Swali rahisi lakini...(b) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali rahisi lakini...(b)

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Jaguar, May 8, 2011.

 1. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watu 13 walifika kwenye guest house yenye vyumba 12 tu na kila mmoja alitaka chumba chake peke yake.Mhudumu alimpatia kila mmoja chumba.Alimchukua mtu wa 1 na wa 2 akawaweka chumba # 1.mtu wa 3 chumba #2,mtu wa 4 chumba #3,mtu wa 5 chumba # 4,mtu wa 6 chumba # 5,mtu wa 7 chumba # 6,mtu wa 8 chumba # 7,mtu wa 9 chumba #8,mtu wa 10 chumba # 9,mtu wa 11 chumba #10 na mtu wa 12 chumba # 11.Baada ya hapo alirudi chumba # 1 aliko waacha mtu wa 1 na wa 2,akamchukua mmoja akampeleka chumba #12.Elezea,mhudumu aliwezaje kumpa kila mmoja chumba chake peke yake?
   
 2. M

  Mr D47 Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado mmoja anabaki
   
 3. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu fuatilia vizuri mtiririko mpaka mwisho,kila mmoja kapata chumba!
   
 4. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  na mtu wa 13 chumba namba.............?
   
 5. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndugu,fuatilia mtiririko,mgao uliishia kwa mtu wa 12 kupewa chumba namba 11.Lakini kumbuka chumba namba moja aliacha watu wawili,akamchukua mtu mmoja tu kati ya wale wawili na kumfanya mtu wa 13 na akaenda kumpa chumba namba 12.
   
 6. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Mmoja alikuwa mjamzito.
   
 7. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ahahahaah!mkuu umenichekesha kweli japokuwa jibu si sahihi!
   
 8. M

  Masuke JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mkuu ukweli ni kwamba kuna mtu mmoja anabaki, maana umeanza mtu wa 1 na mtu wa 2, hapo ni watu wawili lakini pia mtiririko wako umeanzia mtu wa 3 hadi wa 12, ukifanya kama darasa la kwanza tulilosoma sisi la kutumia vihesabio mtu wa tatu hadi wa 12 hao ni watu 10, ukijumlisha na wawili wa mwanzo unapata 12, hivyo anabaki mmoja kutoka kwenye jumla yao ya watu 13, hivyo mtu wa 13 hajapata chumba bado, mwambie mhudumu ajipange amulaze hata mapokezi.
   
 9. M

  Masuke JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  hapo umepata jibu sema tu mtoa swali hajataka kukubali.
   
 10. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unasema kuna mtu mmoja kabaki,unatakiwa uelezee kabaki wapi na kwa jinsi gani amebaki ili tumpe chumba chake,suala si plus and minus pekee,tegua mtego ulipo!
   
 11. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #11
  May 8, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Mtu wa kuminatatu (13) kaevaporate?..
   
 12. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #12
  May 8, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  By the way under 'ceteris peribus' haiwezekani kugawa vyumba 12 kwa watu 13 halafu kila mtu akapata chumba chake....
  Unless, the 13th person alikua haitaji chumba!
   
 13. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hata mimi najua haiwezekani,lakini fuatilia mtiririko utuambie mtu wa 13 tumemsahau wapi na kwa jinsi gani,hilo ndo swali bandugu zangu.
   
 14. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama vp nikupe mji ili utaje jibu sahihi!Nenda PALESTINA
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  May 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Huo mtego sijaubaini lakini lazima huyo mmoja atabaki tu!
   
 16. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Katu mi siendi PALESTINA!
   
 17. P

  P wa ukweli Member

  #17
  May 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yeah, mtririko naukubali mpaka mwisho.. Lakini muhudumu aliporudi chumba no. 1, alimchukua m2 kwanza au wa pili akampeleka chumba no. 12! Still muhudumu hakumgusa mtu wa 13 so hakuweza kumpa chumba mtu wa 13, alikuwa anacheza tu na wale wa2 12 na vyumba 12 tu!
   
 18. M

  Masuke JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Naona mzee tu hutaki kunipa maksi pamoja na kuelezea kote huko bado tu hujaridhika, wewe ungekuwa mhadhiri hamna mtu angekuwa anapata A au B+ kwenye somo lako.
   
 19. Mzee Dogo

  Mzee Dogo JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Aaah, basi mtu wa 13 ni mhudumu-
   
 20. M

  Masuke JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mtego ulipo ni pale huyo mhudumu alivyoanza na watu wawili kuwaweka chumba kimoja, halafu akaenda mpaka mtu wa 12 bila kumgusa mtu wa 13, na akajifanya mtu wa 13 yupo miongoni mwa wale wawili wa kwanza kitu ambacho sio, wale wawili wa mwanzo ni mtu wa kwanza na wapili, hivyo wa 13 bado hajapata chumba, kama mhudumu amekataa kumpeleka mapokezi mwambie awambie wabebane.
   
Loading...