Swali la Ugomvi: Jeshi Lisilo na Nidhamu Linaweza Vipi Kushinda Vita?

Pasco wewe unaamini Zitto ndio mwarobaini wa ugonjwa wa CDM lakini ukisoma wenzako unaona jinsi walivyo honest kuhusu tatizo halisi badala ya chuki tu kwa watu wawili Mbowe na Slaa.
Kwa umri wenu mnapaswa kuwa waungwana na kukosoa bila chuki tu kama mjamzito anapoamua kuchukia kitu tu huku akitoa vijisababu vya kipuuzi.
Ukirudia tena kusoma bandiko la MM utaelewa bandiko hili limekusudia nini.
 
Last edited by a moderator:

Huo si uoga hiyo ndio demokrasia. CCM si mali ya familia.
 
....Lema alipaswa walau kukemewa juu ya hatua yake ya kumkashifu Zitto mitandaoni. Lakini cha kushangaza Katibu Mkuu anamgongea "Like"
"Like" inawezekana ikamaanisha 'Noted', si lazima maana yake kwamba umependa kilichoandikwa. Mfano mzuri ni Pasco, yeye akiipitia post yako katika thread aliyoanzisha ataigongea "Like"
 
Kwa hali halisi ilivyo, Jeshi la kijani (aka Jeshi la Magamba) likichomoza vizuri katika kumteua mgombea wa Urais, basi jeshi hili la Magwanda litashindwa vibaya!
 
"Like" inawezekana ikamaanisha 'Noted', si lazima maana yake kwamba umependa kilichoandikwa. Mfano mzuri ni Pasco, yeye akiipitia post yako katika thread aliyoanzisha ataigongea "Like"

Usilazimishe tafsiri unayoitaka wewe, hata siku moja LIKE haiwezi kuwa mbadala wa NOTED!
 
Kwa hali halisi ilivyo, Jeshi la kijani (aka Jeshi la Magamba) likichomoza vizuri katika kumteua mgombea wa Urais, basi jeshi hili la Magwanda litashindwa vibaya!

Yupi huyo mgombea mzuri atakaekubalika na wenzake wakati kila mtu ccm anadhani yeye ndie anaefaa?
 
Mkuu Mwanakijiji bandiko zuri. Lakini nikuambie kitu kimoja nacho ni hiki: Jeshi kuna nidhamu na amri vilevile. Jeshini hakuna kitu inaitwa Demokrasia bali amri. Hii ni tofauti sana na vyama vya siasa. Nidhamu ndani ya vyama vya siasa ni demokrasia na hoja zenye nguvu badala ya ubabe na vitisho. Kusipokuwa na demokrasia ya kweli ndani ya vyama vya siasa lazima kukosekane nidhamu. Nidhamu itatoka wapi kama kuna kuburuzuna bila demokrasia?
 

Chanzo ni CCM kutaka kuiangamiza CDM kupitia mamluki wake ndani ya CDM hivyo immediate action ni ku castrate hicho chanzo ambacho kinahusishwa na nidhamu mbofumbofu ndani ya jeshi na vita itaendelea kukiwa na amani ndani ya wapiganaji
 
Mfano wa Jeshi na Chama cha Siasa ni mfano mfu- JESHINI NI AMRI TU, UTAKE UNAFUATA USITAKE UNAFUATA HAKUNA DEMOKRASIA KULE. KWENYE CHAMA, TENA KINACHOITWA CHA DEMOKRASIA KUNAFUATWA DEMOKRASIA, KUNA KUHOJI, KUNA KUFANYA SIASA NA MIPANGO ILI UMSHINDE MWENZIO KWENYE CHEO CHAKE.

BAHATI MBAYA MAKALA YA MWANAKIJIJI INAJARIBU KUMSINGLE OUT ZITTO NA WENZIWE KWAMBA "WASIO NA NIDHAMU", SIJUI ANATAKA WAWE NA NIDHAMU KWA MUJIBU WA NIDHAMU ANAYOIJUA MBOWE AU NIDHAMU KWA MUJIBU WA KANUNI NA SHERIA ZA CHAMA?.

HATA KAMA UMEAMUA KUCHAGUA UPANDE, KUWA MUWAZI TU ILI TUKUULIZE MASWALI MAGUMU, YA USHSHIDI UTHIBITISHO WA TUHUMA ZINAZOMKABILI MH ZITTO. USIKWEPE STAND UP AND BE COUNTED.
 

Makavu live
 
"Like" inawezekana ikamaanisha 'Noted', si lazima maana yake kwamba umependa kilichoandikwa. Mfano mzuri ni Pasco, yeye akiipitia post yako katika thread aliyoanzisha ataigongea "Like"

Mkuu kama Lema hakuwa na backing ya viongozi alichukuliwa hatua gain. Tuwe wakweli double standards zitatumaliza
 
"Like" inawezekana ikamaanisha 'Noted', si lazima maana yake kwamba umependa kilichoandikwa. Mfano mzuri ni Pasco, yeye akiipitia post yako katika thread aliyoanzisha ataigongea "Like"

Laiti wenye mtandao wa JF wangetaka kitufe cha "Like" kiandikwe "Noted" wangeweza, na hiyo ni rahisi kweli lakini hivyo ni vitu viwili tofauti. angalia tena dictionary
 

Unataka kusema kuwa demokrasia haiitaji nidhamu? as a matter of fact demokrasia inaweza kusimama tu pale kwenye nidhamu. Think about it.
 
Mfano wa Jeshi na Chama cha Siasa ni mfano mfu- JESHINI NI AMRI TU, UTAKE UNAFUATA USITAKE UNAFUATA HAKUNA DEMOKRASIA KULE.

Sidhani kama unafahamu utendaji wa kijeshi. Jeshini si 'amri tu'. Katika utendaji wa kinidhamu kuna wakati mtu anaweza kukataa amri jeshini na akawa sahihi. Kuna utaratibu wa kufuata amri; hufuati amri tu. NI kujidanganya kudhani kuwa demokrasia inaweza kushamiri na kukua bila kuwa na nidhamu.
 

Nidhamu pekee ya jeshi si hoja ya kushinda vita, kuna vitu kadhaa vinavyoweza kudhoofisha wapiganaji vitani na vitu hivyo visipofanyiwa masahihisho au kuondosha virusi vinavyoweza kudhoofisha wapambanaji katika uwanja wa mapambano.

Jeshi la Marekani lilipokuwa kwenye mapambano huko Iraq ulimwengu ulishuhudia virus waliomo jeshini walivyoathiri jeshi katika mapambano na baadhi licha ya kuvujisha siri kwa maadui waliamua kuchukua silaha za maangamizi na kuwageukia wanajeshi wanzao kuwamaliza kwenye kambi yao, hapana shaka Wamarekani liliwafikirisha na kujutia kutokuwa makini na virus hao.

Kwa mtazamo wa wanakijiji kuendelea kukumbatia virus ndio nidhamu katika mapambano wakati wanadhoofisha na kuharibu mshikamano, uimara wa jeshi katika mapambano ni mshikamano, umoja na malengo ya pamoja, lakini ukishaanza kuunda vikundi ndani ya jeshi ujue umeshabomoa nguvu ya mshikamano na kuruhusu adui kupenya kiulaini ndani ya ngome yenu.

Kwa vyo vyote kuna risk katika kuamua kuondoa virus hawa, ukiangalia madhara ni kidogo kuliko kuendeleza, maana wakiachwa madhara ni makubwa kama ilivyotokea kwa baadhi ya majeshi yalivyosambaratishwa na hawa virus ilivyokuwa akina Lyatonga na wenzake.

Mzee mwanakijiji umetazama upande mmoja wa sarafu tu, jaribu kugeuza upande wa pili uone hii sarafu unayoiongelea ina mwonekana upi.
 



Huwezi kumlinganisha Lema na Zitto. Lema alishambuliana na Zitto kama watu wawili binafsi...ni kama wanajeshi wawili wa kikosi kimoja wakatwangana, hii haimaanishi kikosi kizima kimetwangana. Lakini ukiangalia majibu ya Zitto kwa Lema, Zitto hakuwa anapigana na Lema. Yeye alimhusisha Lema na kifaranga...kwamba kuna mama yake amemtuma. Sasa wapi Lema aliandika kwamba ametumwa na chama kumshambulia Zitto? Yeye Zitto ndo alianza kwa kumponda Lema akitumia magazeti yake pendwa, Lema akamjibu Zitto. Zitto nini kilimfanya amhusishe Lema na chama? Ni wazi kwamba Zitto haipendi CHADEMA na ndiyo maana kila anapopata wasaa wa kujibu tuhuma , hukihusisha chama chote hususani uongozi wa juu kama ndo wanagombana naye. Lema na Zitto wote walikosea kushambuliana, lakini kama ni makosa, basi Zitto amekosa zaidi kwa kuwaingiza wasio kuwemo kwenye ugomvi wake.
Turudi kwenye nidhamu ya jeshi:
Kama ni jeshi kujipanga basi CHADEMA walau wameanza kuona rogue elements na wanaziondoa au kuzishughulikia. Kama wametoa adhabu isiyostahili, hilo siyo kosa, at least wamediriki. Yaani wameona nyufa na wanaziziba...sasa kama wanaziba kwa nondo mahali pa simenti hilo ndo tujadili. Kwangu mimi kikubwa ni kwamba wameliona tatitizo na wamechukua hatua. Huwezi kuwalinganisha na CCM ambao wameona tatizo, wakashindwa kulishughulikia. Walisema watawafukuza "mafisadi" ndani ya siku tisini , lakini hao mafisadi sasa ndo wamekishika chama. Sasa wanamtukana Amiri Jeshi Mkuu kwamba ni Dhaifu, hawezi kuchukua maamuzi magumu. Naye amiri jeshi mkuu amenywea anagugumia tu! Yaani adui anakuchokonoa kwamba "dare to shoot me!" wewe amiri Jeshi mkuu unacheka unasema yataisha yenyewe ..reall? Eti taarifa zinasema wamefunguliwa "mafaili" ili wakigombea uraisi wakatwe...hiyo ndo adhabu ya kumpa rogue military officer? Kumfungulia faili, huku ukimwacha atambe na kukutukana kwamba wewe ni dhaifu usiyeweza kumfanya chochote? Come on....huu ni upuuzi wa hali ya juu wa CCM.
Mimi nasema, ningekuwa niko kwenye kamati kuu ya CHADEMA, ningeongea kama Tundu Lisu, yaani hao wasaliti wa chama hawastahili heshima yoyote zaidi ya kufukuzwa uanachama. Hiyo demokrasia wakaitafute nje ya CHADEMA, they are free!!!
 
Laiti wenye mtandao wa JF wangetaka kitufe cha "Like" kiandikwe "Noted" wangeweza, na hiyo ni rahisi kweli lakini hivyo ni vitu viwili tofauti. angalia tena dictionary
Mkuu sio suala la tafsiri ya dictionary, ni la kimantiki. Umesema wangetaka wangeweza, ila sasa hawajataka na hakipo. Sasa kama hakuna kitufe cha "noted", watu si wanagonga hiyo hiyo iliyopo?
 
Nidhamu pekee ya jeshi si hoja ya kushinda vita,

Ukinisoma utaona sijasema "nidhamu pekee". NItakuwa sielewi jeshi wala masuala ya vita au jinsi ya kutafuta ushindi. Unaweza kubadilisha wanajeshi, vifaa au hata utaalamu lakini huwezi kubadilisha nidhamu. Can you?
 
Ukinisoma utaona sijasema "nidhamu pekee". NItakuwa sielewi jeshi wala masuala ya vita au jinsi ya kutafuta ushindi. Unaweza kubadilisha wanajeshi, vifaa au hata utaalamu lakini huwezi kubadilisha nidhamu. Can you?

Nidhamu ndio msingi wa mwundo na utendaji jeshini, na hakuna jeshi lisilo na nidhamu vinginevyo lisingekuwa jeshi tena maana kinachowaweka pamoja na kutii amri ni nidhamu. Lakini hiyo nidhamu si kigezo cha kushinda vita, kuna makandokando mengi yanayoweza kusaidia kushinda vita na kuna mengi tu yanayoweza kusababisha kutoshinda vita hata kama jeshi lina nidhamu.

Kuna wakati mmoja anaweza kufanya zaidi ya wengine pekee ili kuleta ushindi kama kwenye biblia ilivyotokea kwa Daud kumshinda jabali goliati. Kuna mambo mengi ndani ya nidhamu ambayo yanaweza kusaidia au kusitisha ushindi, yanaweza kuonekana madogo madogo lakini yasipofanyiwa kazi itakuwa kazi pia kazi kufanikiwa.
 

umemaliza mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…