Swissport (Dar & Arusha) Imejaa Rushwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swissport (Dar & Arusha) Imejaa Rushwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 27, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,248
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Swissport (Dar & Arusha) Imejaa Rushwa!

  --------------------------------------------------------------------------------

  Ndugu wana JF, kwanza napenda kumpongeza ndugu yangu Temu kwa jinsi anavyozidi kuliimarisha shirika la Swissport.

  Pili nina machache, nakuomba kaka kama una nia na umedhamiria kuibadilisha kampuni yako jaribu kufanya yafuatayo:

  Mosi:

  Rekebisha tabia za hawa wafanyakazi wako hapo wanapoangalia abiria kwanza ya kuondoka, nimesikitika sana jana tu imejirudia tena hali iliontokea mwezi uliopita, nikiwa nimeongeza kilo 4 tu, dada mmoja akaamua kuningangania kwa kuniomba doler 20, nilimwambia kama umeshindwa kunisaidia naomba tu nipunguze mzigo mpaka alipokuja dada mmoja wa airline husika akaamua kumwambia msamehe na ndipo alipoona aibu.

  Pili
  Wawe wasafi kimaumbile wakumbuke pale kila abiria wanapita sehemu tofauti, pia kukiwa na harufu mbaya wanashindwa kuelewa uhali halisi wa kampuni yako,najua si wote jaribu kuwafunza baadhi...wajue jinsi ya kuwa na customer service....

  TATU:
  Waache rushwa, imefika sasa kila mfanyakazi anaonekana yuko pale kwa ajili ya kuomba abiria pesa mzigo unaozidi, sidhani hilo ndilo jukumu lao ila kama unawalipa mshahara mdogo tunakuomba uwalipe mshahara unaostahili kuliko kuaibisha kampuni yako.

  NNE:
  Wawe na heshima mbele ya abiria,kumekuwa na mambo kadhaa na nikiwa kama msafiri ninaepensa kampuni hii, naomba wajitahidi kujua jinsi ya kuishi na abiria na si kuanza kushikana shikana wanaume kwa wanawake mbele ya abiria kweli ni binadamu wanahitaji mambo hayo ila nahisi kuna sehemu husika za kufanya mambo hayo.

  Tano:
  Jaribu kujali wafanyakazi wako ndugu yangu na kaka yangu,,nilijarib kumuuliza yule binti na kujua sababbu za kuishi vile alilalamika sana mshahara mdogo, maisha magumu, hakuna haja ya kuwaumiza wale watoto pale chini,okoa vizazi vichanga kwa kuwalipa sawa na pato unalopata kama umedhamiria kuijulisha dunia umuhimu wa Swissport!

  Sita:
  Hili suala wala sisemi, hata nikiwa kule Kilimanjaro ninajua mchezo wanaofanyiwa watu kupata ajira, kama ni hivyo rekebisha hilo swala maana nina uhakika wa wafanyakazi wako wengi walio na vyeo vikubwa wakiwa na div 4 ama 0 kabisa na majuzi nilisoma kijana mmoja pale Cargo alishtukiwa na div 0 yake ikawa ni aibu tupu kwa kampuni mtu amekaa miaka 6 superv..hapana rekebisha ajira zako mkuu.

  Mwisho nawatakia kila la kheri
   
 2. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2008
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kutokana na vitendo vyao, hawa jamaa wanatia hasara kubwa katika mashirika husika kwa vitendo vyao. Wakati mmoja jamaa zangu walikuwa wanatoka Dar kuja Helsinki kupitia London. Katika kukagua mizigo baada ya ku check-in wakiwa departure lounge, wakaambiwa kuwa bag moja ni kubwa mno haliruhusiwi kuingia kwenye cabin. Kwa kweli, bag hilo lilikuwa dogo, la kawaida tu, kwa hiyo jamaa yangu akawaonyesha backpacks za Wazungu zilizokuwa kubwa ambazo Wazungu hao walikuwa wameruhusiwa. Wakamjibu kwa kejeli kuwa asiwafundishe kazi, kama hataki aache safari. Ikabidi bag hilo liwekwe kwenye baggage compartment, na hata halikuwekwa tag yoyote, kuwa linakwenda wapi na wala kuwa na jina!. Hii ina maana kuwa bag hilo lilishushwa Heathrow. Jamaa yangu kuona mzigo wake hakuupata, akawaambia Brithish Airways kuwa hawezi kuendelea na safari yake kwenda Helsinki bila kujua mzigo wake uko wapi. Ikabidi aahirishe safari yake, atafute mzigo wake (ambao ulipatikana unazunguka kwenye conveyer belt ya mizigo). Ikabidi British Airways wawape hotel ya kulala, pamoja na chakula kwa siku hiyo mpaka watakapopata connection nyingine kesho yake.

  Kile kitendo cha kuwafanyia jeuri jamaa zangu umesababisha BA kugharamia huduma za hotel na chakula, pamoja na kupoteza muda wa jamaa zangu.
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Rushwa ni kweli kabisa. Hiyo nimewahi kusikia mwenye jamaa akiombwa chochote hapa Dar. Hata ukiangalia mambo mengine wanayofanya unaweza kucheka, utakuta wanakuuliza unakwenda wapi na kufanya nini, ukiwaambia unakokwenda wengine hata miji yenyewe hawajui ukiwaambia unaloenda kufanya nalo hata hawaelewi.
  Ukiwa mzungu hasa Dar ni poa sana, ukiwa na excess luggage unaanchwa tu hata kukuuliza unaenda wapi na kufanya nini hawaulizi. Sijui ni nani aliyeweka wafanya kazi hao na system hiyo, kweli ni aibu sana kila ndugu wanaosafiri wakifika wanakokwenda huwa nauliza airport ilikuwaje wanalalamika. Labda siku yao inakuja, maana naona wenye nchi sasa wanarekebisha nchi yao.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,248
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Nakwambia tanzania imejaa aibu tupu hata wazungu wakija unafikiri wanasachiwa na custom..we ahata siku moja waoga!!!linginne wana tabia ya kudanganya bei ya kilo ukiwa unasafiri ili uweze kubagen nao vizuri!!!!
   
Loading...