako?.
Sawaa maroboti yanaweza yakazalisha vitu vyote vya duniani.lakini je Nani atakuwa na hela ya kuvinunua wakati ajira zimechukuliwa na maroboti?
binadamu atafanya kazi gani ya kumuingizia kipato?
Hatutakiwi kutegemeana kwenye mambo ya kuhudumiwa kama mtwama au jayanti la kuhudumiwa ila tunatakiwa tufanye mambo yetu wenyewe na muda utumike vizuri na kufanya mambo makubwa maana yanahitaji muda, Sasa vitu vinakuja vya kuokoa muda mfano mtu siyo kilema anamaliza kula anakaa anasubiri kupewa maji anawe badala ya kunawa mwenyewe Ili aendelee na kazi za kuboresha kitu alichokuwa anafanya Sasa hapo napo atasema tunategemeana? Kazi yangu ikichukuliwa na robot nitauza hizo robot na nitajifunza kuzirekebisha hizo robot zikiharibika Ili nipate hela na pia nikiwa na muda mwingi nitafanya kazi nyingi ziniingizie hela.
 
Ujio wa teknolojia mpya katika maisha ya mwanadamu mara zote umekua na lengo la kumsaidia mwanadamu kwenye kazi zake za kila siku na maisha kwa ujumla.
Miaka 20 iliyopita hatukua na ATM machine Tanzania,ama zilikuepo chache sana,hii ilipelekea wafanyakazi wa serikalini na sekta binafsi kulipwa na cashier,hapo unaweza kuona ATM machine imeondoa uwepo wa maelfu na malaki ya cashier,kiasi tulitegemea vyuo vipunguze udahili mpya wa wanafunzi wa hio fani lakini matokeo yake wanaongeza na kila mtu mwisho wa siku anakuja kulalamikia tatizo la ajira ambalo wangeweza kulitatua hapo awali,.
........huo ni mfano tu,wa maiaka 20 iliyopita ila zipo fani pia zitakazoathiriwa na uwepo wa teknolojia mpya miaka 20 ijayo,
1.UHASIBU
Uwepo wa blockchains na smart contracts platforms utawezesha mtu aliye nyumbani kitandani kwake,kuangalia Salio,kutuma pesa popote pale duniani,na kuomba mkopo instantly bila kwenda banks wala ofisini.
Kampuni zitakua na uwezo wa kuruns mihamala yao bila kushirikisha muhasibu,auditors firms zitapunguza manual work, platform zitahitaji watu wachache wa kuzisimamia.

2.wafanya kazi wa viwandani.
Tafiti zinaonesha robots zinafanya kazi za viwanda kwa zaidi ya 80% ya binadamu kwa efficiency ya zaidi ya 90%.
Ukienda Europe, America viwanda vya magari na mitambo hadi vya kutengeneza pipi unashangaa wafanyakazi hawazidi hata 100,robots zinafanya kila kitu,hii hata Tanzania itakuja soon,kuruns robots ni rahisi na hazili,haziibi wala hazipumziki.

3.Surgeons
Uhitaji wa madaktari wa upasuaji utapungua kwa zaidi ya 30%,operation nyingi zitakua zinafanywa na robots.......surgeon atakua anafanya operation chache mno, laparoscopic surgery ambayo ilikua inafanywa na binadamu itakua inafanywa na robotic machines,kwa ustadi mkubwa na accuracy .

4.Mitandao ya simu,na Minara ya simu,Vocha.
Taaluma kama telecommunication engineer zitapunguza demand,sababu ya satellite internet ambayo itakua ni popote pale na kwa gharama nafuu,...unaweka tu dish unakula MB za kutosha hata milimani huko,Minara ya simu watoto watakua wanaishangaa wanajiuliza ni nini hiko babu?
Vocha zitakua kwenye makumbusho,vibanda vya MPESA tutafugia njiwa,smart contract platforms zilizokua linked na satellite internet zitaweza fanya kila kitu.

5.
Hii namba mbili kwa nchi nyingi za kiAfrika ikiwemo na Tanzania,bado sana...usije kuona viwanda huko nje ukadhani ndo vitakua hapa kiasi cha kuwepo robots. Bado
 
Hatutakiwi kutegemeana kwenye mambo ya kuhudumiwa kama mtwama au jayanti la kuhudumiwa ila tunatakiwa tufanye mambo yetu wenyewe na muda utumike vizuri na kufanya mambo makubwa maana yanahitaji muda, Sasa vitu vinakuja vya kuokoa muda mfano mtu siyo kilema anamaliza kula anakaa anasubiri kupewa maji anawe badala ya kunawa mwenyewe Ili aendelee na kazi za kuboresha kitu alichokuwa anafanya Sasa hapo napo atasema tunategemeana? Kazi yangu ikichukuliwa na robot nitauza hizo robot na nitajifunza kuzirekebisha hizo robot zikiharibika Ili nipate hela na pia nikiwa na muda mwingi nitafanya kazi nyingi ziniingizie hela.
Hivi ulaya na marekani na Asia na Australia wakitumia maroboti ghafla Africa nayo ikaanza kutumia maroboti.
Nani atamuuzia mwenzie bidhaa?
Uchumi wa dunia utaendeshwa vipi?
 
Hata uwepo wa Diagnostic imaging umepunguza kazi zilizokua zinafanywa na physicians kwenye kufanya clinical examination,........ila hazijareplace uwepo wa physician........kupunguza kwa kazi iliyokua inafanywa na physician hatimae kumepunguza uhitaji wa physicians ambao walihitajika kabla ya hizo machines........na kwa kutumia huo mfano fani zote zimeathirika zingine kwa 100%,80% ,50% hadi 10%.
I practice laws, anyway kila nikijaribu kuitazama hii taaluma sioni jinsi AI itakavyochukua nafasi ya lawyers. Labda unachokiona mimi bado sijakigundua. Lakini likelihood ya kuwa na robotic lawyers kwa kweli siioni kabisa.
Ifahamike kuwa laws are meant to regulate human conduct, sasa hizi mashine kwamba ziweze kufanya kazi inayofanywa na binadamu ambaye will always find a way to maniputate laws!? Wacha tungoje wakati huo ufike tuone huo muujiza wa AI
 
Naona umejibu nje ya point yangu ya msingi.
labda nikuulize unadhani IPO siku itakuja kutokea binadamu hapa duniani asifanye kazi akamuachia robot Peke yake?
Asiyefanyakazi na asile ni Mungu alituusia wanadamu tufanye kazi Ili tupate kipato hivyo hakuna siku binadamu ataacha kufanya kazi akamuachia robot ila kinachofanyika ni huyo binadamu kupata vitu vya kirahisisha kazi na yeye binadamu kupata muda mwingi wa kufanya vitu vingi kwa muda mfupi na vitu vikubwa vyenye kuleta utukufu wa Mungu, mfano swala la kununua umeme au kupata maji likiwa kwa njia ya luku kwa haraka na kununua kitu ulichotumia bila kuibiwa kwa kusomewa vibaya mita tayari hapo wengi au wote watakuwa wameokoa muda na kupata akiba ya kile ambacho wangesomewa mita vibaya na kupoteza mapato yao na kama ni watu wenye kujali kuweka akiba basi watapata akiba ya hela na muda wa kufanya kazi zingine, pili binadamu akiletewa robot hatakosa kazi Ila atapata muda mwingi wa kufanya kazi kwa ufanisi na haraka maana hizo robot bado zitategemea watu kuzitumia kama vitendea kazi ila kazi nyingi zitafanyika kwa muda mfupi kama hizo za kupokea na kutuma pesa ni watu wengi wanaweza kupokea na kutuma kwa wakati mmoja na kuendelea na kazi zingine, kujenga nyumba nzuri kwa muda mfupi kwa vitu hivyo vya kurahisisha kazi na kwenda kujenga tena na hivyo hivyo kwa kazi zote zitafanyika kwa wingi.
 
I practice laws, anyway kila nikijaribu kuitazama hii taaluma sioni jinsi AI itakavyochukua nafasi ya lawyers. Labda unachokiona mimi bado sijakigundua. Lakini likelihood ya kuwa na robotic lawyers kwa kweli siioni kabisa.
Ifahamike kuwa laws are meant to regulate human conduct, sasa hizi mashine kwamba ziweze kufanya kazi inayofanywa na binadamu ambaye will always find a way to maniputate laws!? Wacha tungoje wakati huo ufike tuone huo muujiza wa AI
Kwa hio kazi ya lawyers ni kumanipulate laws na sio kuimplements according to codes of conducts?......lawyers wa nchi yenye mifumo mibovu hao,kama kwenye kesi ya Mbowe
 
Asiyefanyakazi na asile ni Mungu alituusia wanadamu tufanye kazi Ili tupate kipato hivyo hakuna siku binadamu ataacha kufanya kazi akamuachia robot ila kinachofanyika ni huyo binadamu kupata vitu vya kirahisisha kazi na yeye binadamu kupata muda mwingi wa kufanya vitu vingi kwa muda mfupi na vitu vikubwa vyenye kuleta utukufu wa Mungu, mfano swala la kununua umeme au kupata maji likiwa kwa njia ya luku kwa haraka na kununua kitu ulichotumia bila kuibiwa kwa kusomewa vibaya mita tayari hapo wengi au wote watakuwa wameokoa muda na kupata akiba ya kile ambacho wangesomewa mita vibaya na kupoteza mapato yao na kama ni watu wenye kujali kuweka akiba basi watapata akiba ya hela na muda wa kufanya kazi zingine, pili binadamu akiletewa robot hatakosa kazi Ila atapata muda mwingi wa kufanya kazi kwa ufanisi na haraka maana hizo robot bado zitategemea watu kuzitumia kama vitendea kazi ila kazi nyingi zitafanyika kwa muda mfupi kama hizo za kupokea na kutuma pesa ni watu wengi wanaweza kupokea na kutuma kwa wakati mmoja na kuendelea na kazi zingine, kujenga nyumba nzuri kwa muda mfupi kwa vitu hivyo vya kurahisisha kazi na kwenda kujenga tena na hivyo hivyo kwa kazi zote zitafanyika kwa wingi.
Basi hakuna mbadala wa binadamu
 
Kwa hio kazi ya lawyers ni kumanipulate laws na sio kuimplements according to codes of conducts?......lawyers wa nchi yenye mifumo mibovu hao,kama kwenye kesi ya Mbowe
😂😂😂😂 Mkuu, hata Shakespeare alishaandika, let's first kill all the lawyers. Siku utakapoingia kwenye mgogoro na/wa sheria/ kisheria ndiyo utajua kama kazi ya is to manipulate the laws or make laws work in your favour or against you
 
Mkuu kwenye surgeons si kweli.....anatomy haifanani sana kuna tofauti kidogo.........sehemu za mwili pia zinatofautiana ukubwa.....
Ukija swala la upasuaji kutibu kansa ndio haitawezekana kabisa magonjwa hayasomi vitabu.....
Hapa kwenye Surgery soon Surgeons wanaenda kuwa replaced maana AI inauwezo wa kufanya operation kwa precision kubwa kuliko binadamu
 
Kwa Afrika bado sana. Hayo mambo yatakuja ila kwa mwendo wa kobe.
Jiulize mpaka sasa Serikali bado inahangaika na kujenga shule, maji na umeme. Labda useme miaka 1000 mbele hivi. Kwa sasa bado sana.
Wenzetu wameshaanza kutumia roboti tayari sisi hapa Tanzania kuna kiwanda gani kinatumia Roboti? Ukienda hospital iwe private au serikali kuna uhaba wa vifaa pamoja madawa. Sasa hizo teknolojia wataweza kuzimudu?
Hata mambo ya satelite bado sana ila baadhi huduma zipo ila mpk utumie kampuni za nje km Google. Sasa hivi hata huduma ya fiber, ukiwa Gongo la mboto hiyo huduma ya Zuku, TTCL n.k hakuna.
Afrika hakuna pesa ndiyo maana mpk sasa tunatumia jembe la mkono.
1980......wazee wetu waliopata exposure walisema Africa bado sana kutumia computers,ATM machines,.....simu,TV etc,hata kumiliki gari ilikua ni anasa sana miaka hiyo..........muda haudanganyi
 
Veterinary. Hii hata miaka 1000 ijayo tutahitajika tu
Mkuu Chancellor Sasa hivi Kuna app ambayo nascan kinyesi Cha kuku hapohapo napata majibu ya ugonjwa alionao kuku. Kisha napewa list ya dawa za kutibu. Kaa chonjo Mkuu. Yara Wana app Yao moja inaitwa farmcare inatoa ushauri kama wa Bwana Shamba.
 
Kwa Afrika bado sana. Hayo mambo yatakuja ila kwa mwendo wa kobe.
Jiulize mpaka sasa Serikali bado inahangaika na kujenga shule, maji na umeme. Labda useme miaka 1000 mbele hivi. Kwa sasa bado sana.
Wenzetu wameshaanza kutumia roboti tayari sisi hapa Tanzania kuna kiwanda gani kinatumia Roboti? Ukienda hospital iwe private au serikali kuna uhaba wa vifaa pamoja madawa. Sasa hizo teknolojia wataweza kuzimudu?
Hata mambo ya satelite bado sana ila baadhi huduma zipo ila mpk utumie kampuni za nje km Google. Sasa hivi hata huduma ya fiber, ukiwa Gongo la mboto hiyo huduma ya Zuku, TTCL n.k hakuna.
Afrika hakuna pesa ndiyo maana mpk sasa tunatumia jembe la mkono.
Kwanza hata umeme wa mambo hayo uko wapi???Robot likikata power linakuacha unajifia hapo lenyewe limesizi theatre
 
Aisee sikua najua hili.....huu uzi unaweza kua msaada kwa wadogo zetu wanapambana kutafuta Diploma na Degree za fani mbali mbali.
Kijana mjanja ni yule anayesoma fani ambayo ni ngumu kufanywa na machines au robots,ngumu kuwa replaced etc
Kama vile
 
Hiyo app unaidownload kwa kutumia 66mb kisha km kuna malipo utalipia 20,000 kwa mwezi. Sasa jiulize hapo unaweza kununua robot na trekta? Unauwezo wa kulipia laki 2 kwa mwezi kupata satellite internet? Wenzetu wameshaanza hayo mambo kitambo sana ila sisi Afrika itakuja kwa mwendo wa kobe.
Kwasasa inawezekana kwa mambo rahisi rahisi km App ukiwa na smartphone yako tu unafanya

Back
Top Bottom