Swali la utafiti: Wafanyabiashara Ulaya na Marekani huachwa wafanye watakalo?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
16,004
Amani iwe kwenu.

Swali hili la utafiti linalenga kupata uzoefu kutoka kwa wajuzi wa biashara nchi za ulaya na amerika.

Kumetokea hoja kinzani na makelele juu ya serikali kusimamia sheria na udhibiti wa bidhaa na huduma kwa walaji,limetokea kundi ambalo limetowa "vijisababu" ili tu kuonyesha wafanyabiashara wananyanyaswa.Mf."ni haki yangu kuuza mali yangu","je kama mimi ni mtengeneza juice" nk.

Kutokana na utata huo hapo juu,je nchi zilizoendelea uzoefu ukoje kwa masuala yafuatayo;

1.Adhabu gani hutolewa kwa wanaokiuka masharti ya leseni zao?

2.Mfanyabiashara yupo huru kuuza bidhaa atakavyo,huru?

3.Sheria za "consumer protection" zipoje?

4.Ni hatua gani huchukuliwa ikigundulika vitendo vya biashara vitapelekea serikali kugombana na raia?

Hoja ni nyingi,ninahitaji kujifunza kutoka kwa wazoefu.

Nawasilisha.
 
Mkuu ningekuwa rais leo leo ningekuapisha kuwa DC ,umenena point
Wanachosha sana watu, kwenye masuala muhimu ya haki za kibinadamu wanaleta ubabe, kwenye masuala ambayo seikali ilisha tangaza ni huria wamefeli wanataka kuleta ulinganisho na nchi zinazojali demokrasia na haki za binadamu, hivi soko huria soko holela nani aliliasisi? Tunachoshana bure tu.
 
Ulaya kila mfanyabiashara anafanya yake na haingiliwi na serikali labda akiuke masharti ya ufanyaji biashara, na kule ushindani ndiyo unaamua soko, wanazalisha Sana wateja hakuna, imefikia kipindi ili watengeneze bidhaa za bei nafuu siku hizi wanahamisha viwanda inchi masikini ambako gharama za uzalishaji ziko chini na mishahara ya wafanyakazi iko chini ndiyo maana makampuni makubwa yanakimbilia inchi kama India na kwingineko
 
Kwa nini kwenye biashara tuwatazame ulaya na marekani lakini kwenye suala la uchaguzi huru hamtaki kuzitizama hizi nchi? Tuache unafiki.
Sasa basi Raisi yupo sawa,kwanini akisimamia sheria mnabinua midomo ICC,ICJ..Triump?
 
Ulaya kila mfanyabiashara anafanya yake na haingiliwi na serikali labda akiuke masharti ya ufanyaji biashara, na kule ushindani ndiyo unaamua soko, wanazalisha Sana wateja hakuna, imefikia kipindi ili watengeneze bidhaa za bei nafuu siku hizi wanahamisha viwanda inchi masikini ambako gharama za uzalishaji ziko chini na mishahara ya wafanyakazi iko chini ndiyo maana makampuni makubwa yanakimbilia inchi kama India na kwingineko
Je ulaya wanaruhusu ukiritimba (monopoly) na (collussion/cartel) kwa wafanyabiashara ili kupanga bei ya bidhaa?
 
Wanachosha sana watu, kwenye masuala muhimu ya haki za kibinadamu wanaleta ubabe, kwenye masuala ambayo seikali ilisha tangaza ni huria wamefeli wanataka kuleta ulinganisho na nchi zinazojali demokrasia na haki za binadamu, hivi soko huria soko holela nani aliliasisi? Tunachoshana bure tu.
Haki zipi za binadamu zimekandamizwa?
 
Bahati mbaya umeanzisha uzi biased, umewatambulisha wafanyabiashara pekee Kama wahujumu bila kuonesha watunga sera wanaingiliaje nguvu za soko ambazo Kama taifa tuliamua kuzifuata bila mipango( kichwakichwa), kwa sasa hivi kwa sehemu kubwa tunagombana Na matokeo ya tatizo, serikali ndiyo iliyovunja bodi ya sukari, serikali ndiyo inayotoa vibali vya kuingiza sukari toka nje ya nchi(Kumbuka kashfa ya sukari ilivyomtumbua mzee Iddi Simba akiwa waziri), serikali hii ndiyo iliyopiga marufuku uingizaji wa sukari toka nje ili kulinda viwanda vya ndani, serikali hii ndiyo imetangaza juzi Arusha kutenga fungu la kutosha la kuagiza sukari ya kutosha toka nje ya nchi, hadi hapo hatuna sera inayoelekeza nini endelevu kifanyike, tunaishia kusikia amri za maelekezo. Wafanyabiashara nao Ni wananchi Kama walivyo walaji. Tusihukumu upande mmoja kwa hisia Tu kwamba serikali Ina nia njema Na wananchi Na wafanyabiashara wanatafuta Tu faida, jaribu kuangalia wajibu wa msingi wa serikali Na imefanya nini kuutimiza!.
 
Je ulaya wanaruhusu ukiritimba (monopoly) na (collussion/cartel) kwa wafanyabiashara ili kupanga bei ya bidhaa?
Sijui kama nchi hii ina ukiritimba wewe ndio umeniambia, nini kinasababisha ukiritimba? Viwanda vinazalisha bidhaa ya kutosha? Maana kama kila siku viwanda vinatimiza wajibu wake wa kuzalisha mali sidhani kama bei itakuwa juu wala kuna mtu ataficha mali, utafichaje wakati kila siku inatoka huko? Na kwa nini isiwe kila mfanya biashara akanunue bidhaa kwenye viwanda mnaweka vibali kwa baadhi ya watu? Haya yameasisiwa na ccm wenyewe.
 
Bahati mbaya umeanzisha uzi biased, umewatambulisha wafanyabiashara pekee Kama wahujumu bila kuonesha watunga sera wanaingiliaje nguvu za soko ambazo Kama taifa tuliamua kuzifuata bila mipango( kichwakichwa), kwa sasa hivi kwa sehemu kubwa tunagombana Na matokeo ya tatizo, serikali ndiyo iliyovunja bodi ya sukari, serikali ndiyo inayotoa vibali vya kuingiza sukari toka nje ya nchi(Kumbuka kashfa ya sukari ilivyomtumbua mzee Iddi Simba akiwa waziri), serikali hii ndiyo iliyopiga marufuku uingizaji wa sukari toka nje ili kulinda viwanda vya ndani, serikali hii ndiyo imetangaza juzi Arusha kutenga fungu la kutosha la kuagiza sukari ya kutosha toka nje ya nchi, hadi hapo hatuna sera inayoelekeza nini endelevu kifanyike, tunaishia kusikia amri za maelekezo. Wafanyabiashara nao Ni wananchi Kama walivyo walaji. Tusihukumu upande mmoja kwa hisia Tu kwamba serikali Ina nia njema Na wananchi Na wafanyabiashara wanatafuta Tu faida, jaribu kuangalia wajibu wa msingi wa serikali Na imefanya nini kuutimiza!.
Bodi ya sukari haijavunjwa,ipo.Toa uzoefu kwa nchi za ulaya na amerika kulingana na hoja.Je kwa amerika na ulaya ikigundulika mfanyabiashara kaficha bidhaa adimu nini hutokea?..Ninakubali kuwa wafanyabiashara ni wananchi ila miongoni mwa wananchi kuna wahalifu.
 
Tatizo letu tunategemea mtu mmoja tusuluhishie matatizo yetu badala ya kujenga mifumo mizuri ya kiutawala. Ningekuwa mimi Magufuli ningeanza na kufumua mifumo tuliyonayo ambayo imepitwa na wakati. Ni aibu leo hii tuko katika karne ya 21 na bado tuna tatizo la watumishi hewa.
 
Hoja ya Zanzibar haihusiki hapa.Jikite kwenye mada.
Unapouliza ulinganisho wa masuala ya nchi mbili linganisha yote na si baadhi ya mambo, kifupi ni kuwa nchi hizo ulaya na marekani hakuna alie juu ya sheria ndio maana unahoji haya lakini kwetu sivyo chama tawala kipo juu ya sheria ndio maana unapata kizunguzungu huelewi linaloendelea nchi sababu ni nini.
 
Tatizo letu tunategea mtu mmoja tusuluhishie matatizo yetu badala ya kujenga mifumo mizuri ya kiutawala. Ningekuwa mimi Magufuli ningeanza na kufumua mifumo tuliyonayo ambayo imepitwa na wakati. Ni aibu leo hii tuko katika karne ya 21 na bado tuna tatizo la watumishi hewa.
Mfumo ni nini?...mbona Kenya walipitisha Katiba mpya na sasa wanajipanga kubadili baadhi ya vifungu?Ufisadi umetamalaki?.Bila kuwa na tabia ya watu kusimamia sheria hata tukiletewa Katiba ya amerika hakutakuwa na mabadiliko.Kenya na Katiba mpya Jaji kala rushwa ya dola milioni 2.
 
Back
Top Bottom