Swalla ya EID (Iddi) Yatumika KISIASA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swalla ya EID (Iddi) Yatumika KISIASA?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mozze, Sep 10, 2010.

 1. m

  mozze Senior Member

  #1
  Sep 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimejiuliza leo, ni nani na NAMNA gani wahusika wanachagua sehemu ya kufanyia Swala ya EID?
  Nakumbuka Kinana aliwahi kusema Mgombea uraisi wao atarudi Dar kwa ajili ya mapumziko na kushiriki Eid, lakini nimeona Eid kufanyika Tanga.
  Nashawishika kuona kuwa imepangwa huko ili mgombea Urais yw CCM ambaye alikuwa Tanga kwa kampeni aweze kutumia nafasi hiyo kutoa ushawishi wa kisiasa hasa kwa Waislam wenzake.
  Kwa tafsiri yangu huu ni Mchezo mchafu! na Ndugu Waislam wa Tanga TUSIDANGANYIKE!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  kWA HAWA JAMAA muda huu watatumia kila upenyo kuomba ridhaa toka kwa kila kikundi cha kijamii!
  Waangalie mzee asije akajisahau na kutoa ahadi za kujenga misikiti 100 mkoani Tanga!...huh!
   
 3. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  ....na iendelee kuwa ni tafsiri yako na mtazamo wako.
   
 4. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Swala ya Eid kitaifa hufanyika kwa kuzunguka na mara nyingi huangalia upatikanaji wa viongozi wakuu wa kitaifa ili ushiriki wao uweze kuipa swala hii macho ya walio wengi. Na ukweli ni kwamba Kikwete pamoja ya kwamba ni mgombea wa urais BADO pia ni rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa bahati mbaya kwenye mikusanyiko kama hii inayolazimu wanene wa nchi wawepo, kumwalika ndugu Kikwete ni kufuata itifaki.

  Itasikitisha kuona kama waalikwa na waumini watakubali kutumia na kutumika katika Eid kuendesha siasa na hii itakuwa ni kukiuka makubaliano ya maadili ya uchaguzi ambayo vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi walitia saini.
  Kingine pia Tanga siku zote ni ngome imara ya CCM na hili kila mmoja analijua na sasa haingii akilini CCM kutumia sala ya Eid kujinadi Tanga, ikiwa watafanya hivyo.

  Jamani tusikimbilie kulalamika lalamika au kuhisi mchezo mbaya kila wakati hii huonesha kutokujiamini kwetu.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Hapa Kenya kibaki kaamua kuifunika sikukuu na kuwaambia wafanyakazi waendelee na kazi, in short hapa si mapumziko wala nini, kesho eid pili ndo sikukuu ya kitaifa na j3 watu wanakwenda maoficini kama kawa!
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  wewe ulitaka ifanyike wapi..?!!
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hata Lindi ingekuwa safi tu
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  .
  Nani asiyefahamu kwamba BAKWATA ni kitengo cha propaganda cha ccm toka enzi na enzi? Bakwata itawaburuza waislamu wa Tz hata mwisho wa siku kama ccm itaendelea kuwa madarakani. Ni njia pekee ya waislamu huru kujinasua na Bakwata ni kuiondoa ccm madarakani.
  Wasipofanya hivyo wasitarajie hata siku moja kuwa na maamuzi huru.
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Wangeifanyia Karatu au Tarime :lol::eek2::eyebrows:
   
 10. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  kwani kufanyika TANGA kuna makosa gani.. si ni mkoa pia wenye waislam wengi
   
 11. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hivi unafahamu ya kwamba Bakwata hakuna uanachama, na pia si lazima wa kila mwislamu kufuata kile ambacho Bakwata wanafanya au shauri? Bado sijajua wala ona uhusiano kati ya Bakwata na uhuru wa waislamu Tanzania kama unavyoainisha katika ujumbe wako hapo juu. Migogango baina ya baraza hili na waumini wa Kiislamu inaeleweka na kwa uelewa wangu haijawa ya kisiasa kama vile ilivyo migongano yoyote ile ambayo hutokea baina na watu na makundi mbalimbali.
  Hivi majuzi hapa tulipokuwa tunajadili sakata la TUCTA na serikali, lilikuja tishio la kura za wafanyakazi na kuna bwana mmoja alifafanua wazi ya kuwa "Tanzania hakuna kura za makundi", na hivi ndivyo naamini pia hata kwa Waislamu ndio jinsi ilivyo.
  Kura ya mtanzania inapigwa kwa kuangalia ni nani atatetea vyema maslahi ya mpiga kura huyo na si nani atatetea maslahi ya vikundi mbalimbali. Leo hii Tanzania sidhani kama Bakwata wana uwezo wa kushinikiza waislamu wakipigie kura chama chochote kile kwa sababu yeyote ile.

  Tukirudi katika mada, hili swala la Eid kuswaliwa kitaifa Tanga, Lindi, Mara, Kigoma, Dar au kwingineko kokote kule ni vyema lisichukuliwe kisiasa. Hii ni sikukuu ya kidini na ni vyema watu wakaachiwa wapumzike na sio kuletewa kero za siasa.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kama ndivyo kwa nini Bakwata ndio hutangaza siku na mahala pa sala ya Idd Kitaifa. Hawa Bakwata ni nani na nani kawapa mamlaka ya kufanya hivyo kwa waumini wote wa Tanzania!
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Apige kampeni Msikitini au Makanisani mwaka huu...kazi anayo, kuna wengine nimeona wanatumia mpaka miariko ya mahafari kulazimisha kugeuza kampeni...kawa ahadi nini?
   
 14. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #14
  Sep 10, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sala hapa kuwa kufanyika tanga ni makosa, hapana ni sikuku ya idd kugeuzwa kuwa kampeni za kisiasa za ccm,
  ebo kumbe una mtazamo finyu namna hiyo? kufanyika tanga sikukuu imemfuata kikwete hilo halina halina ubishi
   
 15. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  wabongo tunalalamikia kila kitu, du

  malalamishi mengine hayana msingi jamani

  JK ni Raisi aliyepo madarakani hivyo angealikwa hata kama ingekuwa wapi, labda yeye kama angeweza kumtuma mtu.
   
 16. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kwa taarifa yenu tu, Mzee Mwinyi ndio mgeni rasmi baraza la Eid,-- soma michuzi/jiachie blog na sio JK. Nakubaliana na wanaosema kuna agenda ya kisiasa kwenye suala zima. Kama JK angekuwa mgeni rasmi baraza la Eid, ningeelewa, lakini nina uhakika amekwenda kuswali kama muislamu wa kawaida na kupiga kampeni kidogo then ataishia kuendelea na kampeni zake. Kumbuka anakaa ikulu akiwa Tanga, na kwa kuwa viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu wako tanga, who knows ni wangapi watapigana vikumbo kwenda ikulu kuonana na mzee? People, think outside the box!!!
   
 17. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  wewe ndo unamtazamo finyu! nafikiri hii ni nchi huru .. mtu anasali mkoa wowote anaojisikia! .. sasa wewe ulitaka tanga kusiwe na sala ya ead AU? hata hivyo tanga inagawanyika kwa kura za CCM & CUF ... chadema hawana chao kule.
   
Loading...