mimi naichukia ccm kwa sababu nakiona ni chama kinachojitahidi kuficha mabaya yanayofanywa na serikali,na yakijitokeza wanayatetea kwa nguvu zote na wanawachukia wale walioyatoa hayo mabaya.Swali hili ni kwa wale ambao katika fikra zao na mioyo yao wameamua kuikataa CCM. Wameamua kutokujiunganisha wala kujiambatanisha na chama tawala. Kwa hawa CCM ni kinyume nao. Napenda kujua hasa wale wanaoikataa CCM wanaikataa kwa sababu gani hasa? Maana wengine wanaikataa CCM kwa kadiri ya kwamba wako nje lakini wakiingia ndani au wakionjweshwa vya ndani wanakuwa wa kwanza kuitetea. Inawezekana wanaoikataa CCM hawaikatai kwa sababu moja ya msingi isipokuwa sababu nyingi za binafsi?
Je wewe unaikataa CCM? umewahi kujiuliza ni kwanini?