Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,369
- 5,512
ingeweza kushughulikia mambo hayo yote ungeiunga mkono na kuikubali? Vipi kama ikianza kufanya hivyo sasa?
Hilo ni wazo la kinadharia sana. Haiwezekani CCM (ikiwa madarakani) kufanya la maana bila mapinduzi makubwa kutokea yatakayoibandua CCM toka kwenye makucha ya mafia (mafisadi) wa ndani na nje. Kazi yao ni moja tu hivi sasa: ni kusimamia na kuratibu uporaji wa rasilimali za nchi kwa manufaa ya kikundi maalumu cha "mabwana" ndani ya chama. Wana-CCM wasio na "nasaba" wanatumika tu kama vibarua (watwana) kwa ujira/ushawishi wa makombo.
Baada ya kuimarisha mfumo wa rushwa/ufisadi, hao mafia sasa wamefikia hatua ya kutumia mauaji na hofu kama mkakati wa kubakia madarakani na kukandamiza haki zote na utu wa Mtanzania ili kila mtu aishie kutegemea fadhila zao ili aweze kuishi na kupata "maendeleo"; wanaendesha kampeni ya udini, ukabila na ukanda(?) ili kuligawa kabisa taifa lipoteze kabisa umoja mradi tu wao wabakie na kudumu madarakani kama nyenzo pekee yenye uwezo wa kuunganisha nchi!
Sioni namna CCM kinaweza kurejea kwenye misingi ya ustaarabu zaidi ya kuwekwa nje ya madaraka ya serikali ili angalau mafia wakikimbie na kukiacha kianze upya - kama kitaweza kupona hilo likitokea. Hiki chama hivi sasa ni kama vile kimekumbatiwa kikamilifu na shetani ambaye hakina namna ya kumponyoka!