Swali la Ugomvi: Jeshi Lisilo na Nidhamu Linaweza Vipi Kushinda Vita?

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,899
Likes
8,133
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,899 8,133 280
Mara nyingi utaona watu wanalisifia sana jeshi letu la Ulinzi hasa baada ya operesheni fulani. Mfano mzuri ni hili la kwenda DRC na kuwachakaza M23; licha ya kupoteza wapiganaji kadhaa jeshi letu bado limesifiwa kwa umahiri katika medani ya mapambano.

Kwa wale tulioshuhudia kwa karibu Vita ya Kagera na harakati za Ukombozi wa Nchi zilizoko Kusini mwa Afrika tunajua ni kwa kiasi gani jeshi letu lilijipatia heshima katika kushiriki mapambano, kutoa mafunzo na kulinda usalama wa nchi yetu. Kiasi kwamba tulijiaminisha kuwa jeshi letu ni mahiri kabisa katika eneo letu hili. Kutokana na ujuzi huo tumekuwa na kiburi cha ufahari wa jeshi letu; ndio maana tunapochokozwa na majirani zetu hatuchelewi kuanza kushadadia vita na mapambano kwa sababu tunaamini kabisa kuwa katika eneo letu hakuna nchi ambayo inaweza ikaingia vitani na sisi ikatupiga; siyo Malawi, siyo Rwanda wala siyo nani.

Siri ya mafanikio haya ya jeshi letu ni nini hasa? Je ni kwa sababu tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika vifaa vya kijeshi? (hili si kweli); je inawezekana ni kwa sababu tuna silaha za kisasa zaidi kuliko wengine? au kwa sababu sisi ni Tanzania kana kwamba kwa kuwa Tanzania basi automatically jeshi letu ni bora zaidi? Au kuna siri kubwa zaidi na ya msingi?

Naomba kupendekeza kwa msomaji kuwa siri ya mafanikio ya jeshi lolote duniani (likiwemo la kwetu) imelala kwanza kabisa katika nidhamu (discipline). Jeshi lisilo na nidhamu haliwezi kushinda vita hata kama lina silaha, wataalamu au mabilioni ya pesa. Vitu vingine ni muhimu sana katika kufanikisha mapambano lakini hakuna kitu muhimu kama kuwa na wapiganaji walio na nidhamu iliyopitiliza; ambao wanatambua majukumu yao barabara na ambao pamoja na makamanda wao wako moyo mmoja kutafuta ushindi. Hakuna brigedi, hakuna kikosi, hakuna company ambayo inaweza kusimama peke yake au kujifanyia mambo yake kwa ajili ya sifa zake yenyewe. Jeshi lote na sehemu yote chini ya majenerali husika ndio linaenda kutafuta ushindi. Jeshini hakuna sifa ya kikosi moja au kapteni mmoja!

Lakini ni hii nidhamu ndio msingi wa ushindi. Baada ya nidhamu hii ni ile hali ya kujitoa kwa lengo lililoko - total commitment to the cause. Mara baada ya lengo kuwekwa bayana -kumtambua adui na kupambana naye - vikosi vyote chini ya makamanda wao na wote hao chini ya kamandi kuu ya vita (Military High Command) vita vinaenda kupiganwa. Hiyo MHC nayo inapata maelekezo yake ya malengo ya kisiasa kutoka kwa viongozi wa kiraia wa nchi (civilian authorities) wakiongozwa na Amiri Jeshi Mkuu. Kutoka hapa ndio suala la vifaa, utaalamu n.k vinapokuja.

Wapo wanaoitwa makamanda katika siasa za Tanzania; na hasa katika chama kikuu cha upinzani CDM. CDM wameaminisha umma wa Watanzania kuwa wao "wapiganaji" wanataka kweli kuiondoa CCM madarakani. Mengi yanasemwa na mengi yanaahidiwa. Tunachoshuhudia sasa hivi na kwa muda kidogo sasa kunafanya tuhoji kama zipo brigedi zilizoasi, kamandi zilizopoteza amri, au kama kuna makomandoo ambao wameenda rogue! Majibizano kufuatia amri ya Kamati Kuu na jinsi ambavyo vikundi mbalimbali - wenyewe wanajiita wapiganaji - vinajitokeza kupingana vyenyewe kwa vyenyewe na hasa tukishuhudia kile ambacho tunaweza kuita MHC ya kisiasa imegawanyika inabidi tubakie na swali ambalo tayari limeshaulizwa na wengine vile vile.

Je, bila nidhamu tunaweza kushinda kweli? Bila kuwa pamoja kwa malengo na harakati adui anaweza kushindwa kweli? Je, kuna uwezekano wapiganaji wakaamua kujipigania vita vyao vyenyewe bila kujumuisha harakati zao na zile za jeshi zima? Je, makamanda wenyewe wanapowekeana bunduki vichwani mwao huku wakitunguana wenyewe kwa wenyewe kama watu wanaotungua tetere kwenye nyaya za umeme kweli kuna matumaini ya kushinda vita? Siyo kwamba tutafika kwenye final stand hatuna mtu wa kurusha risasi ya mwisho? SIyo kwamba tutajaribu kusonga mbele vitani huku kila kamanda anachechemea na wapiganaji wa vikosi mbalimbali wanatoka damu wengine wakiwa wameangamizwa na risasi za wenyewe kwa wenyewe (friendly fire)?

Wazo.

MMM
 
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
2,619
Likes
310
Points
180
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined Jan 6, 2012
2,619 310 180
Mzee MM

Asante kwa bandiko lako fikirishi. Unataka kumaanisha kuwa 'jeshi' la CHADEMA halina nidhamu? Hata wewe unajua kuwa hiyo si kweli! Ukiwa na wapiganaji wachache wanaotaka/wanaoonekana/ wanaopata tuhuma za kuharibu malengo ya jeshi unasema jeshi zima!

Kinachoonekana kutokea ndani ya CHADEMA (kwa kusukwa au kutengenezwa na hata kuchezwa na many players), unastahili kuwa unaujua uhalisia wake!
 
monoclinic

monoclinic

Senior Member
Joined
Nov 15, 2013
Messages
144
Likes
28
Points
45
monoclinic

monoclinic

Senior Member
Joined Nov 15, 2013
144 28 45
jeshi lisilo na msemaji...kila mtu anatoa tamko
lake kwenye mitandao ya jamii....

hakuna mgawanyo wa madaraka..kila mtu ni mtoaji tamko...
 
F

Fringe

Senior Member
Joined
Jul 5, 2011
Messages
178
Likes
1
Points
0
F

Fringe

Senior Member
Joined Jul 5, 2011
178 1 0
Kumbuka babu slaa kapigwa marufuku kukanyaga kigoma. ...imebaki mikoa 24 (kwa hesabu ya mikoa ya zaman)
 
Mwendabure

Mwendabure

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Messages
2,144
Likes
545
Points
280
Mwendabure

Mwendabure

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2011
2,144 545 280
tutavuka na hili... viva CDM!
 
monoclinic

monoclinic

Senior Member
Joined
Nov 15, 2013
Messages
144
Likes
28
Points
45
monoclinic

monoclinic

Senior Member
Joined Nov 15, 2013
144 28 45
kuvuka sio shida tunaweza kuvuka lkn ni wangapi???
na je hao walizama walistahili kweli?au kisa walikua wasumbufu wa haki safarini....

hakuna mwanasiasa yoyote wa kumuamini duniani hata mzazi wako....
 
Rapherl

Rapherl

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Messages
3,314
Likes
1,496
Points
280
Rapherl

Rapherl

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2012
3,314 1,496 280
Jeshi ambalo kamanda anamshabikia adui kwavile tu anamshambulia kamanda mwenzake asiyempenda...

All in all kama kuna makamanda CHADEMA lema is not one of them ni muhuni flani aliyetakiwa kuwa street fighter huko,atatuuza huyu kwenye uwanja wa vita...

Sent from BlackBerry 9520
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Likes
2,514
Points
280
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,514 280
Kuelekea ktk uchaguzi mkuu kutakuwa sana na makala km hizi .."Chadema watashida kilaini iwapo...blah blah na blah na blah..."
 
Ng'wamapalala

Ng'wamapalala

JF Gold Member
Joined
Jun 9, 2011
Messages
6,332
Likes
135
Points
160
Ng'wamapalala

Ng'wamapalala

JF Gold Member
Joined Jun 9, 2011
6,332 135 160
Neno Amiri Jeshi Mkuu ni unique na halipewi kwa mtu anayetafuta uzooefu katika medani za kisiasa na kivita. Hili neno linapewa mtu mwenye hekima, busara na uzoeefu wa changamoto za kisiasa na kivita kwa ndani na nje.

Ndiyo maana pale jeshi linapoona Amiri Jeshi Mkuu anashindwa kufanya kazi yake ipasavyo katika kuisimamia nchi katika vita vya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa maadui wa nje na ndani huwa linafikia uamuzi wa kumwondoa kidemokrasia na ikibidi huwa hata linafikia kutumia njia ya coup d'état kama hakuna njia iliyowazi katika kufikia malengo hayo kidemokrasia.

Ni ujinga na pia ni kukosa hekima na busara kwa Amiri Jeshi Mkuu kuiingiza nchi kwenye vita wakati anafahamu uwezo wa jeshi lake kupambana na adui ni mdogo na kikubwa zaidi anafanya hivyo bila kuipa na kuiacha diplomasia ichukue kwanza mkondo wake katika kutafuta chanzo na suruhu ya mgogoro.

Jeshi linapokosa nidhamu, kuna uwezekano mkubwa wa Amiri Jeshi Mkuu kutandikwa risasi na wanajeshi wake yeye mwenyewe kwa sababu hawana nidhani jeshini.

Is this CHADEMA?.

Yangu macho na masikio.
 
monoclinic

monoclinic

Senior Member
Joined
Nov 15, 2013
Messages
144
Likes
28
Points
45
monoclinic

monoclinic

Senior Member
Joined Nov 15, 2013
144 28 45
Jeshi ambalo kamanda anamshabikia adui kwavile tu anamshambulia kamanda mwenzake asiyempenda...

All in all kama kuna makamanda CHADEMA lema is not one of them ni muhuni flani aliyetakiwa kuwa street fighter huko,atatuuza huyu kwenye uwanja wa vita...

Sent from BlackBerry 9520

you might have a point somewhere...
jiulize haya
:> ilikua kuna haja gani ya lema kumtusi zitto kuwa ni mnafiki kwenye mitandao wakat wote ni wa baba mmoja.ivi wameshindwa kukaa chini nyumban kwao kuyamaliza....

kwa mwenye akili timamu tu utajua LEMA ni mfuasi wa nani ndani ya chadema... hivi wabunge wooote wa chadema hawakuuona unafiki wa zitto kwenye posho kuona Lema tu na kuamua kumtusi via mitandao?? yeye kama msemaji wa nani,, chama kipi?? bora hata angesema mnyika tungesema ni yupo idara ya habari

haya LEMA alishindwa vipi kuupeleka unafiki wa zito kwenye vikao vya chama viongozi wa ujadili..jaman acheni kufuata upepo watu wapo kazini mjue....
 
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Messages
9,853
Likes
1,264
Points
280
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2010
9,853 1,264 280
Mzee MM

Asante kwa bandiko lako fikirishi. Unataka kumaanisha kuwa 'jeshi' la CHADEMA halina nidhamu? Hata wewe unajua kuwa hiyo si kweli! Ukiwa na wapiganaji wachache wanaotaka/wanaoonekana/ wanaopata tuhuma za kuharibu malengo ya jeshi unasema jeshi zima!

Kinachoonekana kutokea ndani ya CHADEMA (kwa kusukwa au kutengenezwa na hata kuchezwa na many players), unastahili kuwa unaujua uhalisia wake!
HUjajibu swali

Jeshi lisilo na nidhamu kamwe haliwezi kushinda vita...

na nijuavyo mimi, waasi ndani ya jeshi wana mawili tu, kushughulikiwa au kuwa eliminated... jeshi si kama ndoa au ngoma; jeshi halina mchezo

Tuache siasa, kweny hii issue, waasi ndani ya jeshi lazima washungulikiwe na wasipewe tena nafasi jeshini wala kwenye viunga vya kambi

TUKUMBUKE KWAMBA SHIDA YA TANZANIA NI KUWEKA SIASA NA FITNA KILA SEHEMU... AND WE HAVE FAILED MISERABLY, UKIKUTANA NA VIJANA BAADHI WATASEMA BORA AJE DIKTETA TUTASHIKA ADABU, WELL, THIS IS THE OPPORTUNITY TO SHOW KWAMBA JESHI NA MAKAMANDA WAKO SERIOUS
 
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Messages
9,853
Likes
1,264
Points
280
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2010
9,853 1,264 280
you might have a point somewhere...
jiulize haya
:> ilikua kuna haja gani ya lema kumtusi zitto kuwa ni mnafiki kwenye mitandao wakat wote ni wa baba mmoja.ivi wameshindwa kukaa chini nyumban kwao kuyamaliza....

kwa mwenye akili timamu tu utajua LEMA ni mfuasi wa nani ndani ya chadema... hivi wabunge wooote wa chadema hawakuuona unafiki wa zitto kwenye posho kuona Lema tu na kuamua kumtusi via mitandao?? yeye kama msemaji wa nani,, chama kipi?? bora hata angesema mnyika tungesema ni yupo idara ya habari

haya LEMA alishindwa vipi kuupeleka unafiki wa zito kwenye vikao vya chama viongozi wa ujadili..jaman acheni kufuata upepo watu wapo kazini mjue....
LEMA ni radical tu, si mwanajeshi, si mwanasiasa wala si kiongozi.... kuna siku chadema watajutia kuwa nae

he has no control, nor understanding of what leadership is

Lema na zitto wote ni watu waliojiunga na siasa kama opportunists na wote hawana faida kwa nchi
 
haha..kwa vile hamna mifano hai ktk tamaduni zenu kuwa watu wanaweza kuwa na makubaliano ktk fikra moja na kufuata sheria moja.hakumaanishi ni lazima mtu awe mfuasi wa mtu.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,899
Likes
8,133
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,899 8,133 280
Kila jeshi duniani lina watu ambao wanakuwa na mambo yao na hata kulidhalilisha jeshi. TUnakumbuka Gereza la Abu Ghraib, au mauaji ya ile familia kule Afghanistan; hata hapa US kesi ya yule Daktari (major Nadar) aliyewaua askari wenzie. Hili si jambo jipya kuwa na askari rogue, waasi au pure rebels. Hata hivyo katika mifanano yote hiyo utaona kuwa ni ile nidhamu ya kijeshi inayosababisha hatua kali kuchukuliwa kwa wanajeshi. Juzi juzi Wamarekani wamemfunga yule kijana aliyeiba siri za Kidiplomasia ambazo zilichapishwa kwenye wikipedia (na siye wengine tukajua yale mambo ya suti!). Mwenyewe alisema anafanya hivyo kwa "maslahi ya taifa" lakini mahakama haikumuonea huruma; amekula kifungo cha maisha.

Lakini inapotokea kuwa kuna a systematic indiscipline ndani ya jeshi hakuna njia nyingine isipokuwa kuanza upya. Nyerere alifanya hivi na jeshi la KAR alilorithi kutoka Mwingereza (likawa Tanganyika Rifles) pale ambapo lilifanya uasi. Alichukua maamuzi ya lazima kulivunja jeshi na kuanza upya - japo wengine walikuwemo ndani ya jeshi la awali. Lakini kubwa alilosisitiza katika jeshi jipya (JWTZ) ni nidhamu.

Mifano hii itusaidie tu kutafuta njia nzuri ya kushughulikia matatizo yanayokabili upinzani sasa hivi hususan CDM. Vinginevyo hata wale wanaosema wanataka mabadiliko wao wakiingia madarakani watajikuta wanawatu wanawapinga vile vile na gurudumu hili halitakoma...
 
Ngongoseke

Ngongoseke

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2012
Messages
3,210
Likes
42
Points
145
Ngongoseke

Ngongoseke

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2012
3,210 42 145
Neno Amiri Jeshi Mkuu ni unique na halipewi kwa mtu anayetafuta uzooefu katika medani za kisiasa na kivita. Hili neno linapewa mtu mwenye hekima, busara na uzoeefu wa changamoto za kisiasa na kivita kwa ndani na nje.

Ndiyo maana pale jeshi linapoona Amiri Jeshi Mkuu anashindwa kufanya kazi yake ipasavyo katika kuisimamia nchi katika vita vya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa maadui wa nje na ndani huwa linafikia uamuzi wa kumwondoa kidemokrasia na ikibidi huwa hata linafikia kutumia njia ya coup d'état kama hakuna njia iliyowazi katika kufikia malengo hayo kidemokrasia.

Ni ujinga na pia ni kukosa hekima na busara kwa Amiri Jeshi Mkuu kuiingiza nchi kwenye vita wakati anafahamu uwezo wa jeshi lake kupambana na adui ni mdogo na kikubwa zaidi anafanya hivyo bila kuipa na kuiacha diplomasia ichukue kwanza mkondo wake katika kutafuta chanzo na suruhu ya mgogoro.

Jeshi linapokosa nidhamu, kuna uwezekano mkubwa wa Amiri Jeshi Mkuu kutandikwa risasi na wanajeshi wake yeye mwenyewe kwa sababu hawana nidhani jeshini.

Is this CHADEMA?.

Yangu macho na masikio.
Mkuu umemjibu vizuri sana,tunajua anachotetea hapa,kwa sababu anaaminisha watu kama kuna watu hawana nidhamu ndani ya chama,lakini akiwa kamlenga mmoja tu,kasahau waliomo ndani ndio chanzo cha utovu wa nidhamu,hivi gazeti la Tanzania daima likifungwa unadhani makala zake atauza wapi?
 
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
61,483
Likes
29,603
Points
280
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
61,483 29,603 280
Mnatapatapa tu, kujidai kuikuza chadema na kuitolea mifano ya jeshi na USA.

chadema kimenuka, hakuna zaidi!

Hukuyaona ya Mrema na Marando huko zamani? yalifikia tamati hivi hivi, kama tuonavyo sasa. Labda uwadanganye wasiokuwapo.

Chadema kimeshafanya kazi yake kama kilivyopangiwa na sasa ni wakati muafaka kuki-nyutralaizi. Hakuna zaidi.
 
Malafyale

Malafyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Messages
12,323
Likes
5,086
Points
280
Malafyale

Malafyale

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2008
12,323 5,086 280
Mnatapatapa tu, kujidai kuikuza chadema na kuitolea mifano ya jeshi na USA.

chadema kimenuka, hakuna zaidi!

Hukuyaona ya Mrema na Marando huko zamani? yalifikia tamati hivi hivi, kama tuonavyo sasa. Labda uwadanganye wasiokuwapo.

Chadema kimeshafanya kazi yake kama kilivyopangiwa na sasa ni wakati muafaka kuki-nyutralaizi. Hakuna zaidi.
You dreaming!

Madiwani Bukoba walimbishia Rais JK hadharani na CCM kikaogopa kuwafukuza!

Nape anasema CC-CCM imetoa siku 90 mafisadi wajiondoe CCM wenyewe na mafisadi wakajibu ataoondoka yy na kweli hadi leo wapo na kibaya zaidi wamepewa kamati muhimu mno Bungeni!

CCM ni chama legelege kinachowakumbatia wabakaji na walawiti!CHADEMA kwa maamuzi haya wanaonyesha wanakwenda kuichukua dola 2015!

Kigoma inasifika kwa kutuzalishia wana siasa wa hovyo hovyo na haya ya Zitto hayanishangazi!
 
taamu

taamu

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Messages
5,813
Likes
1,808
Points
280
taamu

taamu

JF-Expert Member
Joined Dec 11, 2012
5,813 1,808 280
Wanasiasa wa kigoma wamelogwa si mwamkumbuka kafulila kaharibu cdm yeye na zito kaenda nccr kataka kuleta mapinduzi.mi naona waanzishe miradi ya migebuka tu.mwingine kila siku anasema ---- you bungeni.ni puppets leka tu tigite.
 
UPIU

UPIU

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2012
Messages
602
Likes
17
Points
0
UPIU

UPIU

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2012
602 17 0
LEMA ni radical tu, si mwanajeshi, si mwanasiasa wala si kiongozi.... kuna siku chadema watajutia kuwa nae

he has no control, nor understanding of what leadership is

Lema na zitto wote ni watu waliojiunga na siasa kama opportunists na wote hawana faida kwa nchi
Nidhamu inaweza kuboreshwa na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutenda haki, kama Zitto ameadhibiwa kwa kudaiwa kushiriki kuuandaa waraka wa mabadiliko basi pia na Lema alipaswa walau kukemewa juu ya hatua yake ya kumkashifu Zitto mitandaoni. Lakini cha kushangaza Katibu Mkuu anamgongea "Like"
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,652
Likes
32,394
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,652 32,394 280
Sisi wengine hili tuliliona siku nyingi na tukalisemea humu!. Mimi nilisema, Chadema Haijajipanga ki mipango mkakati wa kushika dola 2015, but ni wishful thinker!.
Japo kwa tatizo ni baadhi ya askari wasionanidhamu, kiukweli tatizo kubwa ni weaknesses kwenye higher commands!.
Wengi badala ya kudeal na chanzo, the causative agents, wana concentrate na matokeo!.
Pasco
 
Forum statistics

Threads 1,251,864
Members 481,917
Posts 29,788,229