Swali lolote kuhusu mambo ya upande wa pili (kiroho)

Sasa hapa kwanini tukahukumiwe ukiwa Allah kashaamua wema wetu na ubaya wetu,mimi nikiwa teyari nimeshapangiwa kwenda motoni si nitakuwa napoteza muda kuswali au nikiwa nimepangiwa kwenda peponi si nitakuwa namaliza bure maji kwenye kuratain?
Nalog off
Hapana mkuu nilichokuwa najaribu kueleza ni uwezo wa mwenyezi Mungu katika yaliyopo kwenye mamlaka, rejea nyuma kidogo ukumbuke kuumbwa kwa Adam, hakujua mwenyezi Mungu kama adam atakula tunda? Hakujua kama Allah adam atamtoa bustanini? Hakujua kama Adam atatubu? Hakujua kama atamsamehe?

Ukijijibu hayo njoo kwa Firauni, Hakujua kama Firauni hata kubaliana na maneno ya Mussa? Hakujua kama Firauni atatubu wakati anakata roho?

Na mengine mengi maana yake alijua kabisa lakini pia ukumbuke kuwa kila kitu anajua mwanzo na mwisho wake na vyote ni vyake na yeye tu ndio yeye kama alivyomuuliza Mussa, ewe bwana wangu wewe ni nani? Akajibiwa na Mwenyezi Mungu Mimi ni Mimi!!!

Kitu pekee kinachoweza kubadili alichokuandikia ni maombi tu na yeye anajua kama utaomba au huta muomba na atakupa au hata kupa wala huwezi kumlazimisha kwa chochote.
Anajua yote na anafanya kila analotaka, mamlaka ni ya kwake mkuu.
Hadi akili za kuchat na kila kitu ni vyake na haramu kaumba yeye na halali yeye

Rakims
 
Ulishawahi kuamka asubuhi ukawa unaskia nyimbo fulani imekukaa either unaipenda au huipendi lakini imekukaa masaa mengi akilini? Tuanzie hapo

Rakims
Ndio mkuu, mara kadhaa.Na imewahi kusababisha mpaka naamua kui download na naiskiliza mfululizo mara kadhaa,mpaka nitakapoanza kuizoea
 
Njia nyepesi na salama zaidi ni kufungua chakra mbili Crown Chakra na Third Eye Chakra
Nawezaje jinsi ya kufungua?, na ikiwa nitawaona hawatoweza kunidhuru wakijuwa nimewaona? Hivi mchawi na mtu aliyefunguwa chakra na third eye wakishindana ni Nani atakayekuwa na power zaidi kuliko mwenzie?
 
Habari yako mkuu, mimi huwa ninaweza nikakaa nikawaza au nikatamani jambo fulani linitokee mfano ninaweza nikatamani siku moja nije kuwa na gari zuri au siku moja nije niishi na mtu fulani n.k, na huwa ninawish kwa kipindi kirefu karibia kila siku na nakuwa naimani kitatokea au nitakipata na kweli jambo hilo ninalolitamani litokee au kitu hicho ninachotamani kuwa nacho ninakipata japokuwa inachukua muda, lakini kwa wakati huo ninapokipata au kumpata huyo mtu huwa ni kama too late yani namaanisha kinakuja wakati ambao huwa sikihitaji tena au sioni umuhumu wake tena. Simaanishi kama nimekata tamaa kukisubiri nikipate hapana bali inakuwa kama kile kitu au mtu niliyekuwa namhitaji amekuwa replaced na kitu kingine au mtu mwingine.

Hapo nilikuwa naomba unisaidie ni kwa nini inanitokea hivyo na ni njia gani nitumie ili niweze kukipata hicho kitu ninachokihitaji kukipata kwa wakati ambao nitakuwa nakihitaji.

Regards.
 
Thread hii nimeandaa mahususi kwa ajili ya kujibu na kutoa maelekezo vile nilivyo jaaliwa kuhusu maisha upande wa pili yaani ulimwengu wa kijini kichawi na kimiujiza, ikiwa una swali lolote kuhusu upande huo basi niulize na wanaofahamu zaidi wataweza kuelekeza kupitia Thread hii ikiwa kuna jambo litakuwa gumu basi tutalijadili kwa pamoja,

View attachment 1080884

Rakims
Mkuu usiku wa kuamkia leo nimeshtuka toka usingizini kidole cha shahada cha mkono wa kulia kikiwa na maumivu kama yale ya pin za kupima malaria ila ni maumivu makali mno, nakumbuka kama nilikuwa nashindana nisichomwe kidole nikawasha taa kuminya kidole nashangaa damu nyingi inatoka kweli lakini hakuna hata mtu wala mdudu yoyote, huu ni uchawi au ni kitu gani?
 
Ndio mkuu, mara kadhaa.Na imewahi kusababisha mpaka naamua kui download na naiskiliza mfululizo mara kadhaa,mpaka nitakapoanza kuizoea
Hiyo huwa kama reminder ya ubongo kuwa kuna jambo lilikuwa likiendelea wakati huo upo shule ilikuwa ni zuri kwa afya ya ubongo wako hiyo unakuwa unajaribu kukukumbusha kuuwekea kile unachohitaji ili uweze kufanikisha service fulani ya mwili au ubongo

Rakims
 
Nawezaje jinsi ya kufungua?, na ikiwa nitawaona hawatoweza kunidhuru wakijuwa nimewaona? Hivi mchawi na mtu aliyefunguwa chakra na third eye wakishindana ni Nani atakayekuwa na power zaidi kuliko mwenzie?
Mchawi anatumia shetani mkuu wewe unatumia roho yako na khalifa wa dunia ni binadamu si shetani wewe utashinda tembelea blog yangu utajifunza zaidi kwa uliyouliza
Rakims Spiritual

Rakims
 
Habari yako mkuu, mimi huwa ninaweza nikakaa nikawaza au nikatamani jambo fulani linitokee mfano ninaweza nikatamani siku moja nije kuwa na gari zuri au siku moja nije niishi na mtu fulani n.k, na huwa ninawish kwa kipindi kirefu karibia kila siku na nakuwa naimani kitatokea au nitakipata na kweli jambo hilo ninalolitamani litokee au kitu hicho ninachotamani kuwa nacho ninakipata japokuwa inachukua muda, lakini kwa wakati huo ninapokipata au kumpata huyo mtu huwa ni kama too late yani namaanisha kinakuja wakati ambao huwa sikihitaji tena au sioni umuhumu wake tena. Simaanishi kama nimekata tamaa kukisubiri nikipate hapana bali inakuwa kama kile kitu au mtu niliyekuwa namhitaji amekuwa replaced na kitu kingine au mtu mwingine.

Hapo nilikuwa naomba unisaidie ni kwa nini inanitokea hivyo na ni njia gani nitumie ili niweze kukipata hicho kitu ninachokihitaji kukipata kwa wakati ambao nitakuwa nakihitaji.

Regards.
Pitia hapa mkuu:
Hiyo uliyonayo ninmediumship

NGUVU ZA MIUJIZA (PSYCHIC POWERS)

Rakims
 
Mkuu usiku wa kuamkia leo nimeshtuka toka usingizini kidole cha shahada cha mkono wa kulia kikiwa na maumivu kama yale ya pin za kupima malaria ila ni maumivu makali mno, nakumbuka kama nilikuwa nashindana nisichomwe kidole nikawasha taa kuminya kidole nashangaa damu nyingi inatoka kweli lakini hakuna hata mtu wala mdudu yoyote, huu ni uchawi au ni kitu gani?
Tizama vizuri katika godoro lako mkuu itakuwa kuna sindano au kichuma cha sindano ukikosa jiangalie mwili wako wote kama kuna sehemu ina respond kwa maumivu kama hayo halafu takwambia ni nini

Rakims
 
Napenda kuwa mchawi make hizi dini za yesu mzungu hazijanikaaa kabisa.

Nisaidie niwe. Mchawi wa kutupwa km kweli upo sijaribishi nataka kweli. Niunganishe ila

Usinibanie kwa wivu!
 
1.Unaota unasafiri lakini haufiki!!!
2.Kwa nini wachawi Wana Roho ngumu kufa(hawafi mapema?)
3.Unatembea njiani unahisi kama vile kuna mtu anatembea nyuma yako ila ukigeukaa humwoni?
 
Thread hii nimeandaa mahususi kwa ajili ya kujibu na kutoa maelekezo vile nilivyo jaaliwa kuhusu maisha upande wa pili yaani ulimwengu wa kijini kichawi na kimiujiza, ikiwa una swali lolote kuhusu upande huo basi niulize na wanaofahamu zaidi wataweza kuelekeza kupitia Thread hii ikiwa kuna jambo litakuwa gumu basi tutalijadili kwa pamoja,

View attachment 1080884

Rakims
Kwema mkuu wangu,mm naomba msaada& ushauri pia,
Mosi:Kuna wakati nikilala hua naota nakimbizwa lkn baada ya mda nawashinda hao wanikimbizao unaweza kunieleza hii imekaaje?

Pili:naomba nitajie walau miti au chochote ambacho nikiwa nacho ndani sintosumbuliwa na nguvu za giza,yaan mti ambao hua wachawi hawapatani nao.asante.
 
Tofauti ya kutambika mizimu ya pande hizo mbili ni makabila ikiwa wote wanakabila moja basi utatakiwa utambike mara moja tu inatosha, na ikiwa una makabila tofauti utabidi utambikie kila moja kivyake na kwa taratibu zake,
Mizimu kumtesa mtu huja pale anapoipa kipaumbele na kutegemea msaada kutoka kwao tu, hapa mtu mwenyezi Mungu anakuwa kamkasirikia kwa maana kategemea mwingine asiyekuwa yeye,
Na ukiogopa hii mizimu ndio inakushurutisha lakini ukiweka hofu kwa mwenyezi Mungu pekee na roho yako ikatakatia kwake basi hautaona usumbufu wowote wa majini haya ya kienyeje(mizimu)

Rakims

Kuna maswali yake mengine hujajibu mkuu
 
Napenda kuwa mchawi make hizi dini za yesu mzungu hazijanikaaa kabisa.

Nisaidie niwe. Mchawi wa kutupwa km kweli upo sijaribishi nataka kweli. Niunganishe ila

Usinibanie kwa wivu!
Habari mkuu,
Sihusiki na uchawi mweusi kama hiyo ndio dhamira yako

Rakims
 
1.Unaota unasafiri lakini haufiki!!!
2.Kwa nini wachawi Wana Roho ngumu kufa(hawafi mapema?)
3.Unatembea njiani unahisi kama vile kuna mtu anatembea nyuma yako ila ukigeukaa humwoni?
Hizi ni dalili za kuwa na jini mkuu na kwa point yako ya 3 ni asili ya mapepo ya makaburini

Rakims
 
Kwema mkuu wangu,mm naomba msaada& ushauri pia,
Mosi:Kuna wakati nikilala hua naota nakimbizwa lkn baada ya mda nawashinda hao wanikimbizao unaweza kunieleza hii imekaaje?

Pili:naomba nitajie walau miti au chochote ambacho nikiwa nacho ndani sintosumbuliwa na nguvu za giza,yaan mti ambao hua wachawi hawapatani nao.asante.
Kuota unakimbizwa ni ishara za kufuatwa na uadui au uchawi ambao bado haujakufika,

Panda mti wa mzaituni nyumbani kwako kama mwenye nyumba mchawi atakufukuza

Rakims
 
Back
Top Bottom