Swali: Muhongo kuielekeza EWURA ni sahihi wakati haiko chini ya wizara yake?

abagabo

Senior Member
Jun 4, 2014
152
225
EWURA haiko chini ya wizara ya nishati na madini, Bali ipo chini ya wizara ya maji na umwagiliaji.

TANESCO ndo ipo chini ya wizara ya nishati na madini. Je, kama ewura imekubali ombi la TANESCO la kupandisha umeme hata kama Muhongo hakuwa na taarifa, ni sahihi Muhongo kuwaandikia barua ya katazo badala ya kuwa andikia barua hiyohiyo TANESCO akiwataka wasitekeleze ongezeko hilo?

Lakini je, mbona hakuwa cc wizara ya MAJI, ambao ndo bosi wa EWURA?
 
uajekundu

JF-Expert Member
Jan 14, 2016
541
500
Kisheria Waziri mwenye mammals na Ewura ni waziri Wa Maji na Muhongo hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya mdhibiti..he was suppose to send it to TANESCO.. Kisheria amekosea ila Kwa sababu nchi hii sikuizi inaendeahwa Kwa woga Wa matamko, acha niangalie muvi inayoendelea
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,945
2,000
Tunachotaka ni gharama za Umeme ZISIPANDE.

Sasa kama EWURA ipo chini ya Wizara ya Kilimo au sijui Wizara gani...it has nothing to do with us.!!!

Gharama za umeme zisipande na kwa hatua ambayo Prof Muhongo umechukua mpaka sasa tunashukuru.

Lazima Waziri wa Nishati usimamie lile tamko lako kwamba umeme hautopanda bei.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,359
2,000
Sheria ya umeme ya mwaka 2008 inamtaja waziri na katika sheria hiyo waziri husika ametafsiriwa ni waziri anaehusika/mwenye dhamana na maswala ya umeme.

Hata hivyo,katika sheria hiyo,ukisoma section inayohusu power of the minister,sheria haitamki moja kwa moja kumpa waziri mamlaka ya kubadili au kufuta maamuzi ya EWURA.
 
abagabo

Senior Member
Jun 4, 2014
152
225
kwa hiyo ww mkuu unataka umeme upande? hapa nashindwa kuelewa kabisa,baada ya tangazo kupanda umeme watu walianza kumlaumu waziri kachukua hatua bado tu mnalalamika tu. mnataka nini sasa?
Mkuu thesym naomba unielewe, hapa natafuta mamlaka aliyonayo Muhongo kwa ewura. Siungi mkono upandishaji gharama za umeme. Je, ikiwa ewura watakomaa, Muhongo analo LA kufanya? Kumbuka tanesco mpaka sasa haijapata maelekezo yoyote kutoka kwa Muhongo
 
milangomitatu

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,484
2,000
Hivi una survive vipi duniani na IQ ya kiwango hiki?
Wewe ndo una akili ndogo hujui chochote kisheria Muhongo hana mamlaka hayo Ewura ipo chini ya wizara ya maji na hata hiyo barua Tanesco hawajakopiwa wakati wao ndo wahusika wakuu
 
abagabo

Senior Member
Jun 4, 2014
152
225
Hivi una survive vipi duniani na IQ ya kiwango hiki?
Kitu gani hukukielewa? Swali ni je, Waziri WA nishati na madini anayo mamlaka ya kutengua maazimio ya ewura iliyo chini ya wizara ya MAJI? KAZI za tanesco au niseme Muhongo zinadhibitiwa na ewura, iweje mdhibitiwa amuelekeze mdhibiti?
 
mzee wa mazabe

JF-Expert Member
May 10, 2016
839
1,000
EWURA haiko chini ya wizara ya nishati na madini, Bali ipo chini ya wizara ya maji na umwagiliaji.

TANESCO ndo ipo chini ya wizara ya nishati na madini. Je, kama ewura imekubali ombi la TANESCO la kupandisha umeme hata kama Muhongo hakuwa na taarifa, ni sahihi Muhongo kuwaandikia barua ya katazo badala ya kuwa andikia barua hiyohiyo TANESCO akiwataka wasitekeleze ongezeko hilo?

Lakini je, mbona hakuwa cc wizara ya MAJI, ambao ndo bosi wa EWURA?
Hoja yako sio kweli,EWURA maana yake ni Energy and Water Regulatory Authority kwahiyo kwenye yoyote inayohusu Energy waziri wa Nishati na Madini ndio boss lakini kenye issue yoyote itakayohusu Maji boss wake ni Waziri wa Maji hata pale EWURA kuna Mkurugenzi Mkuu anaeteuliwa na Rais alafu kuna mkurugezi wa mambo ya Maji na Mkurugenzi anahusika na Nishati zote
 
Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,558
2,000
Ewura haiko chini ya wizara ya nishati na madini, Bali IPO chini ya wizara ya MAJI na umwagiliaji. Tanesco ndo IPO chini ya wizara ya nishati na madini. Je, kama ewura imekubali ombi LA tanesco LA kupandisha umeme hata kama Muhongo hakuwa na taarifa, ni sahihi Muhongo kuwaandikia barua ya katazo badala ya kuwa andikia barua hiyohiyo tanesco akiwataka wasitekeleze ongezeko hilo? Lakini je, mbona hakuwa cc wizara ya MAJI, ambao ndo bosi WA ewura?
Sasa kama EWURA iko chini ya wizara ya maji na umwagiliaji iliendaje wizara ya nishati na madini kuwapandishia bei ya umeme? Kwa nini EWURA ilienda TANESCO ambako hakuko chini ya wizara yao? Huoni kuwa umekosea logic yako hiyo unayotaka watu wakuamini? Yaani nani kati ya wizara hizo mbili imemuingilia mwenzake? Kwa nini usiseme kwamba wizara ya maji iliwaingilia wizara ya nishati kupitia idara yao ya ewura kwa kupandisha bei ya umeme wa tanesco ya wizara ya nishati?
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
11,590
2,000
Ewura haiko chini ya wizara ya nishati na madini, Bali IPO chini ya wizara ya MAJI na umwagiliaji. Tanesco ndo IPO chini ya wizara ya nishati na madini. Je, kama ewura imekubali ombi LA tanesco LA kupandisha umeme hata kama Muhongo hakuwa na taarifa, ni sahihi Muhongo kuwaandikia barua ya katazo badala ya kuwa andikia barua hiyohiyo tanesco akiwataka wasitekeleze ongezeko hilo? Lakini je, mbona hakuwa cc wizara ya MAJI, ambao ndo bosi WA ewura?
Energy and Water Utilities Regulatory Authority- EWURA

Energy - Tanesco

EWURA imeundwa kwa sheria iitwayo EWURA Act.

Hii bodi inawajibika moja kwa moja na wizara za Nishati na Madini, Wizara ya Maji na Ofisi ya waziri mkuu (Mazingira).

Pia inafanya kazi na Tanesco pamoja na TPDC.

Mwenyekiti wa bodi anateuliwa na raisi na wajumbe wa bodi wanatoka sehemu nilizotaja hapo juu.

Kwenye Utawala kuna mkurugenzi mkuu ambae anateuliwa na mawaziri husika.

Ukiangalia kazi za bodi hii kuna sehemu katika sheria ya EWURA Act inaitaka bodi hii kupata mawazo ya waziri husika wa sekta husika kma ya umeme kabla ya kutoa taarifa za kupandisha au kupunguza gharama.

Hivyo kila waziri wa sekta husika anapaswa kuombwa mawazo yake, bila kurukwa.
 
Kidogo chetu

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
1,428
2,000
Hoja yako sio kweli,EWURA maana yake ni Energy and Water Regulatory Authority kwahiyo kwenye yoyote inayohusu Energy waziri wa Nishati na Madini ndio boss lakini kenye issue yoyote itakayohusu Maji boss wake ni Waziri wa Maji hata pale EWURA kuna Mkurugenzi Mkuu anaeteuliwa na Rais alafu kuna mkurugezi wa mambo ya Maji na Mkurugenzi anahusika na Nishati zote
umenena vema mkuu ewura hapa walikuwa wanadili na energy yaani umeme na mwenye dhamana ni wazri wa nishati
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
11,590
2,000
Kisheria Waziri mwenye mammals na Ewura ni waziri Wa Maji na Muhongo hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya mdhibiti..he was suppose to send it to TANESCO.. Kisheria amekosea ila Kwa sababu nchi hii sikuizi inaendeahwa Kwa woga Wa matamko, acha niangalie muvi inayoendelea
Mkuu uloyasema si kweli.

EWURA inawajibika kwa wizara zote za Maji na ile ya Madini na Nishati.

Ndiyo maana yaitwa Energy and Water Regulatory Authority- mamlaka ya udhibiti nishati na maji.

Nishati = Wizara ya Madini na Nishati = Tanesco

Maji = Wizara ya Maji.
 
Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
kwa hiyo ww mkuu unataka umeme upande? hapa nashindwa kuelewa kabisa,baada ya tangazo kupanda umeme watu walianza kumlaumu waziri kachukua hatua bado tu mnalalamika tu. mnataka nini sasa?
Unajifanya hujamuelewa?
 
moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,323
2,000
Kama tanesco ndiyo ilipendekeza bei mpya kwa ewura,,,ina maana kulikuwa na mawasiliano katiya tanesco (ambayo ipo chini ya waziri wa nishati)
Kama tanesco iliweza kufanya mawasiliano na ewura iweje waziri wa nishati ashindwe kuwasiliana na ewura kwa jambo lilelile?
Kumbuka apa waziri wa nishati kasimamisha jambo lililopendekezwa na chombo(tanesco)toka wizara yake.

Mkuu thesym naomba unielewe, hapa natafuta mamlaka aliyonayo Muhongo kwa ewura. Siungi mkono upandishaji gharama za umeme. Je, ikiwa ewura watakomaa, Muhongo analo LA kufanya? Kumbuka tanesco mpaka sasa haijapata maelekezo yoyote kutoka kwa Muhongo
 
WILE

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
4,062
2,000
Wewe ndo una akili ndogo hujui chochote kisheria Muhongo hana mamlaka hayo Ewura ipo chini ya wizara ya maji na hata hiyo barua Tanesco hawajakopiwa wakati wao ndo wahusika wakuu
Common sense tu. Unadhani Waziri wa Maji mambo ya Tanesco yanamhusu?
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,773
2,000
ujuaji mwingine jamani uwe na kikomo...tamanio la mlalahoi juu ya ongezeko la bei ya umeme lilikuwa nini?.. kwani alivyotoa katazo muhongo kuna watu waliopata cholera... mbona tumezidi kujifanya tunajua sana kila kitu? labda we mleta uzi lengo ilikuwa nini juu ya ulichoandika labda utuambie huenda hatujakuelewa
 
milangomitatu

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,484
2,000
Common sense tu. Unadhani Waziri wa Maji mambo ya Tanesco yanamhusu?
Sasa ndo maana nkakwambia una akili ndogo sana na hujui kitu Muhongo alitakiwa kumuandikia Barua Tanesco sababu ndo ipo chini yake na si ewura sababu ewura wapo chini ya wizara ya maji na pia udhaifu mwingine kasahau kuwacopy Tanesco ambao ndio wahusika wakuu sasa unavyomwambia mwenzio ana IQ ndogo nashangaa kuona kumbe wewe ndo una akili ndogo hujui chochote muombe radhi jamaa
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,823
2,000
Energy and Water Utilities Regulatory Authority- EWURA

Energy - Tanesco

EWURA imeundwa kwa sheria iitwayo EWURA Act.

Hii bodi inawajibika moja kwa moja na wizara za Nishati na Madini, Wizara ya Maji na Ofisi ya waziri mkuu (Mazingira).

Pia inafanya kazi na Tanesco pamoja na TPDC.

Mwenyekiti wa bodi anateuliwa na raisi na wajumbe wa bodi wanatoka sehemu nilizotaja hapo juu.

Kwenye Utawala kuna mkurugenzi mkuu ambae anateuliwa na mawaziri husika.

Ukiangalia kazi za bodi hii kuna sehemu katika sheria ya EWURA Act inaitaka bodi hii kupata mawazo ya waziri husika wa sekta husika kma ya umeme kabla ya kutoa taarifa za kupandisha au kupunguza gharama.

Hivyo kila waziri wa sekta husika anapaswa kuombwa mawazo yake, bila kurukwa.
hapo Lichard umemaliza kila kitu,
uzi ufungwe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom