Sababu zangu za kuichukia CCM ni hizi hapa
1. Ahadi
ni wazuri sana kwenye kutoa ahadi lakini hawana utekerezaji. Kwa mfano ahadi za JK za 2010 nyingi sana bado na ukiangalia muda aliobaki nao, hautoshi kuzitekeleza zote. Mfano hospitali za rufaa, viwanja vya ndege, viwanda huko mtwra ndo vinaleta shida hadi sasa, meli ziwa victoria na nyasa, machinga complex, etc etc
2. Kuutazama upinzani kama uadui. Kada wa CCM akimwaga matusi hadharani siyo issue, lakini wa upinzani inakuwa issue. Why double standard? Mfano kesi ya ubunge wa Lema na matusi Mwigulu Nchemba.
3. Bunge kuwa under CCM. Hadi leo sijaona lolote baada ya kumba mwongozo wa waziri mkuu kulidanganya bunge. Ulitakiwa ushahidi na ukaletwa, lakini hadi leo hauna kitu. Wabunge wa CUF waliwapa passport vimada na wote tunajuwa yaliyowakuta. Why double standard?
4. Kauli ya waziri mkuu kuhusu meremeta inaonyesha kuna watu wapo juu ya serikali na serikali inalitambua hilo. Na kwamba serikali inawaogopa watu hao.
5. WanaCCM kutoa kauli zinazopingana juu ya jambo moja. Na ile tabia ya kumuita mtu dodoma na kumtishia lolote haionyeshi uwepo wa demokrasia. Angalia yaliyomtokea Samwel Sitta. Mara atishiwe kunyang'anywa kadi hii yote ni kutokana na msimamo wake juu ya maswala ya kitaifa.
6. Haya, makundi ndani ya CCM ni alama tosha kuwa wapo mle kwa maslahi binafsi. Hata Nape alisema kwenye mkasi kuwa Lema alishinda kwa sababu ya ugomvi ndani ya chama.
7. Kila mtu ndani ya CCM amegeuka mlalamikaji. Huwezi jua nani wa kutengeneza, mfumuko wa bei, siyo sisi tu hata nchi nyingine upo, huduma za kijamii bure jibu haiwezekani kwa vile nchi zingine wanachangia, lakini wanasahau nchi hizo hawana mali asili kama zetu. Huko kwingine hawaibiwa hadi nembo ya taifa, mfano twiga, ndani ya kiwanja chenu cha ndege. Yaani kila mtu analalamikia mgawanyo wa vitalu, hakuna mtekelezaji.
Jamani nina mengi, nasikia uchungu sana pale ninapomwona mwana CCM anajisifia kuhusu shule za kata wakati mtoto wake hasomi huko.
mwingine naye anajisifia kwa urefu wa foleni eti ni maendeleo....
Na hizo kauli zao ndo zinakera kweli, kwa mfano eti hata nyasi tule lakini ndege ya raisi lazima inunuliwe... Khaaaaa, mwingine naye eti waTZ tuna wivu wa kijinga kwa wawekezaji... Mhnnn...