Sylivia Sebastian ashinda taji la Miss Tanzania 2019

mawaridi

Member
Aug 30, 2015
47
123
Miss Mwanza Sylivia Sebastian, usiku huu wa leo amefanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania baada ya kuwashinda warembo wenzake 19 waliokuwa wanawania taji hilo

Sylivia baada ya kushinda taji la Miss Mwanza, alishiriki na kushinda pia taji la Miss Lake Zone

Kwa ushindi huo, Sylivia amefanikiwa kujipatia zawadi ya sh milioni 10 na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Miss World

67830930_2566714930018123_5659131441059062432_n.jpg

=======

Picha: Sylvia atwaa taji la Miss Tanzania 2019

Hatimaye shindano la kumtafuta mrimbwende atakayevaa taji la Miss Tanzania 2019 limekamilika baada ya jopo la majaji kumchagua Sylvia Sebastian kuwa mshindi, katika tukio lililofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Sylvia ni mhitimu wa kidato cha sita na kwa sasa anasoma kozi ya kompyuta katika Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Mrembo huyo kutoka Mwanza amefanikiwa kupenya katika vipengele vyote ikiwa ni pamoja na uwezo wa kujieleza, ufahamu wa masuala mbalimbali pamoja na jinsi alivyoweza kuutumia uzuri wake wa Kiafrika akiwa jukwaani ndani ya mavazi ya aina tofauti.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo na kushuhudia Sylvia akivishwa taji linalompa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urimbwende ya dunia (Miss World 2019) yatakayofanyika Desemba 14, London, Uingereza.
67440711_583699025496799_962744498710944084_n-1.jpg

Waandaaji wa shindano hilo, kampuni ya The Look wametoa Sh. 10 Milioni kama zawadi kwa Miss Tanzania 2019.

Sylvia amepokea taji hilo kutoka kwa Queen Elizabeth Makune aliyekuwa mshindi mwaka 2018.
 
Miss Mwanza Sylivia Sebastian, usiku huu wa leo amefanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania baada ya kuwashinda warembo wenzake 19 waliokuwa wanawania taji hilo

Sylivia baada ya kushinda taji la Miss Mwanza, alishiriki na kushinda pia taji la Miss Lake Zone

Kwa ushindi huo, Sylivia amefanikiwa kujipatia zawadi ya sh milioni 10 na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Miss World

View attachment 1188671

Picha: Clouds Digital
Duu kumbe haya mashindano bado yapo
 
Kweli maisha yanakwenda kasi sana, yani now days hili shindano limekosa kabisa mvuto ama niseme halipati promo kama pale kitambo.
Yaani hili shindano lilikuwaga kitu kikubwa sana hapa Tanzania, hata uchaguzi mkuu haukuwahi kirindima kama shindano la Miss Tanzania.
Leo hii hata wasafi eti imekuwa kubwa hadi kupita shindano la Miss Tanzania.
 
kiukwelii nimelijua tu jana usiku baada ya kupita maeneo ya kijitonyama
 
Sylvia Sebastian( Kilumanga?,Nyanda?,warioba?,Masanja?,Matimbwa?)
Hapo mabano nasubiri jina lake la ukoo la Kibantu. Anayelifahamu tafadhali.
 
Yote kayataka Siti Mtemvu na kuwadi Lundenga,yaani mimi mwenyewe nimejua jana kulikuwa na miss Tanzania baada ya kuona huu uzi,yaani siku hizi Tukio la Miss Tanzania linazidiwa na event za ajabu ajabu.
 
Back
Top Bottom