Taa za barabarani

Masika

JF-Expert Member
Sep 18, 2009
723
30
Habari wadau wa teknolojia? Naomba mnijuze jinsi taa za barabarani zinavyofanya kazi maana zinanishangaza giza likitokea zinawaka mwanga ukitokea zinazima halafu kila siku na zinatumia umeme au mwanga wa jua?
 
Zinatumia umeme, kuwaka na kuzima inaweza ikawa kuna mtu anawasha, zinawaka na kuzima kutokana na timer, au zina light sensor na zinawaka mwanga wa jua ukishuka kiwango fulani na zinazima mwanga wa jua ukizidi kiasi fulani.
 
Inawezekana kuweka mtu wa kuwasha na kuzima lakini hiyo ni kupoteza hela tu kwani utatengeneza ajira pengine hata sio muhimu. Kuna vifaa vinaweza kufungwa ambavyo endapo giza lilajitokeza wakati wowote ule taa hizo zinawena waka pasipo kibarua wala engineer yoyote kwenda kubonyeza chochote...
 
Inategemea ni taa gani.

Mara nyingi taa za barabarani na mjini kwa ujumla (mbele ya majengo) huwa ni mali ya halmashauri ya mji.

Taa hizi huwashwa kwa saa maalumu na kuzimwa saa malumu.

Ndiyo maana miji ya Ulaya, hurudisha saa mbele au nyuma ili kupunguza masaa ya uwashaji taa hasa wakati wa Winter maana masaa ya giza huwa marefu na masaa ya mchana mafupi.

Kuna nchi nilisikia juzijuzi kama sikosei Ireland walikuwa katika kutaka kubadili katiba ili wawe wanarudisha au kupeleka saa mble tofauti na UK kwa siku kadhaa na wakifanya hivyo, wataokoa hela nyingi sana.

Hivyo, katika nchi nyingi, imeandikwa wazi kabisa kuwa, saa zitawashwa saa fulani na kuzimwa saa fulani. Anaweza kuwa anawasha mtu, computer programs nk nk.

Haziwezi kutumia umeme wa jua maana utakuwa hautoshi kuwasha taa zote kwa usiku. Ila kuna maeneo Traffic lights wanatumia umeme wa jua kuendesha taa hizo. Kwa Africa hii kitu inatakiwa na mchana mzima, taa za barabarani zinakuwa za nguvu ya jua.

Wenzetu huwa wana kasheshe sana maana giza refu, barafu inabidi walisafishe au kulimwagia chumvi ili liyeyuke. Ndani ya mabasi na vyombo vingine vya usafiri inabidi wa-heat ili kuwe na joto. Hizo zote, gharama lake kwa halmashauri za mji huwa ni hela za nyingi sana. Ila labda ina uzuri wake maana watu wanajituma kweli ili kujiandaa na WINTER.
 
hizo taa zinakuwa na kitu kinaitwa light dependent resistor (LDR) ambazo resistance yake inafanya kazi kutokana na light intensity. Kwa mfano (LDR nyingine) wakati kunapokuwa na mwanga mwingi (e.g mchana)resistance yake inakuwa kubwa hivyo umeme hauruhusiwi kupita na taa hapo ndipo zinapokuwa off. Na mwanga unapopungua kama mda wa jioni na resistance yake ya electric current inapungua hivyo current inaruhusiwa kupita hapo ndipo unaziona hizo taa zikiwaka automatically.
 
+1 for u sir. Nlikua sijui hii mambo kabisa.
 
ni kweli mkuu ulichoongea kuna hizo LDR lakini kwa uwashaji na uzimaji wa taa hizo za barabaran circuit yake inatumia active component (transistor ingawa nimeisahau jina lake lakini huwa inaoperate kutokana na kias cha mwanga hii transistor ndiyo huhusika na switching action ya taa kufuatana na uwepo wa mwanga.

Ukijaribu kugoogle utapata japo mwanga wa jins inavyo operate.
 
Inategemea na aina gani ya barabara i.e. kuanzia za mtaa mpaka barabara kuu. Teknolojia ziko nyingi na manufacturers wapo wa kila aina............inategemea pia unafuata specifications zipi..........cha msingi lighting level lazima zi-meet minimum requirements za specs husika..........

taa nying za barabarani zinategemea sana na hali halisi ya mwanga........unapokuwa mdogo zinawaka automatic...mambo ya photcell hayo...........power source ziko za aina nyingi......maporomoko ya maji, jua, mafuta, upepo, nuclear, makaa ya mawe nk nk
 
kuna jamaa moja aliniambia kuwa ukichukua tochi ukwamwilika kwenye box ambalo liko hapo ile taa inazima
 
hizo taa zinakuwa na kitu kinaitwa light dependent resistor (LDR) ambazo resistance yake inafanya kazi kutokana na light intensity. Kwa mfano (LDR nyingine) wakati kunapokuwa na mwanga mwingi (e.g mchana)resistance yake inakuwa kubwa hivyo umeme hauruhusiwi kupita na taa hapo ndipo zinapokuwa off. Na mwanga unapopungua kama mda wa jioni na resistance yake ya electric current inapungua hivyo current inaruhusiwa kupita hapo ndipo unaziona hizo taa zikiwaka automatically.

sawa kabisa mkuu...
 
Back
Top Bottom