Swali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Mar 21, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kuna swali limekuwa lina niumiza kichwa kidogo japo si sana. Hivi karibuni kumeibuka tena mijadala kuhusu muungano, Zanzibar na mustakabali wa taifa letu.

  Katika kupitia majibu kwa ju juu (siyo utafiti rasmi) inaonyesha kwamba wengi wetu (walau Watanganyika) wao wana taka aidha ya haya mawili 1)Serikali tatu au 2) Kuvunja muungano.

  Kusema ukweli mimi nakubaliana na wengi. Option yangu ya kwanza ingekuwa serikali tatu ila hata inge bidi kuvunja muungano ni bora kuliko yanayo endelea sasa. Maana baada ya hapo Wazanzibar hawata kuwa na "The Tanganyika/Nyerere Excuse".

  Ila kwa leo nataka tuchambue serikali tatu. Katika serikali tatu kuta kuwa na options mbili kwa maoni yangu:
  1)Serikali za Tanganyika na Zanzibar kupewa nguvu kubwa za kujiamulia na serkali ya URT (United Republic of Tanzania) kuwa na nguvu ndogo na kushughulikia mambo kama foreign affairs, jeshi nk.

  2)Serikali ya URT kuwa na nguvu zaidi na kuamu ni mambo gani serikali za hizi nchi zitaachiwa.

  3) Kugawa nguvu nusu kwa nusu (in theory) kwa serikali za Tanganyika na Zanzibar na serikali ya URT. Kwa maana hiyo serikali zote zina kuwa kama check kwenye hizo nyingine.

  Nadhani options zote zita hitaji debate kubwa maana tuki chagua chaguo lisilo basi ni maumivu tena.
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kinachokera watu wasiozidi 1ml wanalalama kuzidi watu karibu ya 40 ml. ili hali ukiuangalia muungani ni kwa faida ya wazanzibar socially and economically. Bora kuvunja ili tuone watamlalamikia nani.
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwa maoni yangu mimi nadhani the best option ita kuwa namba tatu. Kwa sababu mimi naona kuinyima nguvu serikali ya muungano ita leta matatizo na itaondoa maana halisi ya muungano. Unless kama lengo tokea mwanzo ni kuandaa nchi hizi mbili kuji tenga kwa maana serikali ya muungano isiyo na meno haiwezi linda muungano.

  Option namba mbili nayo ina matatizo yake. Kuzipa serikali za mataifa haya mawili (Tanganyika na Zanzibar) nguvu zaidi kuta kufanya nchi hizi mbili ziangalie tu interest zao na kuacha kabisa kufanya maamuzi yenye manufaa kwa Tanzania.

  Option ya tatu ita hakikisha serikali za mataifa haya mawili haziuwi muungano ila pia ita hakikisha serikali ya muungano nayo hai kandamizi maoni na matakwa ya watu wa mataifa haya mawili.
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Trust me Wazanzibar hawa taki kujitenga mkuu. Wange taka wangesha jitenga. Ndiyo maana kila siku wao hulalamika kwa nini Tanganyika hatu vunji muungano ili hali wanajua kabisa hakuna serikali ya Tanganyika na ni wao wanao dai sana muungano uvunjwe. Tatizo waki tishia nyau kidogo tu URT ina fyata. Kuna hitajika kiongozi ambae hata ruhusu utoto na kuamua Zanzibar waamue mmoja....kubaki au kutoka.
   
 5. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Serikali moja inatosha. Itapunguza administrative costs kwa kiasi.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mi nadhan umefika wakati wa kuuvunja muungano. Hakuna sababu ya kuendelea na muungano wenye manung'uniko, tena yanatoka kwa wanaoufaidi! Zanzibar yenye wakazi wasiozidi nusu ya watu wa dar ina wabunge 50 na Dar inao 8. Wote wanalipwa na serikali ya muungano. Wapo wabunge kila mtaa na ndio maana kuna mbunge aliyeshinda kwa kura 800! Mi nadhani wametunyonya vya kutosha na sasa ifike mwisho!
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Contrary to popular belief serikali tatu siyo lazima iwe gharama kubwa. Tuna weza kuwa na serikali tatu kwa gharama ile ile ya serikali mbili au hata moja. Vitu vinavyo kuza gharamza za serikali ni:
  1. Malipo ya viongozi na marupurupu yao
  2.Ukubwa wa bureaucracy
  3.Idadi ya viongozi nk.

  Tuki taka kupunguza gharama tuna weza. Kwani hata sasa tuna fuja pesa kiasi gani mkuu? Serikali ya muungano yenyewe ina mawaziri na manaibu waziri karibia 60. Hao manaibu hawa fanyi kazi yoyote ya maana administratively zaidi ya kuwa nafasi za fadhila tu.
   
 8. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Muundo wa serikali mbili achilia mbali matatizo ya kimuondo ambayo yalikuwa yanapata nguvu kutokana na nguvu za ushawishi za Mwalimu Nyerere, mazingira ya sasa sio muafaka kabisa kwa Muundo huu.

  Chukulia kwamba 2015 Chadema wanashinda kiti cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano na tayari wao wanaona kwamba swala la CUF na CCM kushirikiana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa sasa sio sahihi, Msimamo huu wa chadema umewagusa sana wazanzibar mpaka damuni. JE unadhani serikali watakayounda itakubalika itakuwaje? kumbuka watakazimika kufanya kazi na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (ambayo mpaka sasa wote tunajua kwamba by 2015 itaongozwa na ama CCM au CUF au itakuwa ya mseto kwa mara nyingine).

  Watanzania wanatakuwa kutambua kwamba mabadiliko ya kisiasa na kimaendeleo (hasa vichwani) ambayo tumeyafikia sasa, kama walivyokubali kutengeneza katiba mpya swala la muungano ni lazima lipewe nafasi ya msingi sana na Kama watakuwa wakweli Muungano huu hauwezi kubaki kama ulivyo.
  Lazima ama tuwe na serikali moja,tatu au muungano uvunjike.

  Wazanzibar wanatakiwa pia wakweli kutoka moyoni mwao kwamba kama Muungano huu utavunjika wataweza kubaki wamoja? Hii ni moja ya hofu aliyokuwa nayo Mwalimu juu ya Zanzibar, aliwafahamu vizuri sana wapemba na waunguja, alijua hakika wakiachwa wenyewe hawawezi kuwa na msimamo wa kusema SISI ni Wamoja, ushahidi ni UCUF na UCCM Uliotamaraki huko.

  Hivyo kwa kweli kabisa zinahitajika busara za hali ya juu sana, na kwa sasa jukumu hilo liko mikononi mwa CHADEMA. Kama itawezekana CHADEMA wareview msimamo wao juu ya siasa za Zanzibar, na wakubali kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama wanavyosema wao wanzibar ni jibu kwa mstakabari mwema wa siasa za zanzibar, waende mbele zaidi ni kuwatambua CUF kama wapinzani wa kweli kabisa wa chama cha mapinduzi (Kote Bara na Visiwani) na kwa vitendo waanze mara moja kushirikiana nao katika michakato yote ya siasa za kipinzani yanayohitaji ushirikano wao kisha KWA MANUFAA YA PEMBA NA UNGUJA WAJIANDAE KUONGOZA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA CHINI YA MUUNDO WA SERIKALI MBILI (Kama ilivyo sasa). Na zaidi ya yote waanze mara moja kuwaeleza watanganyika kukubaliana na Muundo huo (hata kwa gear ya kumuenze baba wa Taifa).
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Taifa_Kwanza nakubaliana na wewe.
   
 10. U

  Uswe JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  we utakua mwanafalsafa mwingine sio yule ef ei el es ef ei ukipenda anasa za showtime niite sey sey....bse we una kigugumizi sana wakati yule anaongea kama cherehani
   
 11. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mimi ningependelea serikali moja ili kupunguza gharama za uwendeshaji, ila najua hili halitawezekana kamwe la Muungano kuvunjika. Nitakubaliana na serikali 3, ila URT itakuwa inahusika na mambo ya msingi ya Muungano na wizara husika za mambo hayo, halafu yale yasiyokuwepo kwenye muungano basi kila upande utajazia wizara zake. Bado pia nataka kuyajua mambo ya msingi ya Muungano yalio hai leo na uiano wake, unajua nimevurugikiwa zaidi pale baraza la uwakilishi lilipodai kuwa swala la mafuta yanayosemekana yapo Zanzibar siyo swala la Muungano. Je rasilimali za bara inakuwaje? Inabidi tutakapoiandika Katiba yetu mpya tuwe bayana kuyaainisha mambo yatakayohusika kwenye Muungano na jinsi ya kuendesha ushirika huo.
   
 12. M

  Matarese JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hapa hakuna cha busara wala nn, kila mtu achukue chake aishie, enough is enough!
   
 13. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  serikali moja ina shida gani? Kwa nini nchi moja inakuwa na serikali mbili? Umeona wapi hiyo? Marais wawili? bunge mbili? Mahakama mbili? ivi hii ni nini? Mie nashindwa kuelewa hapo!!
   
 14. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mhh....i beg to differ. Ivi unadhani pesa serikalini inatumika kwenye hivyo vitatu tu? Kuna pesa za kuendesha wizara. Kwa mfano serikali 3, will mostly mean at least wizara mbili mbili.
  Swali lingine ninalojiuliza....kwa nini tunalinda Muungano. Kwa nini tusiache freedom of self determination?
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Wazanzibar katu hawatakubali kujitenga kwani wanajua wanachofaidi.
  Wataishia kulalamikia mambo flaniflani ili wapewe ofa zaidi.

  Nataka tuwe na tanganyika ili kila mtu ajiendeshe kivyake.
   
 16. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,674
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  I think we need to make it clear!We want Tanganyika back,we don't care how i.e three govts or two countries,period.
   
Loading...