Huwezi kusoma jibu ukatoa hitimisho amejibu swali gani. Hakuna kitu kama hicho. Soma swali, sio jibu, kujua ameuliza nini.
Assumption ya "alitaka kujua nini Sophia Simba amekifanya kutaka nafasi tena," haipo! Shyrose hajanukuliwa kuuliza hivyo.
Ni rahisi sana kuota makengeza ya haraka yanayoweza kuruka swali lililoulizwa, na kuona swali tunalofikiri, au tulilotaka liulizwe.
Inatakiwa discipline na juhudi kuondoa makengeza haya.
Kwa mujibu wa maandishi tuliyopewa hapa - naenda kwa kuamini kilicholetwa hapa kimeletwa accurately and "in good faith" maana sina zaidi- ni kwamba Shyrose kahoji kwa nini Sophia Simba haonekani majukwaani kutetea chama.
Wengine wanaweza kutaka kupenyeza hili katika moja ya "nini alofanya kutaka nafasi tena", lakini wachunguzi zaidi watataka kuliweka katika ufinyu wake hakika, kwamba si swala nene la "nini umefanya" zaidi ya ufinyu wake ambao hata si "nini umekifanyia chama" (maana unaweza kufanya kazi za chama kimyakimya nyuma ya majukwaa).
Swali tuliloletewa ni.
"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."
Swali kama hili alishawahi kuulizwa Malecela (kwake swali lilikuwa kwa nini hasikiki bungeni kutetea wananchi?), akajibu kwamba kusikika sana hakumaanishi kufanya kazi sana, na kufanya kazi sana hakuna maana ni lazima usikike sana. Kimsingi kwamba yeye alikuwa anakata deal behind the scene huko na wapiga kura wake ndo wanajua kazi yake.
Sasa Sophia Simba hata kutoa jibu gracious lenye some semblance of coherence kashindwa.
Ndo anataka kuwa mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama tawala huyu!