Swali rahisi lakini...(b)

yeah, mtririko naukubali mpaka mwisho.. Lakini muhudumu aliporudi chumba no. 1, alimchukua m2 kwanza au wa pili akampeleka chumba no. 12! Still muhudumu hakumgusa mtu wa 13 so hakuweza kumpa chumba mtu wa 13, alikuwa anacheza tu na wale wa2 12 na vyumba 12 tu!
Makofi mfulululululililizo,bravo mkuu!
 
kinacho tokea hapa ni kwamba mtu wa 13 hatujaambiwa yupo wapi so hawakua 13 ila 12
 
kinacho tokea hapa ni kwamba mtu wa 13 hatujaambiwa yupo wapi so hawakua 13 ila 12
Mtu wa 13 alikuwa pamoja na wenzie 12 ila hakuguswa kabisa katika suala la kupangiwa chumba!
 
2+10 = 12 sio 13 coz chumba namba moja wawili, vyumba vinabaki 11 akaweka watu 10 kwenye hivyo vyumba hadi chumba namba 11 that is 1 + 10 kinabaki kimoja anamuweka yule aliyemuweka kwenye chumba namba moja watu 12, still mmja anamiss unataka au hutaki!!!
 
1&2 - 1
3 - 2
4 - 3
5 - 4
6 - 5
7 - 6
8 - 7
9 - 8
10 - 9
11 - 10
12 - 11
Kisha anamchukua mmoja toka chumba namba 1 anampeleka namba 12
Mtu wa13 hajachukuliwa kupangiwa chumba labda utuambie sasa
 
Masuke,toghocho,fredmlay na P wa ukweli majibu yenu ni sahihi na ni wazi swali mmelielewa!
 
Watu 13 walifika kwenye guest house yenye vyumba 12 tu na kila mmoja alitaka chumba chake peke yake.Mhudumu alimpatia kila mmoja chumba.Alimchukua mtu wa 1 na wa 2 akawaweka chumba # 1.mtu wa 3 chumba #2,mtu wa 4 chumba #3,mtu wa 5 chumba # 4,mtu wa 6 chumba # 5,mtu wa 7 chumba # 6,mtu wa 8 chumba # 7,mtu wa 9 chumba #8,mtu wa 10 chumba # 9,mtu wa 11 chumba #10 na mtu wa 12 chumba # 11.Baada ya hapo alirudi chumba # 1 aliko waacha mtu wa 1 na wa 2,akamchukua mmoja akampeleka chumba #12.Elezea,mhudumu aliwezaje kumpa kila mmoja chumba chake peke yake?

Bado mtu wa 13 hajapewa chumba.
 
Watu 13 walifika kwenye guest house yenye vyumba 12 tu na kila mmoja alitaka chumba chake peke yake.

elezea,mhudumu aliwezaje kumpa kila mmoja chumba chake peke yake?

Mtu wa 13 alikuwa pamoja na wenzie 12 ila hakuguswa kabisa katika suala la kupangiwa chumba!

Sasa kama hakuguswa mhudumu alifanikiwaje kuwapa kila mmoja na chumba chake?... Nikirecall swali linatuhitaji tuelezee namna ambavyo mhudumu aliweza kugawa vyumba 12 kwa watu 13 na kila mmoja apate chumba chake mwenyewe.. Endapo kama mtu wa 13 hakuguswa, jibu ni kwamba mhudumu alishindwa...
 
Mtu akikwambia 1/0=0,sio lazima kuforge njia ili jibu lako lifanane na lake,kama haiwezekani sema haiwezekani kutokana na sababu hii na ile.katika swali hili,mimi mtoa swali nimevuruga mpangilio wa ugawaji vyumba kwa makusudi na kuonyesha kila mtu kapata chumba.Kimahesabu hili suala haiwezekani kabisa.Wewe ulitakiwa ugundue uongo wangu uko wapi,ugundue jinsi nilivyomtumia mtu mmoja kama mtu wa pili na baadaye kama mtu wa 13,ni hilo tu mkuu!
 
Mtu wa 13 alimpeleka wapi?!!!!

watu 13 walifika kwenye guest house yenye vyumba 12 tu na kila mmoja alitaka chumba chake peke yake.mhudumu alimpatia kila mmoja chumba.alimchukua mtu wa 1 na wa 2 akawaweka chumba # 1.mtu wa 3 chumba #2,mtu wa 4 chumba #3,mtu wa 5 chumba # 4,mtu wa 6 chumba # 5,mtu wa 7 chumba # 6,mtu wa 8 chumba # 7,mtu wa 9 chumba #8,mtu wa 10 chumba # 9,mtu wa 11 chumba #10 na mtu wa 12 chumba # 11.baada ya hapo alirudi chumba # 1 aliko waacha mtu wa 1 na wa 2,akamchukua mmoja akampeleka chumba #12.elezea,mhudumu aliwezaje kumpa kila mmoja chumba chake peke yake?
 
wako ww hakuwa uongo bali ujinga na kupotezeana muda.

masuali kama haya hapa si pahali pake
 
wako ww hakuwa uongo bali ujinga na kupotezeana muda.

masuali kama haya hapa si pahali pake
Hapa ni pahala pake ila ni kwa ajili ya wale wenye uelewa tu,na walio elewa hawakupoteza muda kutoa jibu.Asiyeelewa haelewi tu na huwezi kumbadilisha na kwa sababu haelewi kinachoendelea katika swali,hilo swali litakuwa ni ujinga kwake!
 
Ndugu,fuatilia mtiririko,mgao uliishia kwa mtu wa 12 kupewa chumba namba 11.Lakini kumbuka chumba namba moja aliacha watu wawili,akamchukua mtu mmoja tu kati ya wale wawili na kumfanya mtu wa 13 na akaenda kumpa chumba namba 12.

mtu wa 13 hajapata chumba mkuu kwani chumba #1 waliingia tu wa 1 na wa 2 then akaenedelea na wa 3 mpaka wa 12, kwa hiyo mtu wa kumi na tatu hajapata chumba
 
Watu 13 walifika kwenye guest house yenye vyumba 12 tu na kila mmoja alitaka chumba chake peke yake.Mhudumu alimpatia kila mmoja chumba.Alimchukua mtu wa 1 na wa 2 akawaweka chumba # 1.mtu wa 3 chumba #2,mtu wa 4 chumba #3,mtu wa 5 chumba # 4,mtu wa 6 chumba # 5,mtu wa 7 chumba # 6,mtu wa 8 chumba # 7,mtu wa 9 chumba #8,mtu wa 10 chumba # 9,mtu wa 11 chumba #10 na mtu wa 12 chumba # 11.Baada ya hapo alirudi chumba # 1 aliko waacha mtu wa 1 na wa 2,akamchukua mmoja akampeleka chumba #12.Elezea,mhudumu aliwezaje kumpa kila mmoja chumba chake peke yake?

Jibu ni kwamba mtu wa 13 hakupewa chumba yaani baada ya mtu wa 12 kupewa chumba #11 mtu wa 13 aliyebaki hakupewa chumba #12 kilichobaki na badala yake akapewa mmoja kati ya wale wawili wa chumba #1 na hivyo mtu wa 13 hakupata chumba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom