Swali la Leo: Ukiona watu wanakimbia huku wanalia

Hapa kuna mantik! Kama mf. Wanatoka kusi kwenda kaskazi huku wanalia na wanakimbia ! Yawezekana Kusi kuna tatizo na kaskazi wendako kuna wokovu. Aidha yawezakua watokako ndiyo wameacha wokovu na wanakimbia kwenda kwenye balaa (ndiyo mana wanalia) bila hiyari yao! Wanakimbizwa. Solution hukurupuki mpaka uende na dira.
 
mimi ningetoa kamera yangu na kuwapiga picha, then nakuja kupost hapa JF.
 
Sijui hili kama ni utani ama la!
Nasikia kabila la Wanyakyusa wa huko Mbeya huwa mwanamke akisikia msiba mahali anaanza kwa kulia na kugaragara kwanza, labda kwa nusu saa hivi, kisha uchungu ukimpungua ndiyo anatulia na kuuliza.."Aliyefariki ni nani?"

Ni yule jogoo wetu mkubwa tunaetaka kumchinja kwenye sherehe ya Mwakitobe akimaliza shule 2014 amegongwa na bajaji ya Mwakaleli
 
Mhhhhhhh........hii ngumu ni sawa na kupiga jiwe ukitaraji muujiza wa kuchota maji.
 
nitakimbia na kulia nao ili tu wasigundue kuwa chanzo cha mbio zao na kilio chao ni mimi niliyejiunga nao....kuwapoteza zaid na kuwatia hofu waendelee kulia na kukimbia wasisimame kamwe.
 
Back
Top Bottom