Swali la Ugomvi: CCM Inaweza Kutoa Mtu Anayeweza Kumzidi Kikwete?

Nakubaliana na wewe MwanaDiwani, SISIEM ina hazina kubwa sana ya viongozi .................... so far walioonyesha nia pamoja na onyo wako at least 7 (January, Ngereja, Sumaye, Sita, Membe, Wasira, Lowasa) ukichanganya na wale wa siku za nyuma kuanzia 1995, Mama Maghembe, Mzee Malecela, Mh. Lowasa, Prof. Mwandosya, Dr. Magufuri, Dr. Mwakyembe, Salim ................. list inaweza kufikia hata mia ikiorodheshwa. Bongo tuna hazina kubwa ya viongozi kuliko USA au China. US sometimes Democrat au Republican huwa hata hawafiki 10 kwa kila chama. SISIEM safari hii lazima tuset record kwenye Guinness book of records!! Namshauri Mangula aongeze dau la kuchukua fomu ili kutunisha mfuko wa chama!! Wewe Mzee Mwanakijiji huoni hiyo hazina ya viongozi SISIEM!!

Ccm hawana lolote wote wezi :thamani ya pesa inashuka kila kukicha
2/sifa ya pili ni kuagiza mali ghafi zote toka uchina htuna viwand
3/ imedumaza akili za watanzania mf kama wewe badala ya ktzama mbdala Wa ccm kwkuwa hawafai unawaz msaada ofa toka ccm
4/hospitali kuna manesi waliofeli form four na hakuna madawa
5/-wanakusanya tirioni 15 ,za maendeleo ni tirioni moja zilizobaki ni za mandazi na vitumbua
6/-kuua,kuteka na green guard Yao hiyo nykti za chaguzi
 
Last edited by a moderator:
Serious???? Huu uwezo wa kuongoza taifa mnaupimaje?????
Bora liendee????
Hapa sasa nakusoma.....
Really? Kuyumba kwa ccm ni kuyumba kwa nchi????? Bado mawazo haya hamjaachana nayo tu?????
I see.....

Hii ya kuyumba nchi nafikiri wana maana ya kuyumba tabaka maalumu la watu (wanaojifikiria ni wateule) watawala.
 
Tumekuwa na serikali ya kisanii, huyu mwenye record amekuwa msanii na mbaya zaidi

amepoteza kumbukumbu sahihi za utamaduni wa ccm katika kuandaa marais

kwakusahau utamaduni mpaka sasa ccm haiwezi kutoka hadharani nakusema wanahazina maana katika hazina kumejaa

mbumbumbu, wasanii na wababaishaji.
 
Fikiria jinsi Rais Kikwete alivyokuwa na ule "mtaji" wa kisiasa mwaka 2005; hivi kweli kuna mwana CCM anayeweza kudai hata kwa mbali kuwa ana rekodi ya uongozi iliyomuandaa kuwa Rais? Kumbuka akiwa na miaka 40 Rais Kikwete alikuwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini na akiwa na miaka 44 tu alikuwa Waziri wa Fedha; miaka 10 Waziri wa Mambo ya Nje... Kama anayetaka kuwa mgombea kupitia CCM hatomfikia JK kwa uzoefu, na maandalizi kwanini tuamini kuwa atakuwa ni mzuri na bora kuliko JK?
Kama uzoefu ulioorodhesha ndiyo kipimo mbona CCM wanao wengi tu, Magufuli, Mwandosya ni bashing yao. Labda tatizo ni kuwa hawajakaa katika Wizara za kufanana na aliokaa Mh Rais.
 

Hapa ninafuu kwa maana ya mchafu aliebainika, alitimuliwa mpaka madarakani, harufu yake imeaacha zaidi uchungu na

uzalilishaji kwa heshima ya mtanzania.nasasa anasaka urais kulipa kisasi na kuiba zaid. Nani asiyekumbuka sekeseke la

RICHMOND
na mikono ya Kikwete na Lowasa?
 
Rais wa 2015 hatatoka kanda ya kaskazini mwa tanzania kwa mujibu wa uvccm,na tamko lilitolewa mkoa wa pwani!kwa hiyo kaeni mkao wa kula maana mlishaliwa kwa miaka 10,na ili ule lazima uliwe-
 
Umerukaruka sana lakini umekiri mwenyewe ndani ya CCM hamna mwenye uwezo ama rekodi nzuri ya kiutendaji hvyo hoja ya Mzee MWANAKIjiji ipo sahihi.
Ndugu, hayo ni mawazo yako kwa sababu hujaelewa mantiki ya hoja yangu.

CCM kwa sasa haina mgombea Urais wa awamu ya tano kwa sababu muda wa kumpata haujafika lakini kinachofahamika ni kuwa, siku hiyo ikifika, basi wanachama wa CCM watamteua mwanachama wenye uwezo kuwa mgombea kupitia CCM ambaye probably ndiye atakuwa Rais wa awamu ya tano.
 
..kuna rekodi, halafu kuna achievements.

..JK alikuwa na rekodi[orodha ndefu ya nafasi alizoshika], lakini hakuwa na achievements.

cc Jasusi, Mzee Mwanakijiji, Kimweri, Gs-300, Kasheshe, Gagnija

Very well said, Same Hekaya bwana mdogo Makamba ametuletea, rekodi zake za kukutana au kuona kadha wa kadha vikifanyika,ukidadisi alichofanya yeye kama yeye hakuna.Ndio ugonjwa uliokuwepo Tanzania,Hatuna Viongozi, tuna watazamaji. ndio maana unakutana na zee zima linalalamika jukwaan, Serikali haifanyi hiki na kile, wakati liko kwenye cabinet.Unakutana na Raisi analalamika kwa nini tatizo flani halitatuliwi, EBO,WTF is this?alitaka katibu tarafa ndio alitatue?you don't get to be president then B**ch about it.You do things.

Ndio maan amara zote mie hutoa Mfano kuwa hawa viongozi tulionao, hata kikampuni mbuzi tu hata Interview hawawezi kupita, na ikitokea bahati mbaya wakapewa nafasi ya kuongoza private company,wangefukuzwa siku mingi tu.ni vile shareholders wa nchi ya TZ,wamelala.
 
Fikiria jinsi Rais Kikwete alivyokuwa na ule "mtaji" wa kisiasa mwaka 2005; hivi kweli kuna mwana CCM anayeweza kudai hata kwa mbali kuwa ana rekodi ya uongozi iliyomuandaa kuwa Rais? Kumbuka akiwa na miaka 40 Rais Kikwete alikuwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini na akiwa na miaka 44 tu alikuwa Waziri wa Fedha; miaka 10 Waziri wa Mambo ya Nje... Kama anayetaka kuwa mgombea kupitia CCM hatomfikia JK kwa uzoefu, na maandalizi kwanini tuamini kuwa atakuwa ni mzuri na bora kuliko JK?
Mzee Mwanakijiji, Nadhani mada kama hizi zinawapotosha wananchi zaidi badala ya kuwafundisha haki na fursa walopewa ktk demokrasia maana tunapofikiria kumchagua mtu badala ya kutazama Chama gani tunarudi nyuma zaidi ktk siasa na utawala wa Kijamaa ambao MTU ndio alikuwa Nyumba au Jembe la kisiasa.

nasema hivi kwa sababu Demokrasia inalenga kutupa mrengo wenye sera na Ilani bora zaidi hivyo kiongozi yeyote anayefaa ama kutazamwa uwezo wake basi utatokana na kiongozi huyo kuweza kusimamia sera na Ilani za chama hicho. Wao watamtazama mtu asokuwa kigeugeu, mwenye Uzalendo, Mwaminifu, mwajibikaji na kadhalika kulingana na imani yao. Na ndio maana tunapewa jina moja tu kutoka kila chama kwa sababu chama hicho kimemuona mtu huyo kuwa ndiye mwenye uwezo huo. Na ndio maana CCM wanaweza kumsimamisha January Makamba wakati sisi wengine tunamwona Magufuli mchapakazi na mzuri zaidi kumbe sii mzuri hivyo kutokana na uwezo wake kuongoza sera na Ilani za chama.

Kama tukianza kufikiria NANI ambaye anaweza kuwa na umaarufu kama wa JK na tukamfagilia basi bado tumelala usingizi wa Kijamaa ambapo mgombea alipewa alama ya Jembe au Nyumba maana uwezo sii wa chama tena bali anatazamwa mgombea kulingana na siasa za Kijamaa. Hivyo kama tunatazama CCM na tunaamini ktk sera zao basi hapo ndio tunaweza kumtazama kiongozi na wala hata siku moja tusipotoshe maana ya Leadership na Management. Na kumekuwa na fikra kubwa sana zinazolenga kumchagua Meneja wa Taifa letu badala ya Kiongozi.

Hivyo basi kwa yeyote watakaye tuletea CCM, kumbukeni sii chaguo lla wananchi bali chaguo la chama, nasi tutazame ni sera zipi na Ilani zipi zinazotulenga sisi wananchi ili kesho na keshokutwa wakivurunda tutanyoosha vidole vyetu ktk sera hizo na hata kuonyesha Udhaifu wa kiongozi huyo ktk utekelezaji wa sera hizo. Kuna vyama watatuletea mbora wa kuongoza mbio za mita 100 na wapo watakao tuletea kiongozi wa mbio za marathon! sisi tunamhitaji nani? ndio swali.. Na mnaweza sana kumuona JK kama kiongozi mbovu na dhaifu kwenu lakini ukweli utasimama kwamba JK katekeleza sera na Ilani nyingi za CCM kuliko viongozi walomtangulia ndani ya demokrasia hii. Je, hizi sera zililenga kumkomboa Mwananchi? hapo mtaamua wenyewe.

- Nawakilisha.
 
Huyu JK alianza mapema sana harakati zake za urais hivyo mimi nashangaa kuona kwanini CCM inawakatalia makada wake kujitangaza mapema pia vipindi na nyakati za kisiasa zimebadilika sana kupita kiasi hivyo ni ngumu sana kwa nyakati hizi kumpata au vyombo vya habari kupata na kumpamba mtu kama ilivyokuwa JK
 
..lakini wanasema sifa moja ya kijana ni kutokuwa na uzoefu.

..sasa kwa msingi wa hoja hiyo, tunatakiwa tutafute the least experienced kijana ndiyo tumpe uongozi.

cc Kimweri, Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Farudume
JokaKuu nimecheka sana, ahsante sana !
Ndio maana nimemwambia MM kuwa watu wanakereka kusikia rekodi, hapa ni ujana tu unaotakiwa.

Sasa na wewe JokaKuu unafanya spinning nyingine, eti atafutwe the least experienced kwasababu ana sifa ya ujana haswa! teh teh

Ninyi wazee, ''sisi vijana tumewakosea nini, mbona mnatusakama sakama"" tumeshasema ukiwa kijana ni sifa, inatosha.
Sasa mnafukunyua nini tena?
 
..kuna rekodi, halafu kuna achievements.

..JK alikuwa na rekodi[orodha ndefu ya nafasi alizoshika], lakini hakuwa na achievements.

cc Jasusi, Mzee Mwanakijiji, Kimweri, Gs-300, Kasheshe, Gagnija

Mkuu JokaKuu,

Shukran kwa kunirukubisha hapa jamvini...kitambo naliadimika,maana nimekinzwa kiduchu na hapa kibaruani!

Kwa kifupi, nakubaliana na hiyo bayana/hojayo njema ulotoa.

Tajaribu pia kupitia kwa undani takriban hoja zoote za Wanajamvi wanziwetu,zilizopo hapa jamvini...ili niweze kuchangia kwa uthabit!

Lakini la muhimu pia,tujaribu kuwa waangalifu zaidi,makini na wenye maono ya mbali!?...ili kuweza kuitendea haki hiyo CCM(ambayo nakhis Muheshimiwa Mwanakijiji anakusudia kuibeza!? Daah!)...na pia tuwe objective kwa yoote tunayokusudia kuyajadili kiundani hapa...ili tuweze kumtendea haki kimjadala na kimtizamo,Rais wetu Mtukufu Bwana Kikwete,au!?

Hapo kwenye bayana yako,nimependa jinsi gani umetahadharisha/umenyambua ule umuhimu wa sisi soote kutambua tafauti pana iliyopo baina ya record and achievement/s!?

Sasa,pia hizo achievement/s pia twaeza zigawa katika makundi kadhaa...kama tutaamua kwenda mbali zaidi!?

Pana baadhi ya wanziwetu/Watanzania na hata wale wa Mataifa mangineyo...waeza kuona pia yakua ile nafsi ya yeye Muheshimiwa Kikwete kuukwaa ule Urais wa nchi yetu...basi tayari ilishakua ni mojawapo ya personal achievements kubwa mno!?...na hata kwa wangi wa Watanzania waliom-support awamu zile zoote mbili, na wangineo mpaka kesho...basi nina hakika yakua wanakhis hivyo!?

Hata hivyo kwa fikra zangu chechefu nakhis, yakua ni muhimu pia kumpima yeye binafsi Rais wetu wa sasa Muheshimiwa Kikwete na wale Waheshimiwa wanziwake wangine walopita!?...yaani nakusudia wale Marais wetu woote walomtangulia tangia awamu ya awali ya Uhuru wetu!?...nakhis kama tutaweza/tutaamua/ kufanza hivyo,basi ndo itakua kipimo/barometer njema ya kufahamu kwa yakini,kama kweli yeye Rais Kikwete ameambulia ku-achieve lolote/chochote kwenye hizo awamu zake zoote mbili,au laa!?

Pamoja na kusema hivyo,pia nimejaribu kuwa makini katika kuzingatia zile nyakati tafauti Taifa letu lilipokua linapitia katika vipindi tafauti vya awamu zilopita (social,economic and political events)!?...za hapo nyumbani na hata katika pembe nyangine za kidunia...maana hali hizo zoote pia kwa namna moja amma nyangine zaliweza/zaweza pia kutusaidia kunyambua/kuhalalisha jinsi gani hizo achievement/s zilipatikana,zilishindikana au hata kuathirika!?

Pamoja na yoote nilojaribu ku-shrink...lakini bado hakuna justification itakayotuzuia/kutukataza, kutazama hizo achievement/s za Rais Kikwete kwa "kumpimisha"/kumlingania na wanziwake walomtangulia,au!?

Sasa, kabla sijakwacha kwasasa ndugu yangu...embu tutazame mfano kiduchu hapa!?

Pana wakti kitambo baadhi ya wanziwetu nje ya hunu-JF...nao walijaribu kutazama zile achievement/s za Rais Ali Mwinyi kiundani,miezi michache kabla hajamaliza zile awamu zake!?

Palitokea makundi tafauti kadhaa...wapo walomsifu mno na kunyambua zile walizoziona yakua ni achievements zake kadhaa!

Wapo pia walomuona yakua hakua makini kwenye misimamo yake...nakhis walikusudia yakua labda hakufikia ile full potential yake kwa kukiogopa kile kivuli cha Mwalimu/"Baba wa Taifa", wakti ule!? Daah!

Pia wapo walomuona yakua ati alikua ni Rais "mbovu" kabisa!?...na ati yakua hakufanza lolote la maana kwa nchi yake Duuh! Teeeh! Teeeh! Teeeh!

Kumbuka yakua, hizo groups zoote pia walitoa logical grounds/reasons kwa hizo well informed opinions and/or critical criticism zao!?

Lakini yeye binafsi Muheshimiwa Rais Ali Mwinyi...alitumia busara njema kwa kutumia fursa na nyakati mbalimbali...kuwapa majawaba wale walokua wakimbeza kwa kuzidhihaki zile achievements zake kadhaa...na takriban mara zoote,yale majawaba yake yalikua yamelenga kuwakumbusha Wananchi wake/Watanzania... yakua,ili kumtendea haki yeye binafsi Rais Mwinyi na pia kuzitendea haki ya kimijadala zile achievements zake "kiduchu"...basi aliwanasihi yakua shuruti pia watazame kiundani na kunyambua kule walipotoka/alipowakuta na alipowaacha!? Duuh!

Yaani hapa yeye Rais Mwinyi...alikusudia kusema yakua...je, mwawezaje kuzifahamu/kuzinyambua achievements zangu bila ya kupata kilinganio!? Yaani kwanini msipimishe na pia zile nyakati nilizokukuteni nazo ndani ya mikono ya "Baba wa Taifa"!? Daah!

Hata vyuoni,shuleni/skuli,si pia panakua na ile "pass mark"!?...ambayo ndo inakua kipimio cha achievement ya msomaji/mwanafunzi,au!?

Sasa, ndo maana nakhis ni vyema pia,ili kupata hizo achiement/s za Rais Kikwete(kama zipo!?...binafsi naamini yakua zipo nyingi mno!)...lazim tutambue je hiyo benchmark/pass mark ni nini/kipi!?...je hakuna athari zozote za kurithiwa kutoka kwenye zile awamu za wale Waheshimiwa/Marais wangine...ambazo labda pia zaezakua zimeondosha/zimeathiri ufanisi wa hizi awamu zake na kuondosha/kupunguza hizo achievements zake!?...au labda pia zimepelekea/zimesababishia kuongeza hizo "achievements" za Rais wetu wa sasa!?

Nimejitahidi mno kutumia hii mifano "local" kiduchu...maana wafahamu yakua mie "sipendi" mno kutumia ile mifano ya Western World,khasa inapokuja masuala ya majadiliano ya social and political ya yenye kukhusu haya Mataifa yetu maduchu...the so called developing World!?

Laiti kama si hivyo, ningalijaribu kutoa mfano yakua...je tutakua tunamtendea haki ipi Rais Baraka Obama, ikiwa tutaamua kutazama achievements zake(kama zipo/anazo!? Daah!)...bila ya kunyambua ni jinsi gani zile awamu mbili za Rais George Bush zilivyotendeka, na yapi aloyarithi yeye Rais Obama toka kwa Muheshimiwa mwanzie!? Daah! Teeeh! Teeeh! Teeeh!

Niwia radhi kwa kuzunguka mno kwenye hii bayana yangu kiduchu...yaani nimejaribu/nimejitahidi kuandika kwa tahadhari, maana nachelea nisijitoa impression labda yakua ati namshutumu au nampendelea yeyote kati ya hawa Marais wetu woote, tangia tumepata "Uhuru" wetu na mpaka kesho!?

Tuko pamoja ndugu yangu!

Ahsanta sana.

Ps; "Mzee Mwanakijiji"...niwia radhi,sikusudii asilan...kupotosha lengo,makusudio walaa maudhui ya mada yako hii!
 
Back
Top Bottom