Swali la Ugomvi: Jeshi Lisilo na Nidhamu Linaweza Vipi Kushinda Vita?

Mnatapatapa tu, kujidai kuikuza chadema na kuitolea mifano ya jeshi na USA.

chadema kimenuka, hakuna zaidi!

Hukuyaona ya Mrema na Marando huko zamani? yalifikia tamati hivi hivi, kama tuonavyo sasa. Labda uwadanganye wasiokuwapo.

Chadema kimeshafanya kazi yake kama kilivyopangiwa na sasa ni wakati muafaka kuki-nyutralaizi. Hakuna zaidi.
kama mlifanikiwa kwa NCCR ya Marando na TLP ya Mrema miaka hiyo, kwa CDM si rahisi - Jipangeni upya!!
 
Ukinisoma utaona sijasema "nidhamu pekee". NItakuwa sielewi jeshi wala masuala ya vita au jinsi ya kutafuta ushindi. Unaweza kubadilisha wanajeshi, vifaa au hata utaalamu lakini huwezi kubadilisha nidhamu. Can you?

Virus niliosema wanaweza kuharibu mambo mengi katika mapambano ndio hao unaona OFISI ZA CHADEMA KUCHOMWA MOTO ARUSHA SASA HIVI nini kinaendelea kama sio hawa virus?
 
Mkuu Mwanakijiji bandiko zuri. Lakini nikuambie kitu kimoja nacho ni hiki: Jeshi kuna nidhamu na amri vilevile. Jeshini hakuna kitu inaitwa Demokrasia bali amri. Hii ni tofauti sana na vyama vya siasa. Nidhamu ndani ya vyama vya siasa ni demokrasia na hoja zenye nguvu badala ya ubabe na vitisho. Kusipokuwa na demokrasia ya kweli ndani ya vyama vya siasa lazima kukosekane nidhamu. Nidhamu itatoka wapi kama kuna kuburuzuna bila demokrasia?


Awali ya yote nimpongeze Mzee Mwanakijiji kwa swali lake la kigomvi lenye maudhui muafaka kwa wakati huu. Tena umepatia kwelikweli maana hawa wana CDM hujigamba sana kwa kujiita "makamanda" dhana ambayo huashiria namna fulani ya jeshi hivi.

Mkuu Kimbunga mtazamo wa Mwanakijiji unaupata kweye misingi ya demokrasia maana japo kuna tafsiri nyingi za demokrasia lakini misingi yake ni ileile miwili.

Msingi wa kwanza ni wengi kuwasikiliza maoni ya wachache. Hapo sasa ndipo hoja na maelezo hutolewa na ya kujibiwa hujibiwa. Lakini msingi wa pili wa demokrasia ni wachache kutii uamuzi wa wengi. Kwamba baada ya majadiliano na kufanya uamuzi lazima wale wachache ambao hawakubali uamuzi wa wengi watii uamuzi huo. Huo utii ndio ambao Mwanakijiji anauita kwa usahihi kabisa, kuwa ni nidhamu. Unaweza kuita huko ni kuburuzwa au jina lolote unalotaka lakini kama kweli mtu ni muamini wa demokrasia hana budi kufuata misingi hii miwili muhimu ya demokrasia. Kwani kila sarafu halali ina pande mbili, na demokrasia halikadhalika. Vinginevyo kama sarafu ina upande mmoja itakuwa feki na ikiwa mfumo wa demokrasia una upande mmoja utakuwa kitu kingine ambacho Wanigeria wanaita "Demon-crazy".

Kuna watu ambao asipokuwa yeye ndiye katoa wazo au yeye ndiye kachaguliwa basi hiyo si demokrasia. Kama kanuni zilizowekwa (hata kwenye katiba ya chama) haziendani na matakwa yake basi huko ni kuburuzwa. Tukubali ukweli kuwa chama chochote kinachofuata demokrasia kuna muda wa kusikiliza mawazo ya pande zote, pamoja na yale ya wachache lakini muda ukifika maamuzi yakafanyika wachache ni lazima wakubali na kutii maamuzi ya wengi. Shida iliyopo CDM ni wachache kutaka wengi watii maamuzi ya wachache kwa kuyabatiza maamuzi ya wachache kuwa ndiyo demokrasia. Si kweli. Huo ndio udikteta au kama Mzee Mwanakijiji alivyoweka sawa kuwa ni uasi. Dawa ya muasi popote inajulikana. Acheni waasi washughulikiwe kwa mujibu wa taratibu.

Mwanakijiji ningependa kwa kupitia chapisho lako uoone udikteta ambao unaletwa na utovu wa nidhamu. Madikteta (aka waasi) huwa wanaamini kuwa ni wao tu tena wao pekee ndio wanaostahili kuongoza jeshi lolote ambalo litapata ushindi (my way or the highway!). Hiyo ndiyo sababu ya hujuma na chokochoko zisozoisha. Wanajua ulichokieleza kuwa jeshi lisilo na nidhamu haliwezi kushinda. Ili wanaoongoza mapambano, (maana wameona ushindi unanukia) wasisinde, silaha ya waasi ni utovu wa nidhamu. Maana kama mambo yote wanayozoza yaliamuliwa na vikao halali vya chama (chama ni wanachama, chama ni vikao) na kwa bahati wenyewe wakiwemo kwenye vikao hivyo, misingi ya demokrasia ikachukua mkondo wake, maamuzi yakafanywa na walio wengi, imekuwaje leo wanapinga? Hawa ni wabinafsi tu na wenye roho za uasi daima. Bila shaka ukifuatilia historia zao utaona kwao wanachokiita demokrasia ni pale wao waliposhinda au mawazo yao yanapokubaliwa.

 
Wanasiasa wa kigoma wamelogwa si mwamkumbuka kafulila kaharibu cdm yeye na zito kaenda nccr kataka kuleta mapinduzi.mi naona waanzishe miradi ya migebuka tu.mwingine kila siku anasema ---- you bungeni.ni puppets leka tu tigite.

Pamoja na kushambulia wanasiasa kutoka sehemu inayonihusu, bado umenipa kufikiri zaidi:
> mahusiano ya Zitto na Kafulila; kutimuliwa kwa Kafulila kutoka Chadema;
>uungaji mkono wa Zitto kwa Kafulila hata baada ya Uongozi wa CDM wakati yeye Zitto aliendelea kumuunga mkono Kafulila wakati yeye ni sehemu ya uongozi wa Chama [huu ni usaliti maana angeweza kumshauri Kafulila aombe radhi na yeye Zitto kuwa mediator].

Nakubaliana na hoja ya Mwanakijiji, Chadema kuchelewa kuchukua hatua walizochukua, walikuwa 'wanawaharibu Makamanda na Askari wao ambao pasi na shaka walifikia mahali wakajidhania kuwa wao ndio Chadema na Chadema ndio wao, na kuwa bila wao hakuna Chadema.

Kama sivyo, basi walikuwa na mission yao ambayo inaweza kuwa ndio sababu Wassira Steven aliitabiria kifo Chadema kabla ya 2015?

Je, kauli tata za Makamanda baada ya uamuzi wa KK ya CDM, hazitoshi kutufanya kuamini kuwa Makamanda tuliowaamini kuongoza Jeshi letu wamepotoka? Je, 'kupotoka' huko kwa Makamanda hawa, ni kwa bahati mbaya au makusudi? Kama ni kwa bahati mbaya, mbona kauli zao zinazidi kuwa tata kila wanapozungumza?

Tuvute subira tuone.
 
Mara nyingi utaona watu wanalisifia sana jeshi letu la Ulinzi hasa baada ya operesheni fulani. Mfano mzuri ni hili la kwenda DRC na kuwachakaza M23; licha ya kupoteza wapiganaji kadhaa jeshi letu bado limesifiwa kwa umahiri katika medani ya mapambano.

Kwa wale tulioshuhudia kwa karibu Vita ya Kagera na harakati za Ukombozi wa Nchi zilizoko Kusini mwa Afrika tunajua ni kwa kiasi gani jeshi letu lilijipatia heshima katika kushiriki mapambano, kutoa mafunzo na kulinda usalama wa nchi yetu. Kiasi kwamba tulijiaminisha kuwa jeshi letu ni mahiri kabisa katika eneo letu hili. Kutokana na ujuzi huo tumekuwa na kiburi cha ufahari wa jeshi letu; ndio maana tunapochokozwa na majirani zetu hatuchelewi kuanza kushadadia vita na mapambano kwa sababu tunaamini kabisa kuwa katika eneo letu hakuna nchi ambayo inaweza ikaingia vitani na sisi ikatupiga; siyo Malawi, siyo Rwanda wala siyo nani.

Siri ya mafanikio haya ya jeshi letu ni nini hasa? Je ni kwa sababu tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika vifaa vya kijeshi? (hili si kweli); je inawezekana ni kwa sababu tuna silaha za kisasa zaidi kuliko wengine? au kwa sababu sisi ni Tanzania kana kwamba kwa kuwa Tanzania basi automatically jeshi letu ni bora zaidi? Au kuna siri kubwa zaidi na ya msingi?

Naomba kupendekeza kwa msomaji kuwa siri ya mafanikio ya jeshi lolote duniani (likiwemo la kwetu) imelala kwanza kabisa katika nidhamu (discipline). Jeshi lisilo na nidhamu haliwezi kushinda vita hata kama lina silaha, wataalamu au mabilioni ya pesa. Vitu vingine ni muhimu sana katika kufanikisha mapambano lakini hakuna kitu muhimu kama kuwa na wapiganaji walio na nidhamu iliyopitiliza; ambao wanatambua majukumu yao barabara na ambao pamoja na makamanda wao wako moyo mmoja kutafuta ushindi. Hakuna brigedi, hakuna kikosi, hakuna company ambayo inaweza kusimama peke yake au kujifanyia mambo yake kwa ajili ya sifa zake yenyewe. Jeshi lote na sehemu yote chini ya majenerali husika ndio linaenda kutafuta ushindi. Jeshini hakuna sifa ya kikosi moja au kapteni mmoja!

Lakini ni hii nidhamu ndio msingi wa ushindi. Baada ya nidhamu hii ni ile hali ya kujitoa kwa lengo lililoko - total commitment to the cause. Mara baada ya lengo kuwekwa bayana -kumtambua adui na kupambana naye - vikosi vyote chini ya makamanda wao na wote hao chini ya kamandi kuu ya vita (Military High Command) vita vinaenda kupiganwa. Hiyo MHC nayo inapata maelekezo yake ya malengo ya kisiasa kutoka kwa viongozi wa kiraia wa nchi (civilian authorities) wakiongozwa na Amiri Jeshi Mkuu. Kutoka hapa ndio suala la vifaa, utaalamu n.k vinapokuja.

Wapo wanaoitwa makamanda katika siasa za Tanzania; na hasa katika chama kikuu cha upinzani CDM. CDM wameaminisha umma wa Watanzania kuwa wao "wapiganaji" wanataka kweli kuiondoa CCM madarakani. Mengi yanasemwa na mengi yanaahidiwa. Tunachoshuhudia sasa hivi na kwa muda kidogo sasa kunafanya tuhoji kama zipo brigedi zilizoasi, kamandi zilizopoteza amri, au kama kuna makomandoo ambao wameenda rogue! Majibizano kufuatia amri ya Kamati Kuu na jinsi ambavyo vikundi mbalimbali - wenyewe wanajiita wapiganaji - vinajitokeza kupingana vyenyewe kwa vyenyewe na hasa tukishuhudia kile ambacho tunaweza kuita MHC ya kisiasa imegawanyika inabidi tubakie na swali ambalo tayari limeshaulizwa na wengine vile vile.

Je, bila nidhamu tunaweza kushinda kweli? Bila kuwa pamoja kwa malengo na harakati adui anaweza kushindwa kweli? Je, kuna uwezekano wapiganaji wakaamua kujipigania vita vyao vyenyewe bila kujumuisha harakati zao na zile za jeshi zima? Je, makamanda wenyewe wanapowekeana bunduki vichwani mwao huku wakitunguana wenyewe kwa wenyewe kama watu wanaotungua tetere kwenye nyaya za umeme kweli kuna matumaini ya kushinda vita? Siyo kwamba tutafika kwenye final stand hatuna mtu wa kurusha risasi ya mwisho? SIyo kwamba tutajaribu kusonga mbele vitani huku kila kamanda anachechemea na wapiganaji wa vikosi mbalimbali wanatoka damu wengine wakiwa wameangamizwa na risasi za wenyewe kwa wenyewe (friendly fire)?

Wazo.

MMM

Ni bahati sana kukuta Jeshi ambalo makamanda wake wana nidhamu ya dhati. Kunakuwepo na makamanda ambao wako jeshini kwa ajili ya kulilinda taifa na kuna makamanda wako kwa ajili ya maslahi binafsi. Hata UPDF wana watu kama kina Kiiza Besidgye! Kinachofanyika ni kuwashauri watoke waanzishe majeshi yao kwa maslahi binafsi au kuwatosa.
 
Chanzo ni CCM kutaka kuiangamiza CDM kupitia mamluki wake ndani ya CDM hivyo immediate action ni ku castrate hicho chanzo ambacho kinahusishwa na nidhamu mbofumbofu ndani ya jeshi na vita itaendelea kukiwa na amani ndani ya wapiganaji

Hapa unawakilisha tabia halisi ya Watanzania, [ na binadamu wote?], tatizo likitokea tunatafuta kwanza mchawi kutoka nje, labda kwa Chadema sio hivyo [wishful thinking].
 
Mfano wa Jeshi na Chama cha Siasa ni mfano mfu- JESHINI NI AMRI TU, UTAKE UNAFUATA USITAKE UNAFUATA HAKUNA DEMOKRASIA KULE. KWENYE CHAMA, TENA KINACHOITWA CHA DEMOKRASIA KUNAFUATWA DEMOKRASIA, KUNA KUHOJI, KUNA KUFANYA SIASA NA MIPANGO ILI UMSHINDE MWENZIO KWENYE CHEO CHAKE.

BAHATI MBAYA MAKALA YA MWANAKIJIJI INAJARIBU KUMSINGLE OUT ZITTO NA WENZIWE KWAMBA "WASIO NA NIDHAMU", SIJUI ANATAKA WAWE NA NIDHAMU KWA MUJIBU WA NIDHAMU ANAYOIJUA MBOWE AU NIDHAMU KWA MUJIBU WA KANUNI NA SHERIA ZA CHAMA?.

HATA KAMA UMEAMUA KUCHAGUA UPANDE, KUWA MUWAZI TU ILI TUKUULIZE MASWALI MAGUMU, YA USHSHIDI UTHIBITISHO WA TUHUMA ZINAZOMKABILI MH ZITTO. USIKWEPE STAND UP AND BE COUNTED.

Wakati MM amejikita katika kukichambua chama cha CHADEMA kwa ujumla hasa Kamandi yake kuu, wewe unataka kumlazimisha aingie katika mjadala wa "for or against Zitto". MM amejikita katika "issues", wewe unamlazimisha ajadili "personalities". wakati wewe unataka kuonesha kwamba CHADEMA si lolote, hasa kwa sababu ya maamuzi waliyoamua kufanya, MM anajaribu kuangalia tatizo liko wapi na kushauri wafanye nini. mimi naona hiyo ni mitazamo miwili tofauti. sana sana ungechangia katika hayo mawazo aliyoyajadili, ama kwa kuyakosoa au kwa kuyaunga mkono. hapo umekuja na mada nyingine kabisa
 
ni kweli bila nidhamu jeshini hakuna ushindi , sasa tunafanyaje ili kumteketeza adui ? Dawa pekee ni kwa kamanda aliyepewa mamlaka kuwaondoa maaskari wasio na nidhamu ndani ya vikosi na kuwarejesha kambini kwa hatua zingine .
 
Jeshi ambalo kamanda anamshabikia adui kwavile tu anamshambulia kamanda mwenzake asiyempenda...

All in all kama kuna makamanda CHADEMA lema is not one of them ni muhuni flani aliyetakiwa kuwa street fighter huko,atatuuza huyu kwenye uwanja wa vita...

LEMARR ni hatari sana. Hapo ndo najiuliza ilikuwaje CDM wakamruhusu kugombea kwa tiketi yao. Mwenendo wake uraiani wajulikana sana huko ARSH. Mtandao wake wa wizi wa magari ya watu unafahamika na yeye ndo kiongozi na mfadhili mkuu wa mtanadao huo hata kamanda wa Mkoa husika hata HQ polisi naamini wajua. Sasa huyu mtu kuwa katika CC ya CDM kulikoni? Kweli CDM kuna seriousness? Lazima umafia wake atauhamishia CDM. CHUNGA BWANA.
 
Kumbuka babu slaa kapigwa marufuku kukanyaga kigoma. ...imebaki mikoa 24 (kwa hesabu ya mikoa ya zaman)

KUDADADEKI yani JK ameweka idadi ya MIKOA hadi MACCM wenyewe hawajuhi ipo Mingapi, juzi nikasikia mwingine sijuhi KIGOMBE, keshi utasikia mwingine HANDENI, kesho kutw autasikia mwingine MSATA.
 
Mzee MM

Asante kwa bandiko lako fikirishi. Unataka kumaanisha kuwa 'jeshi' la CHADEMA halina nidhamu? Hata wewe unajua kuwa hiyo si kweli! Ukiwa na wapiganaji wachache wanaotaka/wanaoonekana/ wanaopata tuhuma za kuharibu malengo ya jeshi unasema jeshi zima!

Kinachoonekana kutokea ndani ya CHADEMA (kwa kusukwa au kutengenezwa na hata kuchezwa na many players), unastahili kuwa unaujua uhalisia wake!

Makene, wote tungependa kuamini hivyo, lakini kinachoonekana si hivyo. Viongozi wenu Kila mtu anatoa matamko ya kutofautiana na 'high command' bila woga wowote; mathalani tamko la mwenyekiti wa Kigoma kuhusu ziara ya Katibu Mkuu, unaona hiyo ni sahihi? Alishindwa nini kuwasiliana na makao makuu na kuwapa taarifa hizo badala yake anatoa press release. Haya yanaonekana Kila sehemu! Hizi ni dalili za jeshi lidilo na nidhamu na kwa hali hii hakuna atakayetoka mshindi - Kati ya Zitto na Mbowe.
 
Back
Top Bottom